Jinsi ya kuondoa madoa na mabaka mwilini

feis buku

JF-Expert Member
Aug 29, 2011
2,342
676
1595929296777.png


BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA KUHUSU TATIZO HILI
Wandugu habari zenu!

wapendwa niliugua tetekuwangu mwezi mmoja umepita, nimepona sasa naendelea na masomo/ kazi yangu kama kawaida. Nimebalkiwa na madoa mwilini especialy sehemu za mgongo na usoni (reception) kiasi. Haya madoa yananikera wandugu natamani kuyaondoa zitoke! Naomba ushauri wa kupata dawa itakayonisaidia kuondoa haya madoa usoni.

Ahsanteni wapenzi FB!
---
Wapendwa wana Jf,

Habari zenu ndugu zangu, na marafiki zangu wote humu ndani!

Wapendwa ma-dokta na wataalamu, na hata wazoefu......Naomba mnisaidie katika hili, Hivi kuna dawa ya kuondoa kovu mwilini?

Mfano labda ulifanyiwa upasuaji katika mguu au mkono au ulipata ajali na ikalazimika kushonwa nyuzi kadhaa ; LAKINI lile kovu bado lipo japokuwa kidonda kimepona. Je kuna dawa yeyote unayoifahamu ambayo inaweza kusaidia kufuta hilo kovu mwilini au hata kulififishaa kabisa lisionekane?

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu ndugu zangu wote humu JF!

ASANTE.
---
Naomba nisaidiwe jinsi ya kuondoa dark spots katika ngozi. Makovu hayo yamekuja baada ya kupona tetekuwanga. Nitumie dawa au njia gani ili makovu hayo yaishe.?
---
Habari ndugu zangu

Mke wangu anasumbuliwa sana na tatzo la kutokwa na vipele wakati wa period toka alipo vunja unga na vimenwachia makovu mwili mzima

Tumezunguka hosptal zote bila mafanikio kama kuna mtu anajua dawa au daktari anipe contact

UFAFANUZI WA KINA WA TATIZO HILI
Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujit-okeza kama viuvimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani Bacteria.

Kwa lugha ya kidaktari chunusi huitwa Acne Vulgaris.Chunusi ndio ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano nchini Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni kumi na sa-ba..Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wa-kati wa balehe (adolescents) .

Karibu asilimia 85 ya vijana kati ya umri wa miaka 12 hadi 25 hupata chunusi na zaidi ya asilimia 20 ya wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka ishirini hupata chunusi wakati mwingine hata watoto wadogo pia huweza kupata chunusi hii ni tofauti na watu wengi wanavyofikiria kuwa chunusi ni dalili ya balehe.

Chunusi ni ugonjwa unaoathiri vifuko au glandi za ngozi.Katika ngozi ya binadamu kuna glandi ziitwazo Sebaceous ambazo zipo chini ya ngozi na kazi yake kubwa ni kutoa mafutamafuta yaitwayo Sebum ambayo hu-saidia kuiweka ngozi kuwa nyevu na yenye mvuto.

Wakati wa balehe mwili wa binadamu hutoa Sebum kwa wingi na kwa sababu wakati huu vikemikali vya mwili yaani sex hormones hutolewa kwa wingi hasa hormone ya kiume iitwayo androgen husababisha utoaji wa sebum kuwa mwingi zaidi kuliko kawaida. Sebum inapotolewa kwa wingi huungana na seli za ngozi zilizo-kufa na kutengeneza mchanganyiko mzito kama nta uitwao comedo ambao huziba vishimo vya kutolea joto.

Maambukizi zaidi hutokea pale ambapo vijidudu yaani baktaria vinaposhambulia vishimo vilivyoziba hapo kivimbe ambacho watu wengine huita Pimple hujitokeza pale ambapo Sebum, bacteria, seli za ngozi na seli nyeupe za damu zinapo-changanyika na kujikusanya katika vishimo vya jasho vilivyoziba na eneo husika hupata vivimbe au vipele ambavyo tunaviita chunusi.

Ukubwa wa kipele hutegemea ngozi ya mtu au kiasi cha mchanganyiko nilioeleza hapo juu katika eneo husika.Vipele vinaweza kuwa vidogo au vikubwa. Chunusi wakati mwingine husababisha mabaka katika ngozi hali hii hutokea pale ambapo seli za ngozi zilizoharibika huondolewa na seli mpya kutengenezwa.

Ngozi mpya hutengenezwa kirahisi tu mahali palipokuwa na chunusi hali hii husababisha mlingano usiosahihi wa ngozi na hutoa kidonda ambacho baadaye hubaki kama baka. Chunusi hutokea zaidi katika uso,kifua ,mabega na mgongoni kwa sababu maeneo hayo yana vifuko au glandi za Sebaceous nyingi.

CHANZO CHA CHUNUSI
Chanzo halisi cha chunusi hakijulikani.hata hivyo baadhi ya vitu vinavyoongeza uwezekanifu wa kupata chunusi ni;
  1. UMRI – Kama nilivyosema hor-mone/vikemikali hutolewa kwa wingi sana mtu anapofikia umri wa kubale-he.Kemikali hizi huongeza utengenezaji wa nta (sebum) katika ngozi ambayo huchochea kutokea kwa chunusi
  2. VIPODOZI –Baadhi ya vipodozi kama Make-up za kina dada na Sprays za ny-wele zina mafuta ambayo yanaweza kusababisha chunusi kuwa nyingi zaidi.
  3. CHAKULA- Chunusi hazisababishwi na chakula bali baadhi ya vyakula hufan-ya chunusi kuwa nyingi zaidi.
  4. DAWA-Chunusi zinaweza kujitokeza kutokana na kutumia dawa kadhaa kama vile antibiotics,Vidonge vya uzazi wa mpango,steroids na tranquilizers.Steroid ni dawa zenye homoni zilizotengenezwa kitaalamu ambazo wakati mwingine wanariadha huzitumia tofauti na ma-kusudio ili kuongeza unene wa misuli yao.
  5. MAGONJWA- Magonjwa yatokanayo na matatizo katika vikemikali (hormonal disorders) huongeza matatizo ya chunusi hasa kwa wasichana.
  6. MAZINGIRA- Chunusi huweza kuwa nyingi zaidi hasa unapoishi mazingira yenye mafuta,grisi au hewa chafu .Kutoa jasho sana hasa katika mazingira ya joto huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi.
  7. JINSIA-Wavulana hupata sana chunusi kuliko wasichana.
  8. FAMILIA- Wakati mwingine chunusi hujitokeza sana kwa wanafamilia wa familia kadhaa kuliko nyingine.
  9. HOMONI- Mabadiliko ya homoni za mwili hasa wakati mwanamke akiwa katika siku zake,ujauzito au mwanamke anapokuwa na umri mkuwa hupelekea kupata chunusi.
  10. USAFI WA MWILI- Kutumia sabuni zenye kemikali,kujisugua sana na kuzitoboatoboa chunusi au vipele hu-sababisha chunusi kuongezeka zaidi.Kukaa muda mrefu na jasho mwi-lini au kutooga huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi
  11. MAWAZO AU STRESS-Mtu anapokuwa na mawazo mengi vimkemikali kadha hutolewa mwilini ambavyo huwe-za kuchangia au kusababisha chunusi

DALILI ZA CHUNUSI
Vipele au vivimbe vidogo vidogo ambavyo pengine husababisha mwasho au vinavyouma ni dalili ya chunusi.Wakati mwingine huweza kujitokeza kama baka dogo na wakati mwingine mtu anaweza utambuzi wa chunusi unaweza kuwa mgumu kutokana na watu walivyomakini au wanavyojenga wasiwasi kubwa katika mwonekano wao hasa usoni.Ikumbukwe kuwa kutokana mwonekano wa chunusi ni rahisi sana.

Daktari kuzigundua, japokuwa katika familia zetu ni mara chache sana mtu akaenda kumwona daktari au mtaalamu wa magonjwa ya ngozi kwa sababu ya chunusi.Pale inavyotokea hivyo basi hali inakuwa ni mbaya zaidi.Hata hivyo si vibaya kumwona daktari ambaye atakuuliza kuhusu chakula, ngozi, dawa unazotumia na vitu vingine vinavyowe-za.kuchangia mtu kupata chunusi

MATIBABU
Matibabu ya chunusi yanajumuisha kupunguza utoaji wa anta (sebamu ), kuondoa seli za ngozi zilizokufa na kuua wadudu yaani bacteria.

Matibabu huweza kutofautiana kutokana na wingia au ukubwa wa tatizo. Suala la kuzingatia ni kuepuka mambo yanayoweza kusababisha chunusi kama nilivyoeleza hapo juu.

DAWA ZA KUPAKA
Kuna dawa za kupaka ambazo hupaka katika eneo la ngozi lililoathirika kwa chunusi. Dawa hizi hupatikana kama cream,lotion,gel au pad.

Dawa hizi hutumika kutibu chunusi ambazo haziko katika hali mbaya hasa kama kuna vijipele vidogo vidogo tu. Mojawapo ya dawa hizi ni antibi-otic kama zenye mchanganyiko wa gentamyicin na betamethasone au dexame-thasone kama vile Gentrisone au Gentriderm cream, Erythromycin,B-Tex na kadhalika.Pia Persol forte Gel husaidia hasa ukianza na asilimia ndogo (2.5%) na kuen-delea kadri ngozi yako inavyohimili dawa. Gentamycin huua wadudu wanaosababisha chunusi wakati dawa nyingine huondoa mwasho.

Dawa nyingine ni zile zinzolainisha nta au Comedolytics na kufanya vishimo vya jasho kufunguka na dawa nyingine huongeza kasi ya utengenezwaji wa seli mpya za ngozi.

Dawa hizi za kupaka hushauriwa kupakwa angalau mara mbili au tatu kila siku hasa baada ya kusafisha kwa maji safi na sabuni ya kawaida na kukausha kwa taulo eneo lenye chunusi na matibabu yanaweza kuchukua wiki kadhaa.

DAWAZA KUMEZA
Wakati mwingine daktari anaweza kumshauri mgonjwa kutumia dawa za kumeza kulingana na wingi au ukubwa wa tatizo.

Dawa kama antibiotics huua wadudu na huzuia chunusi ,dawa hizo ni kama vile Erythromycin topical, Accutane (isotret-inoin), Benzamycin Cleocin T (clindamycin phosphate), Desquam-E (benzoyl peroxide) Minocin (minocycline hydrochloride) na ”Si vema kujinunulia mwenyewe tu na kuanza kutumia bila ushauri wa daktari au mtaal-amu wa magonjwa ya ngozi.”

Wanawake wenye chunusi zisizotibika wanaweza kupewa Anti-androgens kama vile baadhi ya vidonge wa uzazi wa mpango.Chunusi sugu hutibiwa kwa ciorticosteroids na anti-iflammatory drugs ambazo hutibu chunusi sugu ambazo huitwa Acne fulminans na hupatikana zaidi kwa vijana.

MATIBABU MENGINE
Kwa nchi zilizoendelea matibabu yanaweza kuwa hata upasuaji mdogo (skin grafting) au plastic surgery kama chunusi imesaba-bisha baka kubwa na kuna njia kama vile Chemical peel ambapo kemikali hupakwa kwenye ngozi na inapokauka kipande au gamba la juu la ngozi huondolewa na kuondoa baka.

MATIBABU MBADALA
Haya hujumuisha lishe bora na usafi wa mwili.Ni vema kuoga mara kwa mara na kujifuta maji kwa taulo safi na kuiweka ngozi katika hali ya ukavu nakuepuka upakaji wa mafuta mengi ya mgando hasa wakati wa joto.

Watu wenye chunusi wanashauriwa kulAa mlo kamili wenye vyakula vyenye madini ya zinki,nyuzinyuzi, matunda, mboga za ma-jani,vitamin B complex na Chromium. Ni vema kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe,vyakula vya maziwa, tumbaku, sukari, vyakula vilivyoandaliwa viwandani na vyakula vyenye Iodine nyingi kama vile chumvi

MUHIMU

Chunusi haziwezi kutibika kabisa japokuwa iwapo matibabu Yatakuwa sahihi watu 60 kati ya 100 hupona na unapokuwa unatumia dawa usitarajie kupona haraka kwani inaweza kuchukua hata miezi miwili kupata nafuu na zinaweza kujitokeza unapoacha kutumia dawa.Chunusi pia huweza kupona kwa kuacha mabaka ambayo kwa hapa nchini hakuna utaalamu sahihi wa kuyaondoa bali huweza kuondoka kadri muda unavyoenda au kwa kemikali kali ambazo zinaweza kuwa na madhara katika ngozi.

MAMBO YA KUFANYA ILI USIPATE CHUNUSI

Hakuna njia sahihi ya kujizuia ila unaweza kufanya yafuatayo;
  1. Osha taratibu sehemu unayodhani ina chunusi kwa maji safi na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa kucha au kitu choichote kigumu.
  2. Tumia make-up au vilainisha ngozi visivyo na mafuta mgando
  3. Osha nywele zako kila mara na epuka nywele kuziba uso (kwa wenye nywele ndefu)
  4. Kula mlo kamili na epuka vyakula vyenye mafuta mengi.
  5. Usibinye au kutoboa vipele kwa pini au kitu chenye ncha kali.
  6. Epuka kukaa sana juani,mwanga wa asubuhi ni mzuri ili kupata vitamin D
  7. Punguza mawazo


MICHANGO NA USHAURI ULIOTOLEWA NA WADAU WA JF:
KAUMZA,

kutoa Madoadoa yaliyosababaishwa na Chunusi

Mahitaji
Unga wa Riwa
Maji ya Rose (Rose water)
Maji safi ya kawaida
Limao
Mafuta ya Zaituni (Olive oil)

Hatua ya Kwanza
Chukua unga wa Riwa na Maji Rose uyachanganye pamoja na ukoroge hadi mchanganyiko wako uwe mzito.

Hatua ya Pili
Upake mchanganyiko wako katika sehemu yenye makovu na uache hadi ukauke. Unaweza kukaa na huu mchanganyiko huu kwa muda mrefu ila inategemea na nafasi yako pia, mchanganyiko huu unasaidia kunyonya mafuta na kuacha ngozi kavu.

Hatua ya Tatu
Nawa vizuri na maji ya uvuguvugu.

Hatua ya Nne
Paka Juice ya Limao kwenye sehemu yenye makovu. Juisi ya limao inatumika kama brichi ya asili ambayo husaidia kufifisha madoadoa na kuondoa makovu kwenye ngozi .

Hatua ya Tano
Paka mafuta ya Olive kwenye makovu, hii husaidia kulainisha ngozi na kufanya makovu yasionekane kirahisi.

Mambo ya kuzingatia
Wakati unaanza kufanya tiba hii jaribu kuacha kutumia aina ya vipodozi vya kemikali ulivyokuwa unatumia na utumiea hii tiba ya asili isiyo na madhara. Jaribu kufanya zoezi hili walau mara mbili kwa wiki ndani ya mwezi mmoja utaona matunda yake.
---
tumia sabuni za kawaida zisizo na marashii zile ya kuwaogeshea watoto wachanga mfano mbuni..kanga,.. jamaa nk...
tumia maji ya uvuguvugu wakati wa kuosha uso tumia cloves maalum siyo chupi kuepuka bacteria
usije vyakula vya mafuta yaan kuanzia blue band..peanut butter..chips nk
kula matunda na maji kwa wingi
epuka kushika shika uso..yaan kubinya machunusi..pole saaana
---
Tumia sabuni ya carambola na mafuta ya ingrams comphor cream(the skin doctor) ya south africa yanapatikana kwenye maduka makubwa ya vipodozi hata kwenye pharmacy kubwa pia utayapata yapo kwenye kopo la kijani..unapaka makavu hivohvo kama yalivo bila kuchanganya na kitu chochote pia kwa sasa usitumie poda wala make up aina yoyote mpaka uso wako utapokua vizuri..tumia carambola herbal soap na ingrams comphor cream morning and evening daily kwa muda wa mwez mmoja then ulete mrejesho.
---
pole sana mkuu.
tatzo ninaloona nahisi ulihitaji matokeo ya haraka unaweza ulichanganya hizo cream(tube)nyingi kati hazishauriwi kutumiwa zaidi ya wiki mbili,fanya yafuatayo:-

binafsi natumia Grace products,na zinanipa matokeo,umesema umeshazitimua zijaribu tena kwa mwezi mmoja ile sabuni na losheni

kunywa maji mengi
kula vyakula na mbogamboga na matunda (fibre yake itakufaa) tumia aina moja ya tiba acha ku"confuse" ngozi
kama uko ndoani ,make a great deal of sex (sex with purpuse) sex ni tiba kwa magonjwa mengi,leta mrejesho baada ya wiki,utakua different.(nina waswas na "life sex yako"
NB:Usisahau. hill "stress" anaharibu nguzi,epukana nae!
 
Wala usihofu...kuna tofauti kubwa kati ya makovu ya tetekuwanga na mkanda wa jeshi (wote ni virus). Wakati kovu la mkanda wa jeshi halifutiki kamwe...kovu za tetekuwanga huwa zinafutika bila ya kuweka kitu chochote. Na hufutika kabisa kiasi hutanotice kwamba kulikuwa na tetekuwanga.

Kwa hiyo subiri tu kovu zote zitafutika zenyewe taratibu na kupotea kabisa. Ukienda kutafuta product za kufuta utaibiwa tu pesa yako...
 
Dr Riwa ubarikiwe sana ni miongoni mwa watu ntakaowapigia goti leo jion kumuomba mungu awapatie maisha marefu duniani na kuwajaalia afya njema!ahsante sana kwa ushauri wako!!
 
feis buku, polwe sana fb kula na matunda kwa wingi kwa ajili ya vitamin c ili kurutubisha ngozi dear
 
Pole FB nakumbuka nikiwa mtoto nilishawahi kuugua ugonjwa huo, lakini mpaka leo hii ngozi yangu ipo ng'ada kabisa. Usihofu kuhusu hayo makovu kama Dr. Riwa alivyokushauri lakini usiwe na haraka ya kutaka yaondoke ghafla maana nimeona dalili ya kujichukia kutokana na makovu hayo. Hayachukua muda mrefu kutoweka.
 
Naomba nisaidiwe jinsi ya kuondoa dark spots katika ngozi. Makovu hayo yamekuja baada ya kupona tetekuwanga. Nitumie dawa au njia gani ili makovu hayo yaishe.?
 
Kuna sabuni inaitwa 'Black spot soap' ni nzuri sana. Inauzwa shilingi 2000 au zaidi kidogo. Ni nzuri kwa kuondoa alama usoni. Unakuwa unaitumia kuosha uso. Baada ya muda vinafutika vyote.
 
Kuna sabuni inaitwa 'Black spot soap' ni nzuri sana. Inauzwa shilingi 2000 au zaidi kidogo. Ni nzuri kwa kuondoa alama usoni. Unakuwa unaitumia kuosha uso. Baada ya muda vinafutika vyote.

Kaka hiyo sabuni haichubui ngozi na kukufanya uwe kama Tanzania yenye mgao wa umeme? Na hilo jina ndio jina lake ambalo naweza tumia kuuliza madukani ili niweze ipata?
 
Kuna sabuni inaitwa 'Black spot soap' ni nzuri sana. Inauzwa shilingi 2000 au zaidi kidogo. Ni nzuri kwa kuondoa alama usoni. Unakuwa unaitumia kuosha uso. Baada ya muda vinafutika vyote.

Hizo sabuni si nzuri kabisa huwa zinachubua ngozi baada ya muda unaonekana kama mtu anayetumia krimu. Hata usijaribu kamwe!
 
Kuna wataalamu wengi tu wa ngozi, jaribu kwenda huko. Ngozi ni kitu sensitive, na sometimes dawa inayoukusaidia wewe inaweza kutomsaidia au pengine kuidhuru ngozi ya mtu mwingine. Nenda kwa wataalam usije tulaumu baadaye
 
Nenda kwa Kairuki kuna daktari mzuri wa ngozi, yuko siku za jumatatu kama sikosei.
 
Black spot soap ndio jina lake na si kweli kuwa inachubuaa ngozi,hii sabuni ni kwa ajili ya kuondoa madoa kwenye ngozi.

Ila kama vp,basi ni bora ukaenda kwa wataalam wa ngozi au hata kwa Pharmacist yeyote akakuelekeza dawa ambayo ni bora.
 
Hello wandugu. jamani naomba msaada, nimetokewa na chunusi kama wk 3 sasa zimekauka na kuacha nadoa meusi, usoni nitumie nn yatoke. Msaada tafadhali
 
Pole sana dada angu, Jaribu kutumia Retin A cream itakusaidia kwa tatizo lako.Nadhani inapatikana pharmacy au kwenye maduka ya vipodozi
 
Wanasema chunusi nyingi ni kutokana na kuwa na hamu ya sex na kutofanya sex...
sijui labda hilo nikusaidie lol

Kuhusu dawa nenda pharmacy zipo tele
 
Pole sana dada. Mi nlipatwa na hayo madoa nkaenda pharmacy lakin muuzaji alinambia niende hosptl kwanza kwa 7bu kuna dawa zingine zinasabisha madoa zaidi. Hivyo basi ni bora upate ushauri kwa daktari kutokana na ngozi yko ndipo uende hko pharmacy.
 
Mmmh The Boss. Haya bwana.

Asanteni kwa ushauri. Nimeenda phamacy nimepewa BETADERM OINTMENT..Ngoja nijaribu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom