Dawa ya maralia jamani

Nalonga

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
225
53
Habari Wanajamii,Tafadhalini ndugu naomba mnijurishe dawa bora ya maralia kwa mtoto chini ya mwaka mmoja, ambaye ni mara yake ya kwanza kuugua maralia,ipatikanayo hapa nchini Tanzania.

Nitashukuru sana iwapo pia nitafahamishwa Hospitali yenye daktari bingwa wa watoto hapa nchini Tanzania.

Asanteni sana
 
Kama upo Dar nenda hospitali ya Rufaa Muhimbili la kama haupo Dar mji wowote ulipo nenda kwenye Hoıspitali kuu ya mji uliopo utakutana na Ma doctor mabingwa wa matatizo ya watoto huo ndio ushauri wangu
 
Tiba ya Malaria Tiba ya Malaria inategemea mambo kadhaa: * Hali ya mgonjwa (mtoto, mama mja mzito, mtu mzima, ni kali ama sio kali) * Nguvu ya dawa dhidi ya ambukizo l

a viini vya plasmodium. * Eneo la kijiografia ambalo mtu aliambukizwa. Kwa mfano, P.falciparum inayopatikana katika nchi za Mashariki ya kati inaweza kutibiwa na dawa ya

chloroquine, lakini inayopatikana Africa, katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara haitibiki kwa chloroquine. * Aina ya plasmodium inayodhuru mgonjwa. Malaria yasiyo

makali hutibiwa na dawa za kumeza ilhali wagonjwa wenye P. falciparum kali hulazwa hospitalini na kupewa sindano ya maji. Kwa bahati mbaya aina fulani za plasmodium zimeleta upinzani dhidi ya dawa ya chloroquine.
 
Naweza jilinda vipi dhidi ya Malaria?

  1. Msafiri: Kama unasafiri hadi kwenye eneo linalolotambulika kwa Malaria,mtembelee daktari wako ili akupe dawa mahsusi ya kupambana na Malaria ya eneo unalotembelea.Hakikisha umefuata maelezo vizuri.
  2. Wenyeji wa maeneo yalioadhirika na Malaria: Mbu wa aina ya anopheles hupenda kuuma watu nyakati za macheo na machweo kwa hivyo ni bora kujikinga nyakati hizi.Wakati wa machweo unaweza keti ndani ya nyumba iliyoekewa dawa na usiku unaweza kulala neti iliyotibiwa.
  3. Haribu sehemu mbu wanapozaliana: Kipindi cha mwisho katika ukuaji wa mbu hufanyika majini.Mbu wa aina ya anopheles hupendelea maji yasiyo ya chumvi.Ni muhimu kuharibu ama kunyunyuzia na dawa sehemu zote ambazo mbu wanaweza kutaga mayai.Unafaa kutoa chupa,ndoo ama chochote ambacho kinaweza kusimamisha maji,bacillus thuringiensis(Bti) dawa asili ya kuua wadudu kutoka BioVision inaweza kutumiwa kuua mbu wachanga bila kuharibu maji.
  4. Watoto na mama waja wazito lazima wakingwe na Malaria: Nchini Kenya,wanawake waja wazito wana haki ya kupata matibabu 2 ya bure na neti zilizotibiwa. Chukua moja kutoka katiki kliniki yako.
  5. Neti zilizotibiwa: Kila mtu anapaswa kupata neti iliyotibiwa.Kuna aina mbili ya neti hizi nchini Kenya ambazo zinauwa mbu pindi tu wadudu hawa wanapozigusa.Kuna zile zinazopaswa kutibiwa kila baada ya miezi 6nba PowerTabs na zile zinazodumukwa miaka 3 hadi 5 baada ya kutibiwa
 
Nani yuko kwenye hatari ya kuambukizwa Malaria?

Watoto wachanga,watoto na akina mama waja wazito wako kwenye hatarikubwa ya kushambuliwa hata kufa kutokana na Malaria. Watoto wachanga na

watoto wako kwenye hatari kwa sababu wameambukizwa mara chache nahawajajenga kinga dhidi ya chembechembe hiziVamizi la Malaria kwa wanawake wajawazito kalikwa

sababu kinga yao dhidi ya maradhi huwa chini wakati wa uja uzito. Malaria huongeza

tishio kwa mtoto ambaye hajazaliwa kama kuzaliwa kabla ya wakati kutimia, uaviaji wa mimba, maambukizi ya sehemu za siri, uzani mdogo wa mtoto anapozaliwa, kupoteza uja uzito na pia ugonjwa huu unaweza kumsababishia mama kifo.

Malaria hutambulika vipi?

Baridi,kuuma kwa misuli na kichwa zinaweza kuwa dalili za magonjwa mengi mengine. Njia ya pekee unayoweza kudhihirisha kama una Malaria ni kuenda

hiospitalini kupimwa damu. Watu wengi wanaotoka sehemu zilizoadhirika na Malaria pindi wanapoona dalili hizi huenda kwenye maduka ya kuuza madawa kununua dawa

za kupambana na Malaria. Huu sio ushauri mzuri. Ni muhimu kupimwa damu ili aina ya plasmodium inayosababisha maradhi yako itambulike na upewe matibabu yanayostahili.
 
Habari Wanajamii,Tafadhalini ndugu naomba mnijurishe dawa bora ya maralia kwa mtoto chini ya mwaka mmoja,ambaye ni mara yake ya kwanza kuugua maralia,ipatikanayo hapa nchini Tanzania,Nitashukuru sana iwapo pia nitafahamishwa Hospitali yenye daktari bingwa wa watoto hapa nchini Tanzania.Asanteni sana

Wewe unaonekana hapa ni mgeni.....
 
Wewe unaonekana hapa ni mgeni.....

mkuu ugeni wake unahusiana na nini tena?kaomba msaada sehemu husika tumpe majibu kama ndugu yetu mzizimkavu alivyotanguia kumshauri na mm na msisitizia afate ushauri wake
 
Naweza jilinda vipi dhidi ya Malaria?

  1. Msafiri: Kama unasafiri hadi kwenye eneo linalolotambulika kwa Malaria,mtembelee daktari wako ili akupe dawa mahsusi ya kupambana na Malaria ya eneo unalotembelea.Hakikisha umefuata maelezo vizuri.
  2. Wenyeji wa maeneo yalioadhirika na Malaria: Mbu wa aina ya anopheles hupenda kuuma watu nyakati za macheo na machweo kwa hivyo ni bora kujikinga nyakati hizi.Wakati wa machweo unaweza keti ndani ya nyumba iliyoekewa dawa na usiku unaweza kulala neti iliyotibiwa.
  3. Haribu sehemu mbu wanapozaliana: Kipindi cha mwisho katika ukuaji wa mbu hufanyika majini.Mbu wa aina ya anopheles hupendelea maji yasiyo ya chumvi.Ni muhimu kuharibu ama kunyunyuzia na dawa sehemu zote ambazo mbu wanaweza kutaga mayai.Unafaa kutoa chupa,ndoo ama chochote ambacho kinaweza kusimamisha maji,bacillus thuringiensis(Bti) dawa asili ya kuua wadudu kutoka BioVision inaweza kutumiwa kuua mbu wachanga bila kuharibu maji.
  4. Watoto na mama waja wazito lazima wakingwe na Malaria: Nchini Kenya,wanawake waja wazito wana haki ya kupata matibabu 2 ya bure na neti zilizotibiwa. Chukua moja kutoka katiki kliniki yako.
  5. Neti zilizotibiwa: Kila mtu anapaswa kupata neti iliyotibiwa.Kuna aina mbili ya neti hizi nchini Kenya ambazo zinauwa mbu pindi tu wadudu hawa wanapozigusa.Kuna zile zinazopaswa kutibiwa kila baada ya miezi 6nba PowerTabs na zile zinazodumukwa miaka 3 hadi 5 baada ya kutibiwa

Asante sana mkuu,ushauri wako nitaufanyia kazi.
 
Back
Top Bottom