Dawa ya kukojoa mkojo wa manjano (yellow)

mjita

Member
Nov 6, 2011
12
0
Wana jamii naombeni msaada wenu nina tatizo la kukojoa mkojo wa njano sana kwa muda wa miaka mitatu sasa nimekwenda hospitali lakini inaonekana sina tatizo, naomba kujua dawa yake nn wana jamvi. Tatizo hili limekua ni kero kwangu hata ninywe maji mengi vip baada ya muda mfupi tu hali inajirudia tena.
 
Huenda Unakunywa vinywaji strong sana vinavyosababisha dehydration kubwa kwenye mwili!
 
Ina wezekana we ni mshabiki damu wa Yanga au CCM.

Anyways, kunywa maji kutwa mara 12, jumla lita 3 kwa kwa siku.
 
mjita jitahidi kunywa maji mengi sana usichoke, hali itabadilika
 
Last edited by a moderator:
Maji na kutafuna matango mengi ni suluhu ukinywa dawa yoyote unaongeza tatizi
 
Lakini hiyo si ndio rangi ya mkojo? Au njano imepitiliza kama rangi ya yunifom za ze magambaz?
 
Kunywa maji mengi na punguza kula vyakula vyenye protini nyingi...
 
Situmii pompe ya aina yoyote wana jf na ninatumia maji ya kutosha mpaka kero ila baada ya muda mfupi hali inajirudia. Asanteni kwa ushauri wenu
 
Mimi napenda mnisaidie kuna nduguyangu wa kiume anaumwa maeneo ya chini ya kitovu kwenye kinena,nakila wakati anahisi kukojoa na akienda kujisaidi haja ndogo anapata mkojo kidogosana,je nini matibabu yake?na itakua ni tatizo gani?inamsumbua zaidi ya miaka 10 sasa,msaada wenu wadau.
 
Situmii pompe ya aina yoyote wana jf na ninatumia maji ya kutosha mpaka kero ila baada ya muda mfupi hali inajirudia. Asanteni kwa ushauri wenu

Unaweza kunywa maji mengi bila ya mpangilio. Unatakiwa kila baada ya masaa mawili unywe maji glass moja kubwa au nusu lita ya maji kunzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku.
 
Hata mimi nlikua na tatizo kama hilo mara tu nlipokuj Dar ila maji mengi yalikua tiba baaaabu! wa jf naomba mnisaidie jinsi ya kutupia title kwenye jf. nawasilisha wakuu.
 
Situmii pompe ya aina yoyote wana jf na ninatumia maji ya kutosha mpaka kero ila baada ya muda mfupi hali inajirudia. Asanteni kwa ushauri wenu

Nina hofu kuwa shida yako iko kwenye figo. Nikushauri hivi, tafuta mchaichai utakusaidia. Acha kunywa kahawa na chai na kitu chochote chenye caffein.

Na kama unatumia chumvi kwa wingi punguza matumizi ya chumvi.
 
Ina wezekana we ni mshabiki damu wa Yanga au CCM.

Anyways, kunywa maji kutwa mara 12, jumla lita 3 kwa kwa siku.

Fomula ya kunywa maji ni: bordy weight x 0.04= quantity in litres (Uzito wa mwili mara 0.04= jumla ya lita unazotakiwa kunywa kwa siku). Kwa mfano kama una uzito wa kilo 90. Utatakiwa unywe lita 3.6. kama una uzito wa kilo 60 utatakiwa unywe lita 2.4 kwa siku n.k.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom