Mapunye: Fahamu kuhusu chanzo, tiba na athari zake kwa ngozi yako

JamboJema

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,143
209
1579181124688.png

Wanangu wameugua mapunye (vibarango) na nimetumia dawa nyingi bado naona hawaponi. Nitumie dawa gani ambayo haishindwi?

SAME CASES:
Wakuu kwa wale wataalamu naomba endapo kuna dawa kiboko ya kuponyesha mapunye yanayojitokeza kichwani. Nina watoto mmoja miaka 4 na mwingine miaka 9. Wanasumbuliwa sana; nimejaribu dawa nyingi za kupaka pamoja na sabuni(medicated soaps) lakini kupona hakupo! Msaada tafadhali.
---
Habari wadau?
Mimi nina mtoto wa mwaka mmoja ambaye amepata punye eneo la kisogoni,punye hilo kalipata tangu akiwa na miezi 9,nimempeleka hospitali tukaandikiwa dawa atumie lakini bado halijapona,pia nimempa syrup ya minyoo last week lakini tatizo liko palepale,naomba msaada tafadhali.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
---
Habarini wana jf,

Nina tatizo limenipata kama wiki 3 zimepita sasa mgongo wangu umepata vishilingi ama mapunye sikuwa nikijua sababu sijioni''nimeshtuka majirani kunambia vimevimbavimba hata mtu akiwa mbali kidogo anaviona.

Japo haviwashi unless nikae kwenye joto

Tafadhali JF doc naweza tumia dawa gani ya kupaka ama vidonge

Asante!

UGONJWA WA MAPUNYE
Mapunye ni aina ya magonjwa ambayo hushambulia keratini zinazopatikana katika nywele hasa za kichwani. Fangasi aina ya Dermatophites husababisha ugonjwa huu.

USAMBAAJI
Kusambaa kwaugonjwa huu ni pamoja na Kutumia vifaa vya nywele kama chanuo la kuchania nywele kwa zaidi ya mtu mmoja hususan pale ambapo mmoja wa watumiaji hao ana maambukizi ya vimelea vya fangasi hao.

-Kugusana na mtu aliye na maambukizi tayari -Kushirikiana mavazi aina ya kofia na mtu aliyekwisha pata maambukizi hayo.

WANAOWEZA KUUPATA UGONJWA HUU
  • Watu wachafu.
  • Wale wanaoshirikiana na wenzao vifaa vya kunyolea bila kuvisafisha vizuri
  • Wanaoshirikiana vifaa vya kufanya usafi wa mwili zikiwamo taulo
  • Wanaofanya kazi zinazohusisha uwekaji vichwa kwenye maji yaliyotuama kwa muda mrefu
  • Wale ambao tayari wana fangasi za kichwani kwani ni rahisi kwa fangasi hao kujirudia.
  • Wanaofanya usafi wa mwili kwa kutumia maji yaliyobeba vimelea
  • Wasiojikausha vichwa baada ya kuoga au kufanya usafi wa kichwa
  • Watu wenye maradhi yanayosababisha kushuka kwa kingaikiwamo kisukari.
  • Wale wanaokunywa dawa za kuua vimelea (antibayotiki) kwa muda mrefu
  • Watoto wadogo ambao hawajafikia umri wa balehe.

DALILI ZA UGONJWA
Mara nyingi aina hii ya fangasi hugundulika kwa macho hasa kwenye maeneo ambayo fangasi hao wapo kwa wingi. Kwa kutazama ngozi ya sehemu ya kichwa iliyoathirika na maambukizi ya fangasi hao, utaweza kuona madhara yanayokukabili.

MATIBABU
Mara nyingi mapunye hutibika kwa dawa za kutibu fangasi za kupaka ambazo hutibu mapunye na kuyaponyesha kabisa bila kuhitaji kutumia dawa za kumeza. Hii ni kwa kuwa ni rahisi kwa dawa ya kupaka kupenya kwenye ngozi na kusababisha matokeo yanayohitajika.

Jinsi ya kujikinga
Kuna mbinu mbalimbali za kujilinda usipatwe na fangasi:
  • Hakikisha mwili wako hasa kichwani yanabaki na ukavu muda wote
  • Osha nguo, taulo na mashuka kuhakikisha fangasi wanaondolewa
  • Epuka kushirikiana vifaa vya kunyolea nywele hasa kama hakuna namna ya kuvisafisha na dawa maalum ya kuua vimelea kabla hujatumia
  • Epuka kushirikiana katika utumiaji wa vifaa vya kufanya usafi wa mwili kama mataulo. Kama kazi yako inahusisha ukaaji wa muda mrefu kwenye maji basi hakikisha unakausha mwili hasa sehemu za kichwa au uweke dawa ya kuzuia fangasi kwenye maji hayo.

MICHANGO YA WADAU:
dk_isaack.jpg

Na Dk Isaack Maro; Isaac.I.Maro@gmail.com.
KWA UFUPI

    • Mara nyingi mapunye hutibika kwa dawa za kutibu fangasi za kupaka ambazo hutibu mapunye na kuyaponyesha kabisa bila kuhitaji kutumia dawa za kumeza. Hii ni kwa kuwa ni rahisi kwa dawa ya kupaka kupenya kwenye ngozi na kusababisha matokeo yanayohitajika.
Mapunye ni aina ya magonjwa ambayo hushambulia zaidi sehemu ya kichwani mwa binadamu kama ambavyo tuliona wiki iliyopita ambako pia tuliona aina zake, sabu na jinsi yanavyosambaa. Leo tuendelee na sehemu ya pili ambayo inamalizia na jinsi yanavyosambaa.

Ni pamoja na; Kutumia vifaa vya nywele kama chanuo la kuchania nywele kwa zaidi ya mtu mmoja hususan pale ambapo mmoja wa watumiaji hao ana maambukizi ya vimelea vya fangasi hao.

-Kugusana na mtu aliye na maambukizi tayari -Kushirikiana mavazi aina ya kofia na mtu aliyekwisha pata maambukizi hayo
Ni nani yuko hatarini?
Watu ambao huweza kupata maambukizi ya mapunye ni wafuatao:
-Wale wanaoshirikiana na wenzao vifaa vya kunyolea bila kuvisafisha vizuri
-Wanaoshirikiana vifaa vya kufanya usafi wa mwili zikiwamo taulo
-Wanaotoka jasho hasa kichwani kwani huweza kuweka mazingira mazuri zaidi kuruhusu maambukizi yatokee kirahisi
-Wanaofanya kazi zinazohusisha uwekaji vichwa kwenye maji yaliyotuama kwa muda mrefu
-Wale ambao tayari wana fangasi za kichwani kwani ni rahisi kwa fangasi hao kujirudia.
-Wanaofanya usafi wa mwili kwa kutumia maji yaliyobeba vimelea
-Wasiojikausha vichwa baada ya kuoga au kufanya usafi wa kichwa

-Watu wenye maradhi yanayosababisha kushuka kwa kinga ikiwamo kisukari.
-Wale wanaokunywa dawa za kuua vimelea (antibayotiki) kwa muda mrefu
-Watoto wadogo ambao hawajafikia umri wa balehe.

Jinsi ya kuyatambua
Mara nyingi aina hii ya fangasi hugundulika kwa macho hasa kwenye maeneo ambayo fangasi hao wapo kwa wingi. Kwa kutazama ngozi ya sehemu ya kichwa iliyoathirika na maambukizi ya fangasi hao, utaweza kuona madhara yanayokukabili.

Kwenye uhitaji wa vipimo basi sehemu ya ngozi iliyoathirika huchukuliwa kwa ajili ya kufanya vipimo vya maabara na kuangalia aina sahihi ya fangasi.

Matibabu
Mara nyingi mapunye hutibika kwa dawa za kutibu fangasi za kupaka ambazo hutibu mapunye na kuyaponyesha kabisa bila kuhitaji kutumia dawa za kumeza. Hii ni kwa kuwa ni rahisi kwa dawa ya kupaka kupenya kwenye ngozi na kusababisha matokeo yanayohitajika.

Matibabu ya mapunye huchukua muda mfupi kuonyesha matokeo mazuri.

Kama nilivyoandika kwenye makala zilizopita matibabu ya fangasi huleta matokeo chanya mara zote, ila pia huwa ni rahisi kwa maradhi hayo kurudi baada ya kumaliza matibabu kama hatua madhubuti za kujikinga na maradhi haya hazitochukuliwa.

Kwa sababu hiyo, ni vizuri kwa mgonjwa wa fangasi kutumia dawa mpaka wiki mbili baada ya dalili za maradhi kutoweka.

Jinsi ya kujikinga
Kuna mbinu mbalimbali za kujilinda usipatwe na fangasi:-Hakikisha mwili wako hasa kichwani yanabaki na ukavu muda wote

-Osha nguo, taulo na mashuka kuhakikisha fangasi wanaondolewa
-Epuka kushirikiana vifaa vya kunyolea nywele hasa kama hakuna namna ya kuvisafisha na dawa maalum ya kuua vimelea kabla hujatumia

-Epuka kushirikiana katika utumiaji wa vifaa vya kufanya usafi wa mwili kama mataulo. Kama kazi yako inahusisha ukaaji wa muda mrefu kwenye maji basi hakikisha unakausha mwili hasa sehemu za kichwa au uweke dawa ya kuzuia fangasi kwenye maji hayo.AFYA YA NGOZI : Mapunye na athari zake kwa ngozi yako-2 - mwanzo - mwananchi.co.tz

=====

Afya Kwa Ngozi : Mapunye Na Athari Kwa Ngozi Yako

Katika makala yetu Leo hii tunaangalia maradhi ya fangasi yanayoshambulia kichwa au mapunye ambayo kitaalam huitwa Tinea capitis.

Mapunye au Tinea Capitis ni nini?
Aina hii ya maradhi ya fangasi hushambulia eneo la kichwa pekee ukiacha eneo la uso. Kwa maneno mengine, aina hii ya fangasi haishambulii uso bali hushambulia eneo lililobaki la kichwa.

Huwashambulia kina nani?
Haya hushambulia watu wote wa jinsia na umri wote, ingawa huonekana zaidi kwa watoto wadogo. Fangasi hawa hushambulia watoto wadogo ambao hawajafikia umri wa balehe na mara nyingi huacha kushambulia pale mtoto anapofikia umri huo wa balehe.

Mwonekano wake
Mapunye huweza kushambulia eneo lote la kichwa au sehemu tu ya kichwa. Eneo la ngozi ambalo lina mashambulizi ya mapunye huwa na umbo linalofanana na sarafu.

Eneo hili la ngozi lililoathirika kama lina nywele, basi hunyonyoka na hivyo mwonekano wa mfano wa sarafu huonekana vizuri tu hata bila kutumia jicho la kitaalam.

Dalili zake
Ukiachilia mbali mwonekano wa mapunye kama nilivyoeleza hapo juu kuna dalili nyingine za maradhi haya. Hizo ni:
  • Eneo la ngozi lililoshambuliwa kuwasha (ingawa si mara zote)
  • Kubadilika kwa rangi ya ngozi ya eneo lenye maambukizi
  • Ukitazama kwa makini eneo ambalo lina mashambulizi ya maradhi haya utagundua kuna vidoti vyeusi ambavyo vinaonyesha eneo ambalo nywele imeng`oka kutokana na maradhi.
  • Ngozi kubanduka kwenye eneo lenye maambukizi
  • Ngozi kukauka kwenye eneo lenye maambukizi
  • Mara nyingine usaha pia huweza kuonekana kwenye eneo la ngozi lililoshambuliwa na fangasi hawa (hii kwa kitaalam huitwa kerions)
  • Kama maradhi haya yakikaa bila kutibiwa kwa muda mrefu husababisha dalili nyingine kuonekana kama kutoka kwa maji maji kwenye eneo la ngozi lililoathirika pamoja na kutoka kwa harufu mbaya kwenye eneo la ngozi lililoathiriwa na vimelea hivi vya fangasi.
Yanavyosambaa
Kuna njia nyingi zinazoweza kusababisha uambukizi wa mapunye lakini ili uambukizaji huu uwezekane lazima kuwa na mazingira rafiki ya kuwezesha fangasi kuweza kuishi na kuhama kwa urahisi. Mazingira haya rafiki kwa kuruhusu fangasi hawa kuweza kutoka kwenye kichwa cha mtu mmoja kwenda kwa mwingine huhitaji uwepo wa hali ya joto pamoja na majimaji (unyevunyevu).

  • Huwa ni rahisi sana kwa mapunye kuambukizwa kutoka kwenye kichwa cha mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia hizi:
  • Kutumia vifaa vya kunyolea kwa zaidi ya mtu mmoja bila kuvifanyia usafi wa kuua vimelea kama fangasi wa aina hii.
  • Kutumia taulo au nguo ya kujikaushia kwa mtu zaidi ya mmoja hasa pale ambapo mmoja wa watumiaji hao ana maambukizi ya fangasi.
  • Kutumia vifaa vya nywele kama chanuo la kuchania nywele kwa zaidi ya mtu mmoja hususani pale ambapo mmoja wa watumiaji hao ana maambukizi ya vimelea vya fangasi hao.
  • Kugusana na mtu aliye na maambukizi tayari
  • Kushirikiana mavazi aina ya kofia na mtu aliyekwisha pata maambukizi hayo
  • Ni nani yuko hatarini?
  • Watu ambao huweza kupata maambukizi ya mapunye ni wafuatao:
  • Wale wanaoshirikiana na wenzao vifaa vya kunyolea bila kuvisafisha vizuri
  • Wanaoshirikiana vifaa vya kufanya usafi wa mwili zikiwamo taulo
  • Wanaotoka jasho hasa kichwani kwani huweza kuweka mazingira mazuri zaidi kuruhusu maambukizi yatokee kirahisi
  • Wanaofanya kazi zinazohusisha uwekaji vichwa kwenye maji yaliyotuama kwa muda mrefu
  • Wale ambao tayari wana fangasi za kichwani kwani ni rahisi kwa fangasi hao kujirudia.
  • Wanaofanya usafi wa mwili kwa kutumia maji yaliyobeba vimelea
  • Wasiojikausha vichwa baada ya kuoga au kufanya usafi wa kichwa
  • Watu wenye maradhi yanayosababisha kushuka kwa kingaikiwamo kisukari.
  • Wale wanaokunywa dawa za kuua vimelea (antibayotiki) kwa muda mrefu
  • Watoto wadogo ambao hawajafikia umri wa balehe.

Jinsi ya kuyatambua
Mara nyingi aina hii ya fangasi hugundulika kwa macho hasa kwenye maeneo ambayo fangasi hao wapo kwa wingi. Kwa kutazama ngozi ya sehemu ya kichwa iliyoathirika na maambukizi ya fangasi hao, utaweza kuona madhara yanayokukabili.

Kwenye uhitaji wa vipimo basi sehemu ya ngozi iliyoathirika huchukuliwa kwa ajili ya kufanya vipimo vya maabara na kuangalia aina sahihi ya fangasi.

Matibabu
Mara nyingi mapunye hutibika kwa dawa za kutibu fangasi za kupaka ambazo hutibu mapunye na kuyaponyesha kabisa bila kuhitaji kutumia dawa za kumeza. Hii ni kwa kuwa ni rahisi kwa dawa ya kupaka kupenya kwenye ngozi na kusababisha matokeo yanayohitajika.

Matibabu ya mapunye huchukua muda mfupi kuonyesha matokeo mazuri au
Matokeo chanya mara zote, ila pia huwa ni rahisi kwa maradhi hayo kurudi baada ya kumaliza matibabu kama hatua madhubuti za kujikinga na maradhi haya hazitochukuliwa.

Kwa sababu hiyo, ni vizuri kwa mgonjwa wa fangasi kutumia dawa mpaka wiki mbili baada ya dalili za maradhi kutoweka.

Pia, ni vizuri dawa zake ukashauriwa na daktari
Kulingana na jinsi ulivyoathirika na Mapunye hayo.

Jinsi ya kujikinga

  • Kuna mbinu mbalimbali za kujilinda usipatwe na fangasi:
  • Hakikisha mwili wako hasa kichwani yanabaki na ukavu muda wote
  • Osha nguo, taulo na mashuka kuhakikisha fangasi wanaondolewa
  • Epuka kushirikiana vifaa vya kunyolea nywele hasa kama hakuna namna ya kuvisafisha na dawa maalum ya kuua vimelea kabla hujatumia
  • Epuka kushirikiana katika utumiaji wa vifaa vya kufanya usafi wa mwili kama mataulo. Kama kazi yako inahusisha ukaaji wa muda mrefu kwenye maji basi hakikisha unakausha mwili hasa sehemu za kichwa au uweke dawa ya kuzuia fangasi kwenye maji hayo.

DAWA YA MAPUNYE KWENYE KICHWA FANYA HIVI:
(1) Ndimu au limau:
Kabla kwenda kukoga jisugue limau ndani ya kichwa na baadae yale maganda ya limau yatie katika maji ya kukoga yaani yawe maji ya Uvuguvugu halafu ukoshe kwa maji yale kwanza na baadae utumie maji yaliyo safi.

(2) (Fenugreek) kwa lugha ya kiswahili inaitwa Uwatu. Uwatu unachukua vijiko 2 vya chai vya Uwatu (fenugreek) unazirowesha katika maji usiku mzima ili zipate kulainika, halafu unazipoda ponda na baadae unapakaa ndani ya kichwa na uwache kwa muda wa saa moja na baadae kuzikosha ikiwa utafanya hivi siku zote mbaa wataondoka Inshallah bila tabu yoyote.

(3) DAWA YA MAPUNYE AU MASHILINGI: Chukua magamba ya parachichi anika juani halafu kisha yatwange ule unga wake changanya na mafuta ya Zaituni,kosha sehemu ile na maji ya uvuguvugu halafu pakaa ule unga mara tatu kwa siku 7,Utapona..
---
Ndimu au limau: Kabla kwenda kukoga jisugue limau ndani ya kichwa na baadae yale maganda ya limau yatie katika maji ya kukoga yaani yawe maji ya Uvuguvugu halafu ukoshe kwa maji yale kwanza na baadae utumie maji yaliyo safi.

(Fenugreek) kwa lugha ya kiswahili inaitwa Uwatu. Uwatu unachukua vijiko 2 vya chai vya Uwatu (fenugreek) unazirowesha katika maji usiku mzima ili zipate kulainika, halafu unazipoda ponda na baadae unapakaa ndani ya kichwa na uwache kwa muda wa saa moja na baadae kuzikosha ikiwa utafanya hivi siku zote mbaa wataondoka Inshallah bila tabu yoyote.

Dawa nzuri ni Grososovin ni vidonge vilitaka kufanana na panadol....nilienda kwa buruda nikandikiwa dawa iyo kwa umri wake walimpa vidonge 15 anameza 1/2 kila siku baada ya kula usiku na akishameza anatakiwa alale vinanguv sana alitumia kwa mwezi amepona.

Dokta aliniambia watoto wanapochez na mashulen halikwepek so apate dawa inayotibu hadi kwenye dam sasaiv yupo vizuri sana
---
Jambo Jema Dawa ambayo hata mimi sikuiamini lakini kwa kweli ilifanya maajabu makubwa na vibarango vikaisha kabisa ni hii hapa. Tafuta majani ya mmea wa pamba msugulie ktk kila kibarango au punye vizuri kabisa hayata chukua muda yatapona kabisa na hayatarudi tena. Mmea wa Pamba inawezekana ikawa ngumu kuupata hivyo unaweza pia kutumia majani ya mmea wa Nyanya (Mnyanya). Naamini atapona maana nilikua na Mdogo wangu alikua hadi anatia huruma lakini alipona na wala hayakurudi tena.
---
Kwa anaesumbuliwa na mapunye/ringworm kichwan dawa hiz.......
-Erythromycine pills 5dayz dosage
-Alatrol 1 tablet 5dayz dosage
-Dermidex 15gm (Tropical Antifungal therapy)
-Na albendazole 3 dayz dosage
source-Mi mwenyewe zimenisaidia within 3dayz nimepona.

Na kula vizuri usisahau
 
Ni ugonjwa wa ngozi na kwa kuanzia anza na usafi wa mwili ikiwa ni pamoja na kuondoa nywele zote; tumia sabuni zakuogea zenye tiba kwa ngozi kama detol ya maji na usipende kufuga nywele ndefu kwa sasa mpaka ukipona wakti huo huo maji yako ya kuoga jaribu kuyachemsha kabla hujayatumia unaweza kuyaacha yapoe ama ukayaoga ya moto!

kwa watoto chunguza pia viyu wanavyotumia kwa usafi kama ni vya kushare na hsa vifaa vinavyotumika kunyolea ikiwa wanyoa nywele.
 
Pole kwa tatizo hilo, jitahid kuwanyoa nywele hao vijana wako halafu kuna dawa ya mba ya kijani ina xstics za spirit inavikausha within 1 week!ol the bect!
 
Pamoja na usafi kama kutumia mafuta yenye sulphur, kunyoa nywele na kutumia sabuni ya dawa , jaribu kuwapa dawa za minyoo; minyoo mara nyingine husabaisha ngozi kuharibika kwa kuota vipele.
 
Wanangu wameugua mapunye (vibarango) na nimetumia dawa nyingi bado naona hawaponi. Nitumie dawa gani ambayo HAISHINDWI?
Wapeleke hospitali maana that is fungal disease na kuna fungus wengine wapo kwenye damu, hivo ukiwanyoa na kupaka dawa wanaisha na kurudi tena haraka wanahitaji kupima damu na kuchomwa sindano ili kuwaua hawa wadudu kwenye damu!!
 
Wakuu kwa wale wataalamu naomba endapo kuna dawa kiboko ya kuponyesha mapunye yanayojitokeza kichwani. Nina watoto mmoja miaka 4 na mwingine miaka 9. Wanasumbuliwa sana; nimejaribu dawa nyingi za kupaka pamoja na sabuni (medicated soaps) lakini kupona hakupo! Msaada tafadhali.
 
Ndimu au limau: Kabla kwenda kukoga jisugue limau ndani ya kichwa na baadae yale maganda ya limau yatie katika maji ya kukoga yaani yawe maji ya Uvuguvugu halafu ukoshe kwa maji yale kwanza na baadae utumie maji yaliyo safi.

(Fenugreek) kwa lugha ya kiswahili inaitwa Uwatu. Uwatu unachukua vijiko 2 vya chai vya Uwatu (fenugreek) unazirowesha katika maji usiku mzima ili zipate kulainika, halafu unazipoda ponda na baadae unapakaa ndani ya kichwa na uwache kwa muda wa saa moja na baadae kuzikosha ikiwa utafanya hivi siku zote mbaa wataondoka Inshallah bila tabu yoyote.
 
Nadhani pia huwa inakuwa kwenye umri, maana nikiwa mtoto nakumbuka nilipataga nikawa sipendi kabisa na nilijaribu dawa nyingi ikiwepo moja inayoitwa B-Tex ambayo ilinisaidia sijui kama bado ipo.

Nakushauri wapeleke watoto kwa daktari wa ngozi coz inamuumiza sana mtoto kisaikolojia anapoteza hata uwezo wa kujiamini mbele ya wenzako, at that age mtoto ameshaanza kujitambua.

Pole
 
Mshubiri Mwitu au Aloe Vera kwa jina lingine. Ponda paka kichwani kila siku mara mbili asubuhi na usiku.
 
Ahsante FaizaFoxy. Dozi hii ni ya siku ngapi au hadi nione dalili za kupona? Nifahamishe tafadhali.

Hiyo ni mpaka upone na kupona huanza immediately na huchukuwa siku tatu mpaka kumi inategemea na uwingi wa hayo mapunye, utashangaa.
 
Pia, uwe unawanyoa nywele hao watoto angalau kila baada ya wiki mbili. itasaidia kuona kama kuna sehemu sehemu zingine zimepata upele na kama ni dawa inapakika vema kabisa (evenly).
 
Mpwa wapeleke wakachek damu zao pima full b pictur usiogope hii ni mwanzo nakama unaogopa nenda hata na housgirl akupe company

Fuata ushauri wa hapo juu na ikiwezekana chukua na wangu chukua maji weka kwenye sufuria kadogo kichwa chao kinaenea weka nusu ya vinegar kama maji then wainamishe vichwa kwa dk 15
mara tatu kwa siku njoo rudi usafiri na didy bure sichaji mtu
 
Habari wadau?
Mimi nina mtoto wa mwaka mmoja ambaye amepata punye eneo la kisogoni,punye hilo kalipata tangu akiwa na miezi 9,nimempeleka hospitali tukaandikiwa dawa atumie lakini bado halijapona,pia nimempa syrup ya minyoo last week lakini tatizo liko palepale,naomba msaada tafadhali.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu Pole sana Jaribu hizi dawa moja kati ya hizo Dawa tatu hapo chini:

(1) Ndimu au limau: Kabla kwenda kukoga Msuguwe limau ndani ya kichwa na baadae yale maganda ya limau yatie katika maji ya kukoga yaani yawe maji ya Uvuguvugu halafu ukoshe kwa maji yale kwanza na baadae utumie maji yaliyo safi.

(2) (Fenugreek) kwa lugha ya kiswahili inaitwa Uwatu. Uwatu unachukua vijiko 2 vya chai vya Uwatu (fenugreek) unazirowesha katika maji usiku mzima ili zipate kulainika, halafu unazipoda ponda na baadae unapakaa ndani ya kichwa na uwache kwa muda wa saa moja na baadae kuzikosha ikiwa utafanya hivi siku zote mbaa wataondoka Inshallah bila tabu yoyote.

(3) Mshubiri Mwitu au Aloe Vera kwa jina lingine. Ponda paka kichwani kila siku mara mbili asubuhi na usiku. Tumia Dawa mojawapo sio zote tafadhali kisha utpe feedback.
 
Kunadawa in aitwa "Dawa ya Mba", niya maji inarangi ya kijani, unampaka kwakutumia pamba sehemu iliyoathiriwa.
NOTE
Siyo ya kunywa.
Kidogo inaleta maumivu.
 
Nina dawa nlipewaga hospital ni ya unga wa njano, ina tibu kila kitu cha ngozi, vipele, chunusi, mkanda wa jeshi,f angasi, mapunye, makovu etc siijui inaitwaje kitaalamu,ila unaichanganya na mafuta ya mgando kisha unapka sehemu hucka haipt wiki pamepona..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom