Tatizo la upele Kidevuni: Chanzo na matibabu yake

Omumura

JF-Expert Member
Aug 20, 2009
476
18
1591096579145.png


BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA KUHUSUNSHIDA HII
Jamani wana JF naombeni msaada wa ushauri wenu kwani kwa muda mrefu sasa ninasumbuliwa na tatizo la kutoka mapele ya ndevu mara baada ya kunyoa, nimejaribu aftershave nyingi tu lakini naona bado hazijanikubali.

Kwa sasa hivi nilikuwa natumia aftershave iitwayo Bump Patrol!
---
Ndugu wanajamvi, naomba mnisaidie hili la vipele vya ndevu. Kama mjuavyo sio waafrika nywele na vinyweleo vyetu huota kwa kujikunja ikiwa ndani ya ngozi(spiral growth) tofauti na wazungu au wahindi ambao zao huota zimesimama.

Vilevile miongoni mwetu waafrika kuna ngozi ambazo haziathiriwa na outaji huo kwani nywele inatoka hadi nje ya ngozi kwa style hiyo hiyo.

Tatizo linalonikabili mie ni kwamba ndevu nyingi hazioti na kutoka nje ya ngozi, zinazuliwa ndani bila shaka ukuaji wa spiral/coil hivyo kusababisha ngozi kutengeneza kipele kwa juu. Pindi inapofanikiwa kuchomoza juu ya ngozi kipele hukauka na kupona. Ila isipoweza kuchomoza huwa inatengeneza kipele kwa muda mrefu hadi ntakapoivutwa nje ya ngozi.

Nimeshafanya jitihada za kutumia mashine tofauti tofauti za kunyolea na pia shaving cream za magic zenye strengths tofautitofauti bila mafanikio. Mwenye ufahamu, uelewa na experience yoyote ambayo inaweza nisaidia animwagie hapa jamvini tafadhali. Urembo wa ndevu siufurahii mwenzenu.
---
Wana JF habarini?

Wajameni ni changamoto kila nikinyoa ndevu vipele huwa vinaniota sana hasa nikitumia wembe, nimeamua kununua mashine ya kunyolea ila bado vinaniota.

Kila nikimaliza kunyoa huwa napaka spirit ila huwa vinaota tu.

Naomba kama kuna anayefahamu after shave nzuri ambayo nikipata vipele havioti anisadie...
---
Morning!

Hope mmeamka vizuri na siku yetu njema hii ya Jumanne!

Wakuu naomba msaada kwa anayejua dawa nzuri ya kuzuia maupele.Kuna rafik yangu baada ya siku mbili kunyoa ndevu upele unamsumbua sana na kidevu kinawasha mno.

Ananyoa kwa kutumia machine.

Ashatumia magic bado haikusaidia

Kila akitaka kunyoa na baada lazma atumie poaa na maji ya moyo.

After shave za aina nying ashatumia hamna msaada.Kama kuna option nyingne anaomba msaada either dawa za asili au za kizungu!

Muwe na siku njema.Stay blessed!

UFAFANUZI WA JUMLA WA TATIZO HILI
Kwa wastani binadamu anatumia miezi (5) mitano ya maisha yake kunyoa na ndani ya miezi hiyo mitano kwa mwanaume atashave mara elfu 20,000 katika muda wa maisha yake yote. Baadhi ya watu huchukia kabisa ikifika kipindi cha kushave kutokana na changamoto wanazozipata wakati na baada ya kushave. Kushave kuna changamoto nyingi, haijalishi ni unashave ndevu (mwanaume), sehemu za kwapa au sehemu nyeti.

Changamoto hizo zinaweza kuwa

1. Kupata vipele baada ya kunyoa hasa kwenye maeneo yanayozunguka kidevu, kwapani na weusi.

2. Ngozi kuwasha, kutokana na ukavu unaosababishwa na spirit au bidhaa yenye alcohol inayopakwa kweny ngozi.

3. Kupata weusi baada ya michubuko na vipele baada ya kunyoa kupona vinaacha weusi sehemu husika.


Changamoto hizi zinachangiwa zaidi na bidhaa na vifaa tunavyotumia kunyolea. Sio wote wanapata vipele na weusi, ila kwa wale wenye vipele na weusi kwenye maeneo wanayoshave, hiyo inachangiwa na vitu vifuatavyo:

1.kushave bila kulainisha ngozi

2.Kupaka spirit au aftershave yenye alcohol baada ya kushave

3.kutokupaka kitu chochote baada ya kushave

4.kutumia blade ama kiwembe kisicho na makali.

Ufanye nini ili usipate vipele na uondoe weusi?

1. Lainisha ngozi kabla ya kunyoa

Ni muhimu kulainisha ngozi yako kabla ya kunyoa kwa, layer ya juu ya ngozi ina chembe hai zilizokufa, ukilainisha ngozi kabla ya kunyoa itasaidia kuondoa na chembe hai zilizokufa wakati wa kunyoa, pia itasaidia wembe kuteleza vizuri kwenye ngozi bila kusababisha michubuko.

2. Tumia aftershave baada ya kunyoa.

unatakiwa kutumia aftershave ili kupoza ngozi, kuipa unyevu nyevu na kufanya nyororo. Spirit na aftershave zenye alcohol zinafanya ngozi kuwa kavu, itasababisha miwasho na ukijikuna ndo inapelekea kutoka vipele.

3. Nyoa kufatisha muelekeo wa nywele zilivyoota.
Hii itasaidia ngozi isiume zaidi wakati wa kunyoa. Pia hakikisha kiwembe au blade unayotumia kunyolea ni kikali, kikiwa butu Utarudi mara nyingi na kuumiza zaidi ngozi.

4. Usitumie deodorant yenye chumvi ya aluminum na alcohol.
Chumvi ya aluminum na alcohol inachangia kufanya ngozi iwe kavu na kuwasha baada ya kunyoa ambayo itapelekea kupata weusi wa kwapa.

Credit: Aloe life style
MAONI NA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA BAADHI YA WADAU:
Dawa ya kuondokana na Vipele vya ndevu ni ndogo sana.​

Endapo unatumia wembe iwe gelete au aina yoyoyote ya wembe ikiwa ni pamoja na magic shave acha mara moja.

Wembe hukwangua ndevu mpaka mwisho na hivyo kufanya ile ncha ya ndevu kuwa kali sana wakati inapoanza kuota tena. Hi hufanya ngozi kuvimba kwa sababu ule mzizi wa ndevu huichoma ngozi ili ndevu iweze kutoka na hivo kuifanya ngozi kuvimba na ndio hicho mnachokiona ni vipele. Hivyo vipele ni matokeo ya ndevu kusukuma ngozi ili iweze kujitokeza nje hivyo kuifanya ngozi kuvimba. matatizo haya huwakuta sana waafrika kwa sababu nywele za kaifrika ni ngumu na huwa na ncha kali kutokana na asili ya nywele zatu na hivo kusababisha kuichoma ngozi wa nguvu sana.

SULUHISHO
Ukitaka kuondokana na vipele hivi, unachotakiwa kufanya ni kuachana na kutumia wembe. Tumia mashine ya kunyolea ndevu kwani mashine kwa bahati nzuri huwa hauwezi kukwangua na kumaliza nywele zote kama ilivyo wembe.
---
Acha kunyolea wembe wa kawaida huo ndio ushauri, nunua mashine kama bado hujanunua endapo bado vipele vinaendelea nunua TRIODERM tube ambayo imechanganywa Betamethasone, Gentamycin na Tolnaftate.

Paka tube hii mara chache tu pale unapoona ndio kuna tatizo la vipele, muwasho au kama kuna makovu yaliyojitokeza baada ya kupata vipele itaviondoa na utakua soft.

Kuna nyingine inaitwa SKDERM CREAM hii pia itasaidia kukuondolea mapele hayo lakini paka sehem husika tu hapo hapo kidevuni kwenye vipele itaondoa vipele na weusi kisha utabaki ma ngozi yako ya kawaida. Usipake uso mzima kwasababu utakua mwenye uso angavu kama mabinti wapenda urembo sababu inafanya ngozi kuwa nyeupe kiasi kama ni binti sawa lakini kama ni mwanaume na haupendi mambo ya kuonekana una ngozi angavu kidogo paka kiasi tu.

Baada ya kupona uwe unatumia maji vuguvugu kuosha sehem uliyonyoa na upake 'Vaseline' kama ngozi yako ni kavu pia kama ngozi yako inamafuta mengi pakaa 'Vestline snow'.

Yangu ni hayo na ndio huwa natumia na sijawai kupata shida tangu nianze kutumia lakini kabla sijaanza kutumia njia hii nimepata shida sana hizo Aftershave hazina msaada utahangaika bure hazina tofauti na Bump Patrol Original formula. Ni usanii tu zinafanana tu na spirit labda kazi yake ni kuua bakteria lakini sio kutibu vipele.

Mkorintho wa 6
---
Salaama ndugu zangu

Ni kweli kwamba vipele vya ndevu ni tatizo kubwa kwa watu wengi. Tatizo hilo linasababishwa na hair ingrowth zinapoanza kurefuka baada ya kunyolewa au skin inflammation associated with pus forming bacterial infection. Tatizo la hair ingrowth linawasumbua wale ambao ndevu zao ni curled yaani badala ya kurefuka away from the skin zenyewe zinachomoza kidogo kwenye ngozi then zinaota kuelekea ndani ya ngozi.

Kwahiyo ile sehemu ambayo nywele inaingia inavimba amabapo inaonekana kipele. Ukiwa makini siku 3 baada ya kunyoa jichunguze vizuri kwa kutumia kioo utaweza kuona nywele nyingi zipo ndani ya ngozi na kupata muwasho amabao unasababishwa na irritation ya hizo nywele kwenye ngozi. Watu wengine wanatumia kitu chenye ncha kali na kuzichomoa hizo nywele then vipele vinapungua.

Pia utaweza kuona vipele amavyo vimepata infection na kutoa usaha. Kwahiyo kujikinga na tatizo la hair ingrowth ni kwamba usiruhusu nywele kuota na kufanya U- turn na kurudi kwenye ngozi.

Ukiwa mtumiaji wa mashine ya kunyolea na haupendi kuwa na ndevu inakubidi unyoe kila siku lakini wengi wao wanasumbuliwa na ngozi kuvimba na kupata bacterial infection ambapo utapata maumivu ya ngozi! Otherwise tumia mashine ambayo itazibakiza bila kuzikata hadi level ya ngozi ambapo hautopata tatizo la hair ingrowth na vipele havitakusumbua.

Pia unaweza tumia shaving creams au powder mfano magic ambayo nami naitumia bila kupata madhala ya kutokwa na mapele. Unapotumia powder au cream hakikisha hauruhusu ndevu kuota. Huo ni ushauri wangu kwa leo
---
Vipele katika ngozi ni matokeo ya maambukizi ya bacteria. Kitendo cha kunyoa ni kama kufanya jeraha katika shina la nywele hivyo husababisha nafasi kwa bacteria wa ngozi (normal flora) kushambulia kidonda hicho kidogo, body reaction against foreign body (bacteria) huleta inflamation ambayo ndio kipele.

Kuepuka jaribu kutumia nyembe kali ila si kali sana pia si butu kuzuia majeraha, pia ni kitendo cha taratibu si kwa nguvu pamoja na kilainisho shaving jelly yoyote baada ya kunyoa tumia spirit as antiseptic solution kuzuia kuzaliana kwa bacteria hao.

Unyoaji pia unatakiwa kufuata mwelekeo wa muoto anzia ziliko lalia kuliko kwenda against maoteo kwani heleta majeraha zaidi katika shina la nywele. Mf tokea shingoni kupanda kidevuni kuavoid resistance ya nywele. Sometimes mapele yanaweza kutokana na allergy ya kitu furani hivyo tafuta wataalamu zaidi kama havita pona vyenyewe (spontaneously)
---
Hili ni tatizo ambalo hata nami nimekutana nayo sana miaka kadha iliyopita

Elimu aliyotoa mhalisi ni nzuri lakini Mi naona bado haimalizi tatizo tajwa.

Fanya hivi,Acha ndevu ziote usiogope kabisa, hata unaweza acha kama mwezi moja hivi. Maana ukiacha ndevu hivyo yale maupele yanapungua ama kwisha kabisa.

Sasa siku ya kwenda kunyoa hakikisha kabisa una kangua yote na ikiwezekana tumia wembe na hakikisha kbs una LIMAO moja hata mbili mkononi.

Ukimaliza tu kunyoa kata limao ktkt na pakaa kote kwenye usawa wa ndevu! Hata kesho yake pakaa tena!
Halafu kama unatumia wembe sasa hakikisha baada ya siku tatu tena pitisha wembe tena na pakaa limao na hapo mwenyewe utaleta majibu hapa kwamba Jamiiforums kuna kila aina ya mtu.

Pole sana Kamanda!
---
1.osha uso na sabuni
2.paka mapovu mengi ya sabuni.
3.tumia wembe mkali eg gillete achama na wembe bei rahisi.
4.nyoa mdevu kwemda chini tu.ukipata vipele baada ya siku 2.nyoa kwa kwemda juu.
na hakikisha hutumii wemnbe zaidi ya siku 70
4.osha uso vizuri paka lotion.
good luck
---
Tatiza ni kuwa sisi tuko wengine tuna nywele ngumu sasa ukinyoa kwa kukwangua zote huwa ngozi kama inavimba kwa ile distance ya mkwaruzo wakati wa kunyoa.

Sasa hii inasababisha yale mashina ya nywele zilizokatwa kuwa chini ya ngozi na kuanza kutoboa njia nyingine wakati wa kuota
Hii hupelekea kupatwa na vipele ambavyo vinasababishwa na michomo ya zile mashina zinazotaka kuota lakini zinatoboa njia nyingine
Dawa nikunyoa lakini tumia mashina ambayo hutakwaruza lazima hakikisha unaziacha kama vile zinaota na usikwangue hadi chini sana.

Maana yake ngozi inavimba na yale mashina yanapoteza uelekeo wa ile ya zamani na yanatoboa njia nyingine. Hili tatizo huwa haliwapati kabisa wale wenye nywele laini kama wahindi waarabu na wengine kama hao. Hiyo ndo dawa na wengine tukinyoa kile kipara cheupe cha wembe lazima vipele vitokee na tatizo ndo hilo

Au fuga ndevu kama vijana wa sikuhizi naona kila mtu kaacha ndevu
---
Pole sana kiongozi kwanza napenda nikushauri kabla ya kupata tiba kwanza tafuta kujua sababu ya wewe kutoka vipele. Usikimbilie kutibu vipele.

Hilo tatizo ni common sana kwa watu wengi, lakini wengi huwa wanakimbilia madawa na wanashindwa,

Nakushauri kwanza tatizo hili husababishwa na friction ya mashine unazotumia wakati wa ku shavu. Unakuta mtu anakwanguliwa na mashine ilikutoa nywele zote,

Jaribu njia hii kuzuia

1. Tafuta salon moja utakayokuwa unaenda kushavu.

2. Hakikisha unaponyoa ndevu usizitoe zote na kinyozi asiku kwangue ngozi akunyoe juu juu tu.

3. Hakikisha mashine anayotumia ni safi kama utapata ya kwako kwaajili ya ndevu itapendeza.

4.osha kidevu chako kwa maji ya uvuguvugu baada ya kunyoa.

5.kunywa maji ya kutosha

NB
Kwa sasa kwakuwa ngozi imeharibika acha kwa muda wa mwezi 1 usinyoe ndevu, ngozi itarudi kwenye hali yake.
 
ni tatizo letu sote ila lina tatulika mkuu kabisa mkuu uwa na2mia poda fulani ina dawa napewaga na mnigeria ipo safi cku izi ata c2mii cana kama vp nipm 2saidiane mkuu
 
Mmmh jamani huu ndo ugonjwa wangu mkuu, NIMEMALIZA dawa zote, kilichonisaidia kidogo nilinunua mashine kama ya saluni nimeitumia, ikaibwa mota, nikanunua nyingine elfu sabini, juzi mtoto kaiangusha imeharibika, nimenunua bump patrol, mmh maendeleo madogo! sasa nanyoa daily kisha ndo napaka hio bump control! pls nisaidieni pia
 
Bump Patrol za sasa hivi nahisi zinachakachuliwa. Mwanzoni wakati zinaingia zilikuwa effective sana lakini haya matoleo ya sasa ni kama spirit tu ya kawaida!
 
Poleni sana wanyoa ndevu wenzangu. Mimi nilikuwa natatozo hilo lakini niliamua achana na viwembe vya kunyolea including gillete wanavyo sema ni nzuri, kwa sasa natumia mashine ya kunyolea, kwa sasa tatizo hilo limekwisha kabisa. nikitumia mashine sipati kipele hata kimoja.
 
wazee hili ni janga la kitaifa . embu tusaidiane kuambiana tutumie kitu gani ili tuondokane na huu usumbufu wa vipele vya ndevu.
 
tupo wengi mkuu
mwenye kujua atujulishe ila mimi huwa situmii gillete..natumia shaving mashine...nikikusa gilette tu nimekwisha
Nilikuwa mtumiaji mkuu wa aftershave nikidhani zinaondoa vipele, wife alinishauri niache hata kwa miezi miwili nione. Vipele vikaisha.

Mara nyingi ninanyoa saloon kwa magic na napata scrubbing na sipaki after shave kabisa na ninaponyoa kwa gillete ni lazime iwe na makali, isiwe butu maana ikiwa butu lazima vipele vinatoka, na kabla ya kunyoa ninanawa maji ya moto au vuguvugu kidogo na kupaka sabuni ya kuogea. nikimaliza sipaki aftershave kabisa.

Sina kipele hata kimoja, I have a very good baby face.
 
Isisahaulike option ya kutokutumia wembe au mashine kabisa. Sio lazima uwe Osama - unaweza kupunguza kwa mkasi.
 
ukinawa kwa maji moto baada ya kunyoa inasaidia sana, wembe noma tumieni mashine tu
 
Mkuu unatumia wembe? kama unatumia wembe acha tumia mashine kama wanazotumia vinyozi. baada hapo pakaza B&C SKIN TIGHT ni kiboko hii kesho yake tu ukiamka utaona tofauti.endelea siku mbili tatu vitapotea kabisa acha kutumia siku ukikata ndevu tena pakaza kidogo hivyo hivyo na utaona tofauti yake.
 
Tatizo langu mimi ni kwamba nikiacha ndevu ndo vipele vinakuja na ndevu zinaanza kuniwasha, zingekuwa haziwashi ningekuwa napunguza tu kwa mkasi. So tatizo nini hapa?
 
Dawa ya kuondokana na Vipele vya ndevu ni ndogo sana.

Endapo unatumia wembe iwe gelete au aina yoyoyote ya wembe ikiwa ni pamoja na magic shave acha mara moja.

Wembe hukwangua ndevu mpaka mwisho na hivyo kufanya ile ncha ya ndevu kuwa kali sana wakati inapoanza kuota tena. Hi hufanya ngozi kuvimba kwa sababu ule mzizi wa ndevu huichoma ngozi ili ndevu iweze kutoka na hivo kuifanya ngozi kuvimba na ndio hicho mnachokiona ni vipele. Hivyo vipele ni matokeo ya ndevu kusukuma ngozi ili iweze kujitokeza nje hivyo kuifanya ngozi kuvimba. matatizo haya huwakuta sana waafrika kwa sababu nywele za kaifrika ni ngumu na huwa na ncha kali kutokana na asili ya nywele zatu na hivo kusababisha kuichoma ngozi wa nguvu sana.

SULUHISHO
Ukitaka kuondokana na vipele hivi, unachotakiwa kufanya ni kuachana na kutumia wembe. Tumia mashine ya kunyolea ndevu kwani mashine kwa bahati nzuri huwa hauwezi kukwangua na kumaliza nywele zote kama ilivyo wembe.
 
Kuna hii inaitwa Calmurid cream, sina uhakika na availability yake hapo bongo lakini is effective na resuls is just in a day or two, lakini unatakiwa kuendelea kuitumia kama utaendelea kunyolea wembe!
 
Salaama ndugu zangu

Ni kweli kwamba vipele vya ndevu ni tatizo kubwa kwa watu wengi. Tatizo hilo linasababishwa na hair ingrowth zinapoanza kurefuka baada ya kunyolewa au skin inflammation associated with pus forming bacterial infection. Tatizo la hair ingrowth linawasumbua wale ambao ndevu zao ni curled yaani badala ya kurefuka away from the skin zenyewe zinachomoza kidogo kwenye ngozi then zinaota kuelekea ndani ya ngozi.

Kwahiyo ile sehemu ambayo nywele inaingia inavimba amabapo inaonekana kipele. Ukiwa makini siku 3 baada ya kunyoa jichunguze vizuri kwa kutumia kioo utaweza kuona nywele nyingi zipo ndani ya ngozi na kupata muwasho amabao unasababishwa na irritation ya hizo nywele kwenye ngozi. Watu wengine wanatumia kitu chenye ncha kali na kuzichomoa hizo nywele then vipele vinapungua.

Pia utaweza kuona vipele amavyo vimepata infection na kutoa usaha. Kwahiyo kujikinga na tatizo la hair ingrowth ni kwamba usiruhusu nywele kuota na kufanya U- turn na kurudi kwenye ngozi. Ukiwa mtumiaji wa mashine ya kunyolea na haupendi kuwa na ndevu inakubidi unyoe kila siku lakini wengi wao wanasumbuliwa na ngozi kuvimba na kupata bacterial infection ambapo utapata maumivu ya ngozi! Otherwise tumia mashine ambayo itazibakiza bila kuzikata hadi level ya ngozi ambapo hautopata tatizo la hair ingrowth na vipele havitakusumbua.

Pia unaweza tumia shaving creams au powder mfano magic ambayo nami naitumia bila kupata madhala ya kutokwa na mapele. Unapotumia powder au cream hakikisha hauruhusu ndevu kuota. Huo ni ushauri wangu kwa leo
 
Nilikuwa mhanga pia, ila kwa sasa natumia gillette disposable na shaving cream ya gillette, also nivea shaving cream can do. Situmii after shave! Softiii!
 
Back
Top Bottom