Mba kichwani (Dandruff): Fahamu Chanzo, tiba na jinsi ya kuepukana nazo

Chukuwa Mshubiri Mwitu (aloe vera), ponda ponda, kamuwa juisi yake, paka kichwani kila siku. Hata kama una mapunye yataondoka.
 
Hivi wadau mba ni nini? Kitu gani husababisha mba za kichwani? Mfano mimi nina nywele fupi na ninajitahidi sana usafi lakini bado mba wananisumbua na kichwa huwa kinaniwasha nikijikuna na kitana unabaki ungaunga unaoashiria ni mba..je nifanye nini?
 
papaya.jpg



Mbegu za papai tiba ya mba
Pia mapapai yaliyoiva yanatibu mapunye (ringworm), mabichi yanatibu msukumo mkuu wa damu (high blood pressure), mapapai yanatumika kama mkuyati (aphrodisiac), yanatumika kama kituliza maumivu (analgesic), mbegu za mapapai zinapunguza maumivu ya tumbo (stomachache).

Mba au mabaka mabaka kwenye ngozi ni miongoni mwa mambo yanayosababisha ngozi kukosa muonekano mzuri na hata kumfanya mhusika mwenye matatizo kujikuta akijikuna kila wakati.

Kitaalamu mba ni aina mojawapo ya magonjwa yanayoambukizwa na fangasi ambao husababisha muwasho.


Wanawake wengi wanakumbana na matatizo haya ya mba, kutokana na kupaka aina ya vipodozi vinavyowaletea athari katika ngozi zao.

Unapokumbana na tatizo la namna hii ni vizuri kujipaka dawa zinazofaa badala ya kutafuta krimu ambazo ni hatari zaidi. Mbegu za papai ni tiba nzuri na ya asili ambayo haiwezi kukuletea madhara zaidi.

Jinsi ya kuondoa mba kwenye ngozi ya uso.

Mbegu za papai ni dawa ya asili inayoweza kutibu ngozi yako na kukuondolea tatizo la kuwashwa au mabaka yanayokukabili.

Namna ya Kutumia kama ni Dawa Mbegu za Papai.
Unachotakiwa kufanya ni kuzipondaponda na kujipaka kwenye eneo lililoathirika na mba. Hii itasaidia kuondoa ugonjwa huo na kuiacha ngozi yako ikiwa safi na yenye afya nzuri.

Unaweza kutumia krimu maalum za kuondoa mba hizo, zinapatikana katika maduka ya dawa, lakini unachopaswa kufanya ni kufuata masharti na kupaka kwa umakini kwenye sehemu ilioathirika.

Waweza pia kutumia sabuni maalum ya maji, shampoo, poda na hata baadhi ya losheni zote hizi zinaweza kuisafisha ngozi yako na kuifanya iondokane na muwasho unaokukera na wakati huo kuiacha ngozi yako ikiwa safi na yenye kuvutia. tumia kisha unipe feedBack Mkuu Pumb
 
Last edited by a moderator:
Osha/ sugua ngozi yako ya kichwa na shampoo iliyoandikwa anti-dandruff, kila unapooga.

Hakikisha unatumia hair food(mafuta special ya ngozi ya kichwa)baada ya kuoga.

Nadhani Unga unatokana na kushare vitana, taulo, kutopaka mafuta au pia kutoiosha na shampoo scalp yako.
pia inawezekana kuwa mafuta unayotumia si bora/ hayaendani na ngozi yako.

Hivi wadau mba ni nini? Kitu gani husababisha mba za kichwani? Mfano mimi nina nywele fupi na ninajitahidi sana usafi lakini bado mba wananisumbua na kichwa huwa kinaniwasha nikijikuna na kitana unabaki ungaunga unaoashiria ni mba..je nifanye nini?
 
Pole nenda duka la vipodozi nunua mafuta yanaitwa Sulphur 8. Ni mazuri sana ni mafuta mazito ya nywele pala kila siku asubui after three days utaniambia
 
hata mimi naugonjwa huu ila tiba ndo tatizo kila mtu anasema yake. Nitajieni mafuta mazuri au shampoo kwa nywele
 
Hivi wadau mba ni nini? Kitu gani husababisha mba za kichwani? Mfano mimi nina nywele fupi na ninajitahidi sana usafi lakini bado mba wananisumbua na kichwa huwa kinaniwasha nikijikuna na kitana unabaki ungaunga unaoashiria ni mba..je nifanye nini?
Mba ni fangasi za kichwani iliyodumu kwa muda mrefu mkuu,(chronic fungal infection-tinea capitis)
Utapata maambukizi ya fangasi za kichwani kwa kushirikiana kwa mfano chanuo au taulo na mtu ambae tayari ana maambukizi, na pia inaweza kusababishwa na uchafu wa muda mrefu katika nywele.

 
Nawashukuru sana wadau wote mliochangia, naomba muda niufanyie kazi ushauri wenu, nitawapa matokeo. God bless u all!
 
Nawashukuru sana wadau wote mliochangia, naomba muda niufanyie kazi ushauri wenu, nitawapa matokeo. God bless u all!
Na mimi pia ninashukuru kwa kutuletea shukrani kwako usikose na kuweka (like) ninakuongezea dawa nyingine ya Mba mkuu Pumb Mba hutokana na ngozi iliyokufa katika kichwa yaani dead cell.Dawa zilizopo ni :


Ndimu au limau: Kabla kwenda kukoga jisugue limau ndani ya kichwa na baadae yale maganda ya limau yatie katika maji ya kukoga yaani yawe dafi dafi halafu ukoshe kwa maji yale kwanza na baadae utumie maji yaliyo safi.

Fenugreek kwa lugha ya kiswahili inaitwa Uwatu . Hii unachukua vijiko 2 vya chai vya Uwatu (fenugreek) unazirowesha katika maji usiku mzima ili zipate kulainika, halafu unaziponda ponda na baadae unapakaa ndani ya kichwa na uwache kwa muda wa saa moja na baadae kuzikosha ikiwa utafanya hivi siku zote mbaa wataondoka Inshallah bila tabu yoyote. tumia kisha uje unipe Feedback.


707px-Fenugreek-methi-seeds.jpg

Fenugreek Uwatu.
 
Last edited by a moderator:
Nenda kwenye duka la vipodozi kanunue sulphur 8 spray halafu utaniambia kuna wakati mwingine ngozi inawasha hamna mba ila ukitumia hiyo spray ya sulphur 8 no mba no kuwasha utakuja kunieleza
 
Nivyema kujua type gani ya fungs ambao unao inaweza ikawa ni candida au tenia or even cryptococcus spp, na dawa huwa zinaweza kuwa wit higher spectrum yan kutibu fungus wa aina mbalimbali lakin zisilete mafanikio yoyote. kuna dawa nyingi za fungus, kwamfano econozole, muconozole, cotrmozole, mycostatin, griveline. Lakin nivizur kutambua fungus ulio nao ili upate dawa sahih yenye doz sahih. Fika hospital kwa vipimo itakusaidia.
 
Amani kwenu wote.

Ninakerwa sana na tatizo la kuwa na mba kwa kiasi kikubwa kwenye nywele za kichwani. Hii ni tangu nikiwa mtoto mdogo. Nimejaribu njia mbalimbali bila mafanikio;
  • Nimejaribu dawa mbalimbali, kuna zile dawa za cream/za kupaka kama vile Candisdat na nyinginezo
  • Nimejaribu dawa fulani wanauza kwenye vichupa imeandikwa "Dawa ya Mba", ni ya kijani, na naona nia jamii ya Spirit/Alchols..
  • Mwishoni mwa mwaka jana niliamua kunyoa upara kwa wembe kama mara tano mfululizo huku nikitumia dawa hizo, lakini tatizo lipo palepale.

Mba ni kwa kiasi kikubwa sana, hata nikikuna kichwa kidogo tuu unamwagika, I hate this.
Pia huwa napatwa na fungus miguuni lakini siyo wakati wote, kuna kipindi tuu huwa wanatokea, then wanaisha, na wanatokea tena kipindi fulani.

Nitashukuru sana kama kuna mtu ananisaidia kupata ufumbuzi wa hili, linaniudhi sana.
Asanteni.
 
Kwa suala la mba, nikushauri kitu kimoja. Kila siku uogapo, safisha kwa maji ya kutosha nywele zako. Acha povu la sabuni kama dk 2 hivi. Then suuza, paka povu mara ya 2. Ni vizuri kuwa na medicated soap. Tumia family soap.

Kwenye saluni unaponyoa, hakikisha anafuta vizuri mashine, epuka kuchangia kitu kama chanuo nk.

Kwa uelewa wangu, na uzoefu pia, mba ni matokeo ya uchafu kwa kiasi fulani.

Kuhusu dawa ya fangasi wa miguu, kamwe usivae soksi mara 2. Uwe na pea kama kumi hivi.

Pamoja na hilo tumia dawa hii 'Clotrimazole Cream USP- CLOB' Ni nadra kuipata na mara nyingi famasi wanakupambikia kwani Clotrimazole zipo aina nyingi. Fangasi itakuwa history.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom