Dawa ya Fungus

Caroline Danzi

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
3,713
1,263
Wana JF,

Natumai hamjambo wote kwa mpigo.

Nikiwa mmoja wa watu waliowahi kuchangia thread kuhusu dawa ya Fungus. Nina ndugu yangu alikuwa na fungus wa kutisha miguu imeliiwa kama vile amebabuliwa na moto. Amekaa wiki mbili bila kwenda kazini hawezi kuvaa hata kandamibili anavaa yebo yebo tu.

Katika pita pita zangu nikapita pale kariakoo kwa wamasai. Nikawauliza kama wana dawa yoyote ya kutibia fungus? wakaniambia wanayo, sikutaka kuuliza kwa sababu nilishajaribu dawa zote zimeshindwa kazi.

Nikachukua maelekezo mazuri nikaenda kwa ndugu yangu kuanza kutumia dawa. Hivi ninapoandika jamaa yangu kapona na kazi ameanza jana. Dawa imetumika for only 4 days tu. Leo kavaa moka zake za kikongo na soksi kuelekea kazini.

Kwa wale wote wenye fungus, nawatumia hii namba mkajaribu inawezekana ikakuponyesha. Simon 0714 884542 (ni mmasai). Ukipiga ongea shida yako akuelekeze alipo ukachukue. Usiulize jina langu hanijui na mimi pia simkumbuki.

Siku njema.

CD
 
umenena carolyne...... ngoja nikirudi dsm nitamsaka huyu maana anko angu alikuwa na tatizo hili.
 
Back
Top Bottom