Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,843
- 2,664
Huu ugonjwa upo sana na utambuzi wake ni mgumu. Naomba kupata empirical data na evidence kuhusu kipandauso pamoja na dawa (za kienyeji na kisasa) pamoja na wapi matibabu yanapatikana. Kuna mdau anahisi anacho.
MASWALI YA WADAU WENGINE KUHUSU UGONJWA HUU
Nimekuwa na tatizo hilo tangu 2003, kadiri siku zilivyokuwa zikienda mbele ndiyo tatizo lilikuwa likikuwa na kuwa hatari kwa afya yangu.
Nimekuwa nikitumia sumatriptan 100 mg toka 2010, na Mwaka huu nimenadilishiwa dawa, dawa hizo ni jamii ya triptan, zinaitwa RIZACT-10. Nimetumia anti pain/pain killers Kama Panadol na Hedex mpaka nimechoka. Kuna Dr. Alinishauti nichome sidano za Botox kwani ndiyo treatments for chronic migraine, nilienda India, Apollo Hospital na kuchoma hizo sindano lakini hakuna nafuu yeyote toka nichome hizo botox mapema Mwaka huu. Nilienda India January 2013. Mpaka sasa bado natumia hizo RIZACT-10 lakini nafuu ni ya mda mchache tu.
Wanajamvi naamini ninyi mnaweza kuwa msaada kwa huu ugonjwa wangu ulionisumbua kwa miaka 10 sasa. Kiswahili chake huitwa kipanda USO. Ki ukweli nimekuwa mimekuwa non productive kwa shughuli zangu za kila siku. Kila mda kichwa kinauma tena sana, wakati mwingine natapika sana mpaka nichome sindano za pain killer ndo napata nafuta.
Yeyote anayejua dawa ya haya maumivu makali ya kichwa tafadhali nisaidieni tena kwa gharama yeyote kwani ninateseka sana. Tafadhali nisaidieni ndugu yenu ninsteseka mno na haya maumivu mskali ya kichwa.
Habari za asubuhi wapendwa,
Kwa yeyote ajuae dawa ya kipanda uso naomba aniambie maana uvumilivu umenishinda!.
Huwa nasumbuliwa sana na kichwa, maumivu huwa nayasikia kuanzia utosini mbka kwenye paji la uso ambayo husababisha macho yaume pia.
Nimejaribu kunywa pain killers ila ndo kwanza kimezidi!
Habarini, naomba msaada kwa hili tatizo; mi ninapata mumivu makali sana ya kichwa katika paji la uso pale ninapo tizama vitu vyenye mwanga hususani mkali, vitu hivyo ni luninga, computer, simu ya mkononi n.k , nikitizama vitu hivi kwa muda fulani mwanga wake unanitanya macho kuuma ikiambatana na maumivu makali sana ya kichwa katika paji la uso.
Pia mimi ni mkandarasi hivyo asilimia 100% ya muda wangu wa kazi ni juani na ninapokaa juani kutwa nzima napatwa na maumivu makali ya paji la uso, khari hii imedumu kwa takribani miaka 10 na wakati mwingi nashindwa kufanya kazi kwasababu ya tatizo hili, na tangu 2004 mpaka sasa nimekuwa na tatitizo la maimivi makali ya kichwa maeneo ya kisogoni nimefanya CT scan na MRI muhimbili hazikuona tatizo katika kichwa na kutumia dawa za nerves bila mafanikio pia miwani nimevaa kwa muda wa miezi 6 bila mafanikio, imefikia wakati hata mwajili wangu kutaka kuni simamisha kazi kwa ajili ya tatizo hili,jamani kwa mwanye kujua tiba ya tatizo hili anisaidie.
Hello!
Jaman nasumbuliwa na haka kaugonjwa kanaitwa "kipanda uso" yaani kunakuwa na maumivu ya kichwa upande mmoja hasa usoni. Mwenye kujua dawa zinazotibu au kupunguza tatizo hili anisaidie.
Natanguliza shukrani.
MICHANGO YA WADAU
Kuumwa na kichwa kumegawanyika sehemu kuu nyingi sana japo kuwa 1% yake ni ashirio la matatizo ya kiafya ambayo yame-advance. Kama vile concussion of brain,meningitis,encephaliti, na stroke. Kuumwa na kichwa pia inawezatokana na matatizo ya taya, meno au hata kula vitu vya baridi zaidi. Vyakula vyenye nitrite au monosodium glutamate.
Sehemu ambazo huuma ni kama ifuatavyo:
- Mfumo wa fahamu ambao upo kwenye fuvu la kichwa.
- Baadhi ya neva za fahamu zilizoko usoni
Misuli ya kichwani
Mishipa inayopatikana kwenye fuvu la kichwana chini ya ubongo kuna mifumo ya fahamu yenye hisia. Kumbuka fuvu na tishu za ubongo kwa zenyewe haziumi kwani hazina mifumo ya fahamu ambayo inahisia.
Mambo haya 12 nayo yanahusika sana.
1: Nervous tension headaches;
Ni maumivu ya kichwa endelevu upande mmoja au pande zote za misuli ya shingo na upande wa juu wa mgongo,kuumwa na kichwa pamoja na kusinzia. Tumia vitamin b2 na c , ounguza au acha matumizi ya sukari,kahawa,chakula chenye kukusababishia mzio,misongo ya mawazo na ufanye mazoezi yakutosha.
2: Cluster headaches;
Kichwa kuuma haswa upande mmoja wa kichwa kwa maumivu makali, machozi humtoka mtu na makamasi kwa mbali. Kitu cha kwanza ni kutumia chakula chenye protein ya kutosha, epukana na chakula chenye mzio kwako.
3: Hangover headaches;
Hii ni hali ya kichwa kuuma kwa sababu ya matumizi makubwa ya vinywaji vikali haswa pombe. Weka barafu chini ya kichwa yaani maeneo ya kichogoni au shingoni,kunywa maji mengi na juice ya matunda freshi na uache pombe.
4: Exertion headaches;
Hutokea pale ambapo mwili utatumika sana na haswa kwenye ngono. Weka barafu linalouma, kula mlo kamili na usifanye mazoezi.
5: Caffein headaches;
Hali hii hutokea pale ambapo umeacha matumizi makubwa sana ya kahawa kwa ghafla. Kunywa kiasi kidogo cha kahawa kuondoa maumivu na upunguze matumizi kidogokodogo mpaka utakapo acha kabisa.
6: Sinus headaches;
Maumivu haya huanzia upande wa kulia na kushoto wa pua na kupanda mpaka kichwani. Kula vitamini C kwa wingi na umuone mtaalamu wa afya maana saa zingine hii utkana na maambukizi.
7: Bilious headaches;
Kichwa na macho huuma haswa kipanda uso na husababishwa na kula sana, kula vibaya, kutofanya mazoezi na kukosa choo. Fanya mazoezi na kunywa maji yakutosha na kasha fanya enema.
8: Hunger headaches;
Maumivu ya kichwa ambaya husababishwa na kutokula kwa muda. Kula chochote ilimradi kiwe ni protein au carbohydrates .
9: Eyes ram headaches
Haya ni maumivu yanayotokea kwenye macho na wengi hudhani labda wameangalia vibaya japo saa zingine inaweza kuwa sababu. lakini chanzo chake haswa ni ubongo kufanya kazi kupita kiasi. Badili mtindo wa maisha na kama ni mtumiaji wa miwani ni vyema ukamuana mtaalamu aangalie kama lensi zimepotea nuru au la.
10: Menstrual headaches;
Hali hii hutokea kwa kina mama kipindi cha yai kupevuka. Hutokana na mabadiliko ya hormone, muone mtaalamu wa afya.
11: Arthritis headaches;
Haya ni maumivu ya kichwa yanayosikika mpaka shingoni na saa zingine mpaka mgongoni ambayo husababisha maumivu haswa unapozidisha mwendo au shughuli. Kitu kikubwa ni kutibu ugonjwa unaosababisha hali hiyo.
12: Hypertension headaches;
Ni maumivu ya kichwa chote, mwendo mkubwa pia huongeza maumivu. Hali hii husababishwa na shinikizo la damu. Tibu au pambana kushusha shinikizo la damu na halii itaisha bila shaka.
Kabla ya kukupa dawa na ushauri wangu nina maswali nikuulize unijibu.
Je unapata Usingizi wa kutosha? Unalala usiku masaa mangapi? Je, unakunywa maji ya kutosha? Una miaka mingapi? Unapata haja kubwa ya kutosha? Nenda pia kapime macho yako na ukapime tena kwenye mishipa yako ya fahamu huenda una matatizo. Na kitu kingine unakuwa upo juani uwe unavaa kichwani kofia.
DALILI ZA KIPANDA USOKipanda uso (Migraine) ni ugonjwa au maumivu makali ya kichwa anayokuwa nayo mtu baada ya mshipa wa damu (Enlargement of Artery ) kutanuka katika kichwa chake.
Baada ya kutanuka kwa mishipa hii ya damu, pia kuna kemikali ndani ya mwili zinazozalishwa na kuizunguka mishipa hii na kupelekea mtu apate maumivu makali ya kichwa na kutanuka zaidi kwa mishipa.
Maumivu makali ya kichwa hupelekea mfumo wa utendaji kazi wa mwili pia ubadilike, mtu atapatwa na kichefuchefu, kutapika, kuharisha, katika utumbo chakula hakitanyonywa vizuri kiingie mwilini, mtu atashindwa kuona vizuri maeneo yenye mwanga na kutopenda kukaa mazingira yenye sauti au kelele.
Vipo vitu mbalimbali vinavyoweza kuchangia mtu apate tatizo la kipanda uso, vitu hivi haimaanishi kuwa ni lazima kusababishe upate na hata kama haupo katika mazingira ya vitu hivi haimaanishi kuwa huwezi kupata tatizo la kipanda uso, miongoni mwa vitu hivyo ni kama vile: sauti kali au kelele, harufu kali, aleji, mwanga mkali, kuvuta sigara, matatizo ya kukosa usingizi, kukaa bila kula kwa muda mrefu, pombe, kubadilika badilika kwa siku za mwanamke (menstrual cycle fluctuations).
Inawezekana ukawa na tatizo hili la kipanda uso, miongoni mwa vitu vinavyowasaidia watu wenye kipanda uso ni kutumia dawa mbalimbali ukijumuisha dawa za maumivu zenye mchanganyiko na caffeine, pia utumiaji wa chai au kahawa umesaidia baadhi ya watu kuwapa nafuu ya maumivu makali ya kichwa.
Tunaweza kupunguza hatari (risk) ya kupata kipanda uso kwa kubadilisha staili ya maisha yetu ya kila siku, kuepuka vitu vyenye harufu kali, kuepuka utumiaji wa tumbaku (sigara), kupata muda wa kutosha kuupumzisha mwili (kulala), kufanya mazoezi, kutokaa bila kula kwa muda mrefu, kunywa maji ya kutosha.Je, unalo tatizo la kipanda uso (Migraine), dalili zako ni zipi na ni vitu gani ukitumia unapata nafuu?
KUUMWA NA KICHWA / KIPANDAUSOMaumivu ya kawaida ya kichwa huweza kutulizwa na dawa za kuzuia maumivu za aina ya Panadol au aspirini.Iwapo unahisi hayo maumivu kwenye kipji cha uso wako, mashavuni na sehemu zilizo karibu na macho zikifura, kuna uwezekano kuwa umeambukizwa sehemu za kukaza pumzi puani.Iwapo utashikwa na maumivu makali ya kichwa ambayo hayapoi, haikosi kuna uwezekano kuwa umeanza kushikwa na ule ugonjwa sugu wa kipandauso.
Kipandauso (migraine) kina maumivu zaidi kuliko kuumwa kichwa kwa kawaida.Kipandauso huathiri upande mmoja wa kichwa na kuleta kisunzi,au kutaka kutapika.Iwapo unahisi kipandauso unaweza kuona vimulimuli kutokana na muangaza.Pia unaweza kuhisi maumivu makali kwenye jicho moja mara kwa mara.
Ukipatwa na kipandauso, muone daktari wako akuchunguze ili akupe ushauri .Unapopatwa na kipandauso lala chini palipo na utulivu katika chumba kilicho giza kuzuia miale ya jua yanayosababisha kichwa kiume zaidi.
Jaribu usinywe kakao, pombe ama kinywaji chochote kilicho na kakao.Hivi vinaweza kusababisha kipandauso, kunywa maji mengi kila siku.
Utahitajika kumuona daktari ikiwa:
Utahitajika kwenda kwa chumba cha dharura ikiwa:
- Unaumwa na kichwa na hakipoi kwa muda wa juma moja ingawa umemeza dawa za kuzuia maumivu.
- Una matatizo unapozungumza, au unasikia kizunguzungu, miguu haina nguvu. Kuna uwezekano kwamba umeanza kupatwa na ugonjwa wa pigo.
MAUMIVU YA KICHWA HUSABABISHWA NA AINA YA MAISHA TUNAYOISHI NA KUFANYA KAZI KILA SIKU
Jaribu kuepukana na mambo yafuatayo:
1. Msongo wa mawazo
2. Matumizi ya kompyuta kwa muda mrefu.
3. Kufanya kazi ktk mazingira ya kelele nyingi.
4. Kutumia vilevi vikali
Pendelea:
1. Kupata muda wa kutosha kupumzika/kulala
2. Kunywa maji mengi ya kutosha.
3. Kunywa juice ya zabibu zilizoiva vizuri.
AINA KUMI NA MBILI ZA KUUMWA NA KICHWA
Kuumwa na kichwa kumegawanyika sehemu kuu nyingi sana japo kuwa 1% yake ni hashirio la matatizo ya kiafya ambayo yameadvance. Kama vile concussion of brain,meningitis,encephaliti, na stroke. Kuumwa na kichwa pia inawezatokana na matatizo ya taya, meno au hata kula vitu vya baridi zaidi. Vyakula vyenye nitrite au monosodium glutamate.
Sehemu ambazo huuma ni kama ifuatavyo.mfumo wa fahamu ambao upo kwenye fuvu la kichwa.
Baadhi ya neva za fahamu zizlizoko usoni
Misuli ya kichwani
Mishipa inayopatikana kwenye fuvu la kichwana chini ya ubongo kuna mifumo ya fahamu yenye hisia. Kumbuka fuvu na tishuu za ubongo kwa zenyewe haziumi kwani hazna mifumo ya fahamu ambayo inahisia.
Mambo haya 12 nayo yanahusika sana.
1: Nervous tension headaches;
Ni maumivu ya kichwa endelevu upande mmoja au pande zote za misuli ya shingo na upande wa juu wa mgongo,kuumwa na kichwa pamoja na kusinzia. Tumia vitamin b2 na c , ounguza au acha matumizi ya sukari,kahawa,chakula chenye kukusababishia mzio,misongo ya mawazo na ufanye mazoezi yakutosha.
2: Cluster headaches;
Kichwa kuuma haswa upande mmoja wa kichwa kwa maumivu makali, machozi humtoka mtu na makamasi kwa mbali. Kitu cha kwanza ni kutumia chakula chenye protein ya kutosha, epukana na chakula chenye mzio kwako.
3: Hangover headaches;
Hii ni hali ya kichwa kuuma kwa sababu ya matumizi makubwa ya vinywaji vikali haswa pombe. Weka barafu chini ya kichwa yaani maeneo ya kichogoni au shingoni,kunywa maji mengi na juice ya matunda freshi na uache pombe.
4: Exertion headaches;
Hutokea pale ambapo mwili utatumika sana na haswa kwenye ngono. Weka barafu linalouma, kula mlo kamili na usifanye mazoezi.
5: Caffein headaches;
Hali hii hutokea pale ambapo umeacha matumizi makubwa sana ya kahawa kwa ghafla. Kunywa kiasi kidogo cha kahawa kuondoa maumivu na upunguze matumizi kidogokodogo mpaka utakapo acha kabisa.
6: Sinus headaches;
Maumivu haya huanzia upande wa kulia na kushoto wa pua na kupanda mpaka kichwani. Kula vitamini C kwa wingi na umuone mtaalamu wa afya maana saa zingine hii utkana na maambukizi.
7: Bilious headaches;
Kichwa na macho huuma haswa kipanda uso na husababishwa na kula sana, kula vibaya, kutofanya mazoezi na kukosa choo. Fanya mazoezi na kunywa maji yakutosha na kasha fanya enema.
8: Hunger headaches;
Maumivu ya kichwa ambaya husababishwa na kutokula kwa muda. Kula chochote ilimradi kiwe ni protein au carbohydrates .
9: Eyes ram headaches
Haya ni maumivu yanayotokea kwenye macho na wengi hudhani labda wameangalia vibaya japo saa zingine inaweza kuwa sababu. lakini chanzo chake haswa ni ubongo kufanya kazi kupita kiasi. Badili mtindo wa maisha na kama ni mtumiaji wa miwani ni vyema ukamuana mtaalamu aangalie kama lensi zimepotea nuru au la.
10: Menstrual headaches;
Hali hii hutokea kwa kina mama kipindi cha yai kupevuka. Hutokana na mabadiliko ya hormone, muone mtaalamu wa afya.
11: Arthritis headaches;
Haya ni maumivu ya kichwa yanayosikika mpaka shingoni na saa zingine mpaka mgongoni ambayo husababisha maumivu haswa unapozidisha mwendo au shughuli. Kitu kikubwa ni kutibu ugonjwa unaosababisha hali hiyo.
12: Hypertension headaches;
Ni maumivu ya kichwa chote, mwendo mkubwa pia huongeza maumivu. Hali hii husababishwa na shinikizo la damu. Tibu au pambana kushusha shinikizo la damu na halii itaisha bila shaka.
Ushauri wangu nenda hospitali kapime damu unayo damu ya kutosha? Nenda kapime macho? Je unapata Usingizi wa kutosha? Je unatapa choo laini kwa wiki unakwenda haja kubw amara ngapi? Je uanyo mawazo au Stress? Kapime Mapigo ya Moyo wako (High blood Pressure ) Yanakwenda sawa? Kisha uje hapa unipe majibu yako.@DANIEL MWITA
Dawa ya Maradhi ya Kichwa Fanya hivi: Fikicha (Sugua) Tangawizi kwa maji na weka kwenye paji la uso. pia hii ni dawa kwa maumivu ya jino na maumivu ya sikio kwa maumivu ya sikio dondoshea tone moja kwenye sikio.
Ukiwa na Swali au Tatizo lolote linalokukera usikose kunitafuta kwa kubonyeza hapa.Mawasiliano
KIPANDA USO (MIGRAINE) NI DALILI YA UGONJWA WA KIHARUSI
Kwa ufupi
Zipo sababu za ugonjwa huu. Wagonjwa tofauti wanaweza kuhisi moja ya kati ya nyingi zilizopo. Unaweza kutokana na kufinywa au kupungua kwa upenyo wa mishipa ya damu inayopeleka damu sehemu ya mbele ya ukuta wa jicho au au mabadiliko kwenye mshipa wa fahamu wa jicho (optic nerve).
By Dk Isaack Maro
Kipanda uso cha macho ni maradhi yanayosababisha maumivu ya kichwa yakiambatana na matatizo ya macho. Maumivu haya huweza kutokea bila dalili zilizozoeleka za kipanda uso na mara nyingi husababisha kuona kwa shida au kutoona kabisa kwa kipindi kinachozidi saa moja.
Zipo sababu za ugonjwa huu. Wagonjwa tofauti wanaweza kuhisi moja ya kati ya nyingi zilizopo. Unaweza kutokana na kufinywa au kupungua kwa upenyo wa mishipa ya damu inayopeleka damu sehemu ya mbele ya ukuta wa jicho au au mabadiliko kwenye mshipa wa fahamu wa jicho (optic nerve).
Yaweza pia kutokana na maradhi yanayohusisha mfumo wa damu kama vile seli mundu au mwanga mkali unaomulika ghafla machoni. Pengine ikawa harufu kali ya marashi au sauti kubwa.
Msongo wa mawazo, wasiwasi na unywaji wa pombe kupita kiasi ni sababu nyingine. Hata unywaji wa kiasi kikubwa cha kahawa nayo husababisha bila kusahau mabadiliko ya hali ya hewa.
Ugonjwa huu unaweza kumpata yeyote lakini wenye historia ya kuugua wapo kwenye hatari zaidi. Tafiti za kisayansi zinaonyesha maradhi haya hurithiwa. Hii ina maana familia ambazo zina historia ya watu waliowahi kupata maradhi haya huwa kwenye hatari zaidi.
Kipanda uso cha macho kina uhusiano na homoni ya kike inaiitwayo Oestrogen hivyo kumaanisha huonekana zaidi kwa wanawake kuliko wanaume. Siyo tu huonekana zaidi kwa wanawake bali kwenye vipindi fulani kutokana na kuongezeka au kupungua kwa homoni hizo, mfano kipindi cha hedhi.
Kipanda uso cha macho huwa na dalili zinazofanana na kipandauso cha kawaida kama vile kichwa kuuma, kupata kizunguzungu, kusikia kichefu chefu na mara nyingine kutapika.
Ingawa dalili nilizotaja hapo juu huwa zinaonekana kabla au wakati wa maumivu makali ya kipanda uso si mara zote hutokea kwenye kipanda uso cha macho.
Kuumwa kichwa unapotazama mwanga mkali au kusikia sauti ya juu ni dalili nyingine ya ugonjwa huu. Lakini dalili kubwa ya kipanda uso cha macho ni kuona taswira ya vitu kama nyota au mwanga mkali wa mistari mistari.
Wengine huona giza muda mfupi kabla tatizo kutokea. Dalili ya kuona mwanga mkali wenye nyota nyingi ni dalili inayoripotiwa na wagonjwa wengi zaidi. Hali hii hudumu kwa kipindi kifupi kisichozidi dakika sitini au saa moja.
Tafiti zinabainisha dalili za maradhi haya mara nyingi hufanana na za maradhi mengine hivyo mgonjwa anatakuwa amuone daktari ili vipimo vitakavyothibitisha.
Historia ya maradhi na vipimo vikionyesha kuwa kweli tatizo la mgonjwa ni kipanda uso cha macho basi atapewa dawa za kutuliza maumivu ya kichwa na kuzuia kuongezeka kwa shinikizo la damu kwenye macho.
Yapo madhara ya kipanda uso cha macho ambacho mara nyingi husababisha maumivu makali ynayaomfanya mgonjwa kushindwa kufanya shughuli zake za kawaida ingawa huwa haudumu kwa muda mrefu.
Mara nyingi kipanda uso cha macho huwa ni ishara ya maradhi mengine makubwa na yenye matokeo mabaya zaidi. Ugonjwa huu unaweza kuambatana na majeraha au uvimbe kwenye ubongo.
Pengine waweza kuwa dalili ya kiharusi au kutanuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo (aneurysm) kama siyo maradhi ya mishipa ya damu inayosambaza damu kwenye ubongo.
Yaweza kuwa ishara ya maumivu ya mishipa ya fahamu au kichwa kikubwa (hydrocephalus) hasa kwa watoto. Wakati mwingine humaanisha upungufu katika maumbile ya fuvu la kichwa.
Chanzo: Kipanda uso ni dalili ya ugonjwa wa kiharusi
THEORIES ZINAZOELEZEA JINSI TATIZO HILI LINATOKEAKuna theories nyingi zinazoelezea pathophysiology (mechanism) ya jinsi tatizo hili linatokea,lakini hakuna hata moja iliyokubalika universally. Lakini pia hakuna dawa hata moja iliyothibitika kutibu/kumaliza tatizo hili universally. Ila kuna vitu kadhaa vinavyokubalika universally juu ya ugongwa huu.
1. Watalamu wote wanakubaliana kwamba hakuna uhakika wa nini hasa kinasababisha ugonjwa huu (kuna theory nyingi).
2 .Walamu wote wanakubaliana kwamba hakuna dawa ya uhakika inayotibu/inayomaliza tatizo hili kwa wagonjwa wote.
3. Watalamu wote wanaclassify type 2 za migraine headache: Typical na Atypical-Typical migraine ina classical signs & symptoms ("Zigzag silvery" vision dakika kadhaa kabla ya kichwa kuanza kuuma, unilateral headache yaani kichwa kinauma upande mmoja wa uso, kichefuchefu na mdomo kujaa mate au kutapika kabisa, photophobia yaani mgojwa hapendi kuona mwanga, kichwa kuuma kwa masaa hadi siku kadhaa kisha maumivu yanapotea kabisa) Kwa upande wa Atypical migraine, dalili hizo nilizotaja sio lazima zionekane zote kwa wakati mmoja.
4. Watalamu wanakubaliana kuwa kichwa kikishaanza kuuma hakuna dawa yoyote ya kumeza ya maumivu inayofanya kazi vizuri. Hii ni kutokana na kwamba kunakuwa na slow down ya gut movement na decreased absorption tumboni (stomach & intestines). Dawa utameza lakini haitafanya kazi vizuri kama inavyotegemewa.
5. Watalamu wanakubaliana kuwa kupona kwa maumivu hakutegemei dawa, kwa maana kwamba hata usipotumia dawa muda ukifika maumivu yanaondoka yenyewe.
6. Kuna utafiti umeonesha kwamba kadiri umri unavyozidi kwenda,frequency ya attacks inapungua! Pia wengine wanasema hata intensity ya maumivu hupungua,ingawa hii haijakubalika sana.
7. Hakuna data wala ushahidi unaoonesha kuwa migraine inaweza kupelekea mtu kupata uchizi, wala kifafa,wala kifo! Isipokuwa kuna taarifa za kuwepo idadi ndogo sana ya wagonjwa waliopata matatizo ya kuona ingawa bado haijathibitika kama ni kwa sababu ya migraine.
8. Pia takwimu zinaonesha kuwa,ungonjwa huu unaanza kuonekana baada ya kipindi cha utoto kupita.Mara nyingi watu huanza kuupata ukubwani, na inaonekana wanawake wanaathirika kwa wingi kuliko wanaume kiuwiano.
9. Pamoja na kwamba ugonjwa huu unaanza kuonekana zaidi ukubwani,lakini watalamu wanasema huu ni ugonjwa wa kurithi.Kwa hiyo ndugu yangu kama ndio hivyo, inawezekana tatizo hili lipo kwenye familia yenu! Mimi kwetu upo!
10. Watalamu pia wanasema kwa kuwa hakuna uhakika hasa ni nini sababu ya tatizo hili, wanasema, upo uwezekano wa tatizo hili kupotea bila tiba yoyote ya maana. Hapa ndipo kidogo kuna ukakasi, maana wapo watu wameombewa wakapona, wapo waliotumia dawa za wamasai wakapona nk, nk, nk. sasa huko siwezi kwenda zaidi!
Kwa nini nimetoa mchango wangu hapa? Mimi pia ni mhanga wa tatizo hili tangu nikiwa na umri wa miaka 14. Binafsi mimi ni mwanachuo ktk chuo kikuu fulani cha udaktari hapa nchini. Na kiukweli, kwa jinsi ugonjwa huu ulivyonitesa, naweza kusema, ndicho kichocheo kikubwa kilichonifanya nisome kozi hii.
Kwa sasa frequency imepungua sana;mwanzo nilikuwa napata attacks hata mara mbili hadi tatu kwa wiki,ila siku hizi ninaweza kukaa hadi miezi minne sijapata attack kabisa. Hata intensity nahisi imepungua tofauti na mwanzo;ingawa inawezekana labda ni kwa sababu nimeishazoea. Usually mimi maumivu huwa masaa 2-3 baada ya hapo nakuwa mzima kabisa na ninaendelea na shuguli zangu as usual.
But all in all maumivu ni makali jamani, asikwambie mtu. Every shughuli is shut down; huwezi kufanya chochote.
Nise tu pole kwenu ndugu yangu, maana na mimi naufahamu muziki huo!