Dawa ya kupinga ufisadi: Ni maandamano au Migomo?

RMA

JF-Expert Member
Oct 10, 2010
409
87
CUF na TUCTA wanapanga kuandamana. Ni sawa! Lakini jamani tungepiga kura kwa uangalifu, tungekuwa na sababu ya kuandamana? Si tuliyataka wenyewe? Tulipiga kura kama vipofu, sasa tunalalama kama vichaa! Na bado tutaandamana kama vipofu na kujikuta tunajikuna maji ya kuwasha kama vichaa!

Watanzania kilio cha nini? Maaandamano ni suluhisho? Kama kweli ipo nia thabiti ya kupinga utawala mbovu, dawa madhubuti kwa sasa ni migomo ya nchi nzima kila kona ya nchi. Maandamano hayana tija. Si mtaambulia maji ya kuwasha tu? Iwapo migomo haiwezekani, basi kaeni kimya mnyolewe vizuri!

Ni nafuu umeme ungepanda kwa asilimia mia na saba ili tupate akili, kwa kuwa siasa za Tanzania zimekuwa mithili ya ushabiki wa Yanga na Simba bila kuangalia uhalisia wa maisha. mak.ralph@yahoo.com
 
RMA nakuunga mkono,kufanya maandamano ni kujidanganya coz haitaleta effect yoyote,la msingi ni kufanya mgomo nchi nzima!
 
Back
Top Bottom