Tatizo la upele Kidevuni: Chanzo na matibabu yake

kwanza nikupe pole...nunua machine za kukatia nywele original siyo feki,sababu haziwi za moto kwa mda mrefu..hiyoi inatakufanya ngozi yako kutoungua.nyoa na machine yako taratibu..bila kukwangua hadi ngozi then baada ya hapo chukua taulo lenye majimaji ya uvuguvugu sijafishe kwenye kidevu chako..mapele yatakwenda yanapungua taratibu mpaka kwisha,then unaweza kuendelea kunyoa kwa kusugua kidevu mpaka ndevu zote zinakwisha hapo mapele yatakuwa yalikwisha kauka mda mrefu..

Tafadhali;usipakae powder walaspirit au mafuta yoyote yale kabla kunyoa au baada ya kunyoa.
hii njia ni bomba zidi kuliko nyingine yeyote ile hata mie nlipata shida sana nkashauriwa hivihivi saizi nakula bata tu kidevu soft hakuna vipele wala nini well done mkuu
 
Kwa muda mrefu now ninasumbiliwa na tatizo la kutoka vipele baada ya kunyoa ndevu,nimetafuta tiba sana lakini hakuna nafuu yani mpaka now sijui tiba nitaipata lini,mara ya mwisho dactari aliniambia vipele vinatokea bse ndevu zinapoota zinashindwa kupenyeza kwenye ngozi hivyo kujisokota kwa ndani na kusababisha vipele,please anayefahamu tiba yake anipe taarifa.PLEASE TUKAWA SERIOUS MTU ANAPOOMBA USHAURI AU MSAADA KWA MAMBO YANAYOGUSA AFYA NA SI KUANZA KUKEJELI.
 
vipele vya ndevu ni tatizo linalowasumbua watu wengi. Kama upo Dar es Salaam nakushauri uende duka la S.h amon lipo posta ununue after shave ambayo inaweza ikakusaidia au uwaelezee tatizo lako wanaweza kukusaidia. Naweza kukushauri pia unaponyoa ndevu usikwangue ndevu zote mpaka zikaisha,unaponyoa unaweza ukabakisha ndevu kidogo,kufanya hivi ni kwa lengo la kuepuka machine ya kunyolea isikwaruzane na ngozi. Njia hii itakusaidia sana ndugu.
 
Hili ni tatizo ambalo hata nami nimekutana nayo sana miaka kadha iliyopita

Elimu aliyotoa mhalisi ni nzuri lakini Mi naona bado haimalizi tatizo tajwa.

Fanya hivi,Acha ndevu ziote usiogope kabisa, hata unaweza acha kama mwezi moja hivi. Maana ukiacha ndevu hivyo yale maupele yanapungua ama kwisha kabisa.

Sasa siku ya kwenda kunyoa hakikisha kabisa una kangua yote na ikiwezekana tumia wembe na hakikisha kbs una LIMAO moja hata mbili mkononi.

Ukimaliza tu kunyoa kata limao ktkt na pakaa kote kwenye usawa wa ndevu! Hata kesho yake pakaa tena!
Halafu kama unatumia wembe sasa hakikisha baada ya siku tatu tena pitisha wembe tena na pakaa limao na hapo mwenyewe utaleta majibu hapa kwamba Jamiiforums kuna kila aina ya mtu.

Pole sana Kamanda!
 
Ok.usiuumize kichwa ipo gentlemanpride.isipokusaidia utarudishiwa pesa yako. I'm sure 200%. Mm nimesaau kbsa.
 
Ndugu wanajamvi, naomba mnisaidie hili la vipele vya ndevu. Kama mjuavyo sio waafrika nywele na vinyweleo vyetu huota kwa kujikunja ikiwa ndani ya ngozi(spiral growth) tofauti na wazungu au wahindi ambao zao huota zimesimama.

Vilevile miongoni mwetu waafrika kuna ngozi ambazo haziathiriwa na outaji huo kwani nywele inatoka hadi nje ya ngozi kwa style hiyo hiyo.

Tatizo linalonikabili mie ni kwamba ndevu nyingi hazioti na kutoka nje ya ngozi, zinazuliwa ndani bila shaka ukuaji wa spiral/coil hivyo kusababisha ngozi kutengeneza kipele kwa juu. Pindi inapofanikiwa kuchomoza juu ya ngozi kipele hukauka na kupona. Ila isipoweza kuchomoza huwa inatengeneza kipele kwa muda mrefu hadi ntakapoivutwa nje ya ngozi.

Nimeshafanya jitihada za kutumia mashine tofauti tofauti za kunyolea na pia shaving cream za magic zenye strengths tofautitofauti bila mafanikio. Mwenye ufahamu, uelewa na experience yoyote ambayo inaweza nisaidia animwagie hapa jamvini tafadhali. Urembo wa ndevu siufurahii mwenzenu.
 
Pole sana mkuu, tatizo ulilonalo ni sawa na langu! Hata mimi nimehangaika bila mafanikio, kidevu kimekomaa balaa! By the way, kuna after shave inaitwa BUMP PATROL(sory kwa kuitangaza, ni ktk kusaidiana!) hiyo inasaidia kuondoa mapele na kufanya ndevu ziote vizuri! Lakini, INATEGEMEA NGOZI IMEHARIBIKA KIASI GANI!! Kwa uzoefu wangu haiwasaidii wote!! Jitahidi kuosha kidevu na maji ya moto baada ya kunyoa na siku nyingine usiku, kisha paka hiyo dawa kila siku. Hii ni uzoefu wangu, si maelezo ya kitaalam! Kwangu imenisaidia kimtindo!
 
Pole sana mkuu, tatizo ulilonalo ni sawa na langu! Hata mimi nimehangaika bila mafanikio, kidevu kimekomaa balaa! By the way, kuna after shave inaitwa BUMP PATROL(sory kwa kuitangaza, ni ktk kusaidiana!) hiyo inasaidia kuondoa mapele na kufanya ndevu ziote vizuri! Lakini, INATEGEMEA NGOZI IMEHARIBIKA KIASI GANI!! Kwa uzoefu wangu haiwasaidii
wote!! Jitahidi kuosha kidevu na maji ya moto baada ya kunyoa na siku nyingine usiku, kisha paka hiyo dawa kila
siku. Hii ni uzoefu wangu, si maelezo ya kitaalam! Kwangu imenisaidia kimtindo!
Thanx much uncle Jei Jei, Pump Patrol nlishaitumia kweli ilinipa afadhali ila tatizo likawa inafika wakati hainisadii tena. Mfano nikifungua chupa mpya naitumia then ikifika nusu hainipi tena matokeo mazuri. Ndo hapo nikaacha kunyoa kwa mashine nikaanza shaving cream ya Magic ipo kwenye tube! Ni gel like substance. Kidogo nayo imenisaidia lakini haijaweza kuondoa kabisa. Huwa kuna kipindi vinashamiri na kipindi vinapungua. Ndo maana nikaona ngoja tuexchange experience
 
Thanx much uncle Jei Jei, Pump Patrol nlishaitumia kweli ilinipa afadhali ila tatizo likawa inafika wakati hainisadii tena. Mfano nikifungua chupa mpya naitumia then ikifika nusu hainipi tena matokeo mazuri. Ndo hapo nikaacha kunyoa kwa mashine nikaanza shaving cream ya Magic ipo kwenye tube! Ni gel like substance. Kidogo nayo imenisaidia lakini haijaweza kuondoa kabisa. Huwa kuna kipindi vinashamiri na kipindi vinapungua. Ndo maana nikaona ngoja tuexchange experience

pride after shave the answer inauzwa 23000 tu hata mtu anamapele ya nyuma ya shingo ambayo yanatoa usaha inaondoa yote ukinunua me nilikuwa ya kidevu yote yameondolewa na situmii maji ya moto wala nini sa hvi npo soft itafute ukishindwa ni pm
 
pride after shave the answer inauzwa 23000 tu hata mtu anamapele ya nyuma ya shingo ambayo yanatoa usaha inaondoa yote ukinunua me nilikuwa ya kidevu yote yameondolewa na situmii maji ya moto wala nini sa hvi npo soft itafute ukishindwa ni pm
Thanx mtaalam! Ngoja niifanyie kazi nikikwama nitakuPM.
 
kikubwa naomba mtafute machine za kunyolea sio za nyembe za kawaida kweli ni gharama 80000 lakin zipo na za chini na sikwenda salon mimi nilikuwa natatizo hilo lakini nilipo nunua machine yangu sijaona tena
 
Wadau naomba msaada wenu mimi tatizo langu nikinyoa ndevu na wembe lazima nitoke mapele na nimejaribu kutumia after shave mbalimbali bila mafanikio lakini nikitumia machine zetu za salon safi hakuna matatizo.
 
1.osha uso na sabuni
2.paka mapovu mengi ya sabuni.
3.tumia wembe mkali eg gillete achama na wembe bei rahisi.
4.nyoa mdevu kwemda chini tu.ukipata vipele baada ya siku 2.nyoa kwa kwemda juu.
na hakikisha hutumii wemnbe zaidi ya siku 70
4.osha uso vizuri paka lotion.
good luck
 
Mimi ninanyoa ndevu kila baada ya siku mbili,yaani naruka siku mbili,nikinyoa mfululizo lazima nitoke vipele,ila cha ajabu ni kuwa situmii mapovu wala shaving cream,ila ninapomaliza kunyoa hiyo siku ya tatu huwa napaka after shave,i use Denim after shave ni cheap kwakweli,unaweza kujaribu utaratibu wangu kwani nanyoa kavukavu kwa kutumia nyembe za Gillete nikimaliza najipangusa na kitambaa kikavu then napaka after shave yangu.
 
Back
Top Bottom