Dawa ya kusafisha Tumbo (Msaada)

Larusai Mux

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
979
275
Salam wakuu,

Ni siku ya tano sasa nasumbuliwa na Kiungulia (Bile......), haijalishi nimekula aina gani ya chakula basi ni shida tu. Nimejaribu kuomba ushauri kwa watu nao wakasema ni tumbo chafu hivyo inabidi nitapike au niharishe ili uchafu uishe, naombeni ushauri zaidi na tiba husika.

Shukrani..
 
Kama unataka kuharisha kunywa mafuta ya Mzaituni [Olive] saa 10 alfajiri hakikisha choo ni cha peke yako na ukitaka kuhara kukate kula kitu chochote.
Nb: utachamba hadi kijambio kiume.
 
Kama unataka kuharisha kunywa mafuta ya Mzaituni [Olive] saa 10 alfajiri hakikisha choo ni cha peke yako na ukitaka kuhara kukate kula kitu chochote.
Nb: utachamba hadi kijambio kiume.
mbona ni balaa na nna miaka mingi sijaarisha wala kutapika mkuu,nashkuru kwa ushauri
 
Salam wakuu,
ni siku ya tano sasa nasumbuliwa na kiungulia(bile......),haijalishi nimekula aina gani ya chakula basi ni shida tu.
Nimejaribu kuomba ushauri kwa watu nao wakasema ni tumbo chafu hivyo inabidi nitapike au niharishe ili uchafu uishe,
naombeni ushauri zaidi na tiba husika.
Shukrani

Tumia Alovera juice nakuhakikishia itakusaidia Sana. Ni PM ukihitaji nikuletee popote ulipo
 
Habari ndugu pole na tumbo. Nakushauri kama bado wasumbiliwa tumia Antidiarr, itakusaidia sana na hata kwa wale wenye matatizo ya muda mrefu, wakitumia dawa hii nawahahikishia hakuna taabu tena. Nimewapa wengi na wamerudisha majibu ya ufumbuzi wa matatizo yao. Unaweza ni PM.
 
kunywa maji glass mbili alfajiri km saa 11 utapata choo fasta then utakuwa fresh
 
Kama unataka kuharisha kunywa mafuta ya Mzaituni [Olive] saa 10 alfajiri hakikisha choo ni cha peke yako na ukitaka kuhara kukate kula kitu chochote.
Nb: utachamba hadi kijambio kiume.

aisee hawezi kupoteza "locki" kweli
 
Salam wakuu,
ni siku ya tano sasa nasumbuliwa na kiungulia(bile......),haijalishi nimekula aina gani ya chakula basi ni shida tu.
Nimejaribu kuomba ushauri kwa watu nao wakasema ni tumbo chafu hivyo inabidi nitapike au niharishe ili uchafu uishe,
naombeni ushauri zaidi na tiba husika.
Shukrani

USICHOKIJUWA KUHUSU MARADHI YA KIUNGULIA

Kiingulia ni acidity iliyozidi kufuatia kula kitu chenye acidity. Maharage yakilala yana ferment hivyo kutengeneza more acidity state hivyo ukiyala vimengenyo vya pelipeptaid, peptaid na pepton vyenye kazi ya kuyeyusha wanga vinatoa acid nyingi ukichanganya na ile ya maharage matokeo yake ni kiungulia.

Dawa ya kiungulia ni kunywa alcalinine yoyote au base ili kuineutralize ile acid na kutengeneza chumvi na maji hivyo kutokuwa na madhara tena.

Dawa ya kawaida sana ni vidonge vya magnesium tricilicate au actal. Majivu yakichanganyika na maji yanatengeneza alcaline solution ambayo pia inaneutralize ile acid. Tatizo la majivu hakuna kipimo sahihi ukizidisha, hata ile acid ya kawaida ya kusaga chakula inakuwa neutralized hivyo chakula kinashuka kilivyo.

Usipotafuta suluhisho la kudumu kuicontrol hiyo acid tumboni kwako, inaweza kumungunya mpaka ngozi laini ta tumboni hivyo kusababisha vidonda vya tumbo vinaitwa ulcers.

DAWA YA KUTIBU KIUNGULIA KWA TIBA MBADALA:

KIUNGULIA::
TIBA;:
Changanya glasi moja (250ml) ya maziwa na kijiko kikubwa 10ml) cha mafuta ya habat soda.
Kunywa mchanganyiko huu na urudie kutwa mara tatu (1×3) kwa muda wa siku 5. tumia kisha uje unipe feedback

Chanzo.
USICHOKIJUWA KUHUSU MARADHI YA KIUNGULIA
 
Salam wakuu,
ni siku ya tano sasa nasumbuliwa na kiungulia(bile......),haijalishi nimekula aina gani ya chakula basi ni shida tu.
Nimejaribu kuomba ushauri kwa watu nao wakasema ni tumbo chafu hivyo inabidi nitapike au niharishe ili uchafu uishe,
naombeni ushauri zaidi na tiba husika.
Shukrani

Nishatumiaga Castor Oil....kule kulikonikuta ni zaidi ya kuharisha...I would advise uitumie pia.
 
Nashkuru kwa ushauri wakuu,japo naona ile hali imeisha.
Sijatumia chochote ila ni baada ya kusitisha unywaji wa uji wa ulezi saa nne asubuhi kwa siku tano hivi,huenda kilikua chanzo?!..
 
Nishatumiaga Castor Oil....kule kulikonikuta ni zaidi ya kuharisha...I would advise uitumie pia.

Ulienda kununua wapi haya mafuta? Kwenye pharmacy hizi za kawaida ama tuba asili ama mpaka kariakoo.

Na pia, ulitumia kipimo gani, ulikunywaje yani.

Mwisbo, nimeona kuna ya kijani na mengije meusi.. Yapi ndio yanafaa kunywa kutibu choo.
 
Kuna mtu alikuja nayo nyumbani. Sikuuliza alipoyatoa.

Nilikunywa kijiko kimoja tu cha chakula.

Sikumbuki rangi ya chupa ila nakumbuka yenyewe hayakuwa na rangi, kama maji
 
Kuna mtu alikuja nayo nyumbani. Sikuuliza alipoyatoa.

Nilikunywa kijiko kimoja tu cha chakula.

Sikumbuki rangi ya chupa ila nakumbuka yenyewe hayakuwa na rangi, kama maji

Kaka nashukuru, juzi nilinunua kichupa cha Castor Oil pharmacy. Jana jioni nikameza vijiko vinne.
Usiku mzima nimeharisha tu, huku nakunywa maji. Sasa hivi niko mwepesiiiiii
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom