Tatizo la upele Kidevuni: Chanzo na matibabu yake

Nilikuwa na tatizo kama lako. Kwa kweli linakera sana. Nilijarinu kutumia creams za aina mbalimbali lakini haukusadia. Nikatumia pia hizi mashine za kunyolea ndevu nazo hazikusaidia. Katika kutafuta solution ya hili tatizo, nilikutana na article fupi kwenye mtandao ambayo iliuliza kama baba/babu yako alikuwa na ndevu alikuwa anatokwa na vipele akinyoa? Kama jibu ni hapana then walikuwa wanatumia vifaa gani kunyoa ndevu zao? Baada ya kutafakari nikakuta kuwa enzi hizo wazee wetu walikuwa wanatumia vitu simple na basic kunyoa na walikuwa hawatokewi na vipele. Tokea nianze kutumia hizo zana sijawahi kutokewa na vipele tena.

Sisi vijana wa siku hizi tunacomplicate mambo sana. Na hii teknologia imeleta zana mpya lakini nyingi naona wanafanya biashara tuu. Inabidi turudi kwenye basics za kunyoa ndevu. Nikipata muda nitaweka hizo bacics hapa. Ila shaving is supposed to be funny. We need to take our time when shaving. Nakumbuka wazee wangu walikuwa wanachukua zaidi ya nusu saa wakinyoa ndevu. Sie kutokana na sababu mbalimbali within 5 minutes kwisha kazi! Hapo mapele lazima yawepo
 
nilikuwa mtumiaji mkuu wa aftershave nikidhani zinaondoa vipele, wife alinishauri niache hata kwa miezi miwili nione. Vipele vikaisha.

Mara nyingi ninanyoa saloon kwa magic na napata scrubbing na sipaki after shave kabisa na ninaponyoa kwa gillete ni lazime iwe na makali, isiwe butu maana ikiwa butu lazima vipele vinatoka, na kabla ya kunyoa ninanawa maji ya moto au vuguvugu kidogo na kupaka sabuni ya kuogea. nikimaliza sipaki aftershave kabisa.

Sina kipele hata kimoja, I have a very good baby face.

Hakikisha kabla ya kunyoa umeosha uso kwa sabuni na majimoto. Unaponyoa uso ukiwa mchafu, wembe unapokata ndevu uchafu huingizwa kwenye vitundu vidongo sana juu ya uso, uchafu ukiingia ndani vitundu hivyo hufunga na kusababisha uvimbe usoni, uchafu huo hutoka mwilini kwa kugeuza uvimbe kuwa usaha. Hakikisha unatumia wembe wowote wenye makali, na usirudie kutumia mwembe zaidi ya mara moja kunyolea.
 
Natumaini mko salama kabisa hapa jamvini japo kijana mwenzenu niko hoi, nimetokewa na vipele shingoni baada ya kunyoa ndevu na viwili kati ya hivyo vimekua vikubwa na kunipa maumivu mpaka ndani ya koo. Nisaidieni kijana wenu kama kuna mwenye kujua dawa ili nirudi hali ya kwaida nashindwa kufanya kazi
 
Jaribu kutumia dawa inaitwa Bump Patrol. Unapaka baada ya kumaliza kunyoa. Kwa uraisi zaidi nenda kwenye maduka ya S.H Amon lakini unaweza kujaribu sehemu zingine.

wPC9b60j9kIQwAAAABJRU5ErkJggg==
 

Attachments

  • bump_patrol_sas.gif
    bump_patrol_sas.gif
    13.6 KB · Views: 533
kwa uzoefu wangu binafsi huwa suala la kupaka mafuta kwenye kidevu baada ya kunyoa husababisha kupata vipele, hii inanitokea mimi binafsi ingawa bado sijafanya research kwa wengine
so huenda ikawa sababu, jaribu kuepuka kupa mafuta kwenye kidevu
 
Labda nikuulize unaponyoa ndevu kuna kitu chochote unachopaka ili kurahisisha unyoaji? kama vile shaving foam au sabuni? Kwa uzoefu wangu ukitumia shaving foam hasa ya Gillet na Nivea zinasaidia kurahisisha kunyoa.

Pia unaponyoa jitahidi kutumi wembe si zaidi ya mara 2 kwani kutumia wembe uliokwisha makali kunachangia kuleta vipele. Jitahidi unaponyoa uanzie kooni kupandisha kidevuni badala ya kuanzia kidevuni kushuka shingoni.

Point ni kwamba waswahili wengi ndevu zao zinaota kwa muelekeo wa kulala kutokea kidevuni kushuka shingni so ukinyoa kuanzia kidevuni utashindwa kuzitoa kabisa zinabaki kwa kiasi kidogo ingawa wewe unaweza kuona umenyoa zote. Vishina vya ndevu vinavyobaki hujipindia ndani ya ngozi na kusababisha mapele na wakati mwingie hadi kutunga usaha!

Pia tafuta na after shave ya aina niliotaja na unapopaka usipake kama mafuta mwilini bali weka kwenye kiganja then unafanya kama unapandika au unamchapa vibao mtoto! Jaribu hivyo!
 
bump patrol sio nzur inazoea ngoz na hatimae inakuwa haifanyi kaz vzur nunua dawa inaitwa NEO MEDRO NENDA KITUO CHA MABASI MUHIMBILI CHA BUGURUNI UTAPATA CJAJUA UPO SEHEMU GANI M INANISDAIDIA SANA
 
bump patrol sio nzur inazoea ngoz na hatimae inakuwa haifanyi kaz vzur nunua dawa inaitwa NEO MEDRO NENDA KITUO CHA MABASI MUHIMBILI CHA BUGURUNI UTAPATA CJAJUA UPO SEHEMU GANI M INANISDAIDIA SANA
kwa mtindo huu kila mtu atakuja na after shave yake!
Kwako inaweza haikusaidii lakini kwa mtu mwingine inamsaidia!
 
Vipele katika ngozi ni matokeo ya maambukizi ya bacteria. Kitendo cha kunyoa ni kama kufanya jeraha katika shina la nywele hivyo husababisha nafasi kwa bacteria wa ngozi (normal flora) kushambulia kidonda hicho kidogo, body reaction against foreign body (bacteria) huleta inflamation ambayo ndio kipele.

Kuepuka jaribu kutumia nyembe kali ila si kali sana pia si butu kuzuia majeraha, pia ni kitendo cha taratibu si kwa nguvu pamoja na kilainisho shaving jelly yoyote baada ya kunyoa tumia spirit as antiseptic solution kuzuia kuzaliana kwa bacteria hao.

Unyoaji pia unatakiwa kufuata mwelekeo wa muoto anzia ziliko lalia kuliko kwenda against maoteo kwani heleta majeraha zaidi katika shina la nywele. Mf tokea shingoni kupanda kidevuni kuavoid resistance ya nywele. Sometimes mapele yanaweza kutokana na allergy ya kitu furani hivyo tafuta wataalamu zaidi kama havita pona vyenyewe (spontaneously)
 
kwangu mimi huwa natatizo hilo nilijaribu dawa za kila aina bila mafanikio ila nikapata ushauri kuwa nisinyowe nikamaliza zote pia nisikae kwa mda mrefu bila kunyoa tokea siku hiyo sina tena tatizo hilo.
 
msaada jamani izi ndevu zna nizeesha, naomba ushauri wa mashine nzuri au jinsi gani ntaweza kuwa nazinyoa au kuzitoa bila kubakiza alama na vipele. nimejaribu magic na cutting machines za saloon tatizo bado linaendelea
 
kwanza nikupe pole...nunua machine za kukatia nywele original siyo feki,sababu haziwi za moto kwa mda mrefu..hiyoi inatakufanya ngozi yako kutoungua.nyoa na machine yako taratibu..bila kukwangua hadi ngozi then baada ya hapo chukua taulo lenye majimaji ya uvuguvugu sijafishe kwenye kidevu chako..mapele yatakwenda yanapungua taratibu mpaka kwisha,then unaweza kuendelea kunyoa kwa kusugua kidevu mpaka ndevu zote zinakwisha hapo mapele yatakuwa yalikwisha kauka mda mrefu..

TAFADHALI;usipakae powder walaspirit au mafuta yoyote yale kabla kunyoa au baada ya kunyoa.
 
Tumia machine original kunyolea halafu ukimaliza paka "after shave original"....tatizo lako kwishney!
 
kwanza nikupe pole...nunua machine za kukatia nywele original siyo feki,sababu haziwi za moto kwa mda mrefu..hiyoi inatakufanya ngozi yako kutoungua.nyoa na machine yako taratibu..bila kukwangua hadi ngozi then baada ya hapo chukua taulo lenye majimaji ya uvuguvugu sijafishe kwenye kidevu chako..mapele yatakwenda yanapungua taratibu mpaka kwisha,then unaweza kuendelea kunyoa kwa kusugua kidevu mpaka ndevu zote zinakwisha hapo mapele yatakuwa yalikwisha kauka mda mrefu..

TAFADHALI;usipakae powder walaspirit au mafuta yoyote yale kabla kunyoa au baada ya kunyoa.

ahsante sana mdau kwa ushauri naenda game kutafta original machine
 
Ukishanyoa tumia "bump patrol" kila siku, itaondoa vipele vyote.
 
Kuna dereva mmoja wa dala dala alikamtwa pale lugalo wakamleta kikosini niliona vijana wakimnyoa ndevu na mikono yani walikua wakimnyofoa nafkiri inaweza ikawa tiba nzuri ila alikua anapiga kelele sijui walikua wanampaka spirit sina hakika!!!
 
Pole kuna mtu ana ndevu utafikiri sisimizi wapo kwenye sukari na kidevu cheusiiii tiii dawa yake usiwe unanyoa mara kwa mara ndevu(I means daily) acha hata siku 12) then usitumie spirit inakomaza kidevu na kua kama chuma chenye kutu
 
Back
Top Bottom