Dawa ya Babu inawezekana kuwa katika mfumo wa vidonge -WHO

RGforever

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
6,878
5,424
UTAFITI unaoendelea kufanyika
wa dawa ya Mchungaji Ambilikile
Mwasapile wa kijiji cha Samunge
umebainika kuwa dawa inatibu
maradhi sugu na Shirika la Afya
Duniani [who] Kuikubali dawa hiyo


Hayo yamebainishwa na Askofu
wa Kanisa la KKKT na kubainisha
kuwa shirika hilo limekubali kuwa
dawa hiyo inatibu maradhi sugu
kama ilivyobainishwa awali katika
utafiti wa kina walioufanya.


Imesemekana kuwa dawa hiyo
inawezekana kuwa katika mfumo
wa vidonge na chupa.


Shirika la Afya Duniani WHO
ambalo lilituma wataalamu wake
kuichunguza dawa ya babu,
limebainisha hilo na kulifanyia kazi
mikakati hiyo ya kuweka dawa
hiyo katika mifumo hiyo na si
kikombe pekee kama
ilivyozoeleka, alisema Askofu
huyo.

Pia dawa hiyo imethibitishwa na
taasisi ya TMF na kubainisha kuwa
dawa hiyo inatibu maradhi sugu.


Hayo yalisemwa jana na
Mwenyekiti wa TMF, Marwa
Gonzaga jijini Dar es Salaam.
Alisema wakati wakiendelea na
utafiti huo walibaini kuwa tiba hiyo
ni mchanganyiko wa mizizi ya miti
shamba ya aina mbili ambayo ni
kisayansi unafahamika kama
Carissa Spinarum na mti wa
Ntuntwa.

Tayari dawa ya babu imeshajizolea
sifa ndani na nje ya nchi ambapo
watu wameendelea kumiminika
kijijini hapo kunywa dawa hiyo.


Hata hivyo taarifa zilizopatikana
baadae zimesema kuwa babu
amekataa dawa yake kufanyiwa
mabadiliko yoyote kwakuwa
Mungu hapendi.

Babu alisema kuwa kwakuwa
dawa hiyo ni ya miujiza alioteshwa
na Mungu, masharti aliyopewa na
mungu kwenye ndoto yake
hayaruhusu dawa hiyo ifanyiwe
mabadiliko yoyote yale. Labda
kama ataoteshwa ndoto nyingine
ya kupewa ruhusa kufanya hivyo.
 
Taribu mkuu na hizi habari za radio mbao! WHO huwa wanatangaza habari za utafiti wao kwa Dunia nzima bila kupitia kwa mtu binafsi au Taasisi yoyote.
 
Na hayo masharti kwamba lazima itolewe na mchungaji mwenyewe yatawekwaje kwenye vidonge?
 
Sawa wampe hati miliki ya hiyo dawa ili babu ale shavu hadi vilembwe vyake
 
Inatakiwa nguvu ya ziada kumshawishi babu ili akubali kama wataalamu wanavyoshauri. Kama wapo ndugu zake na babu humu tunaomba wamwombe akubali!!!!
 
tuombe Mungu dawa ya babu itibu kweli hayo maradhi. tunaihitaji sana. ila WHO hawahitaji msemaji toka KKKT au kwingineko. na nadhani kwa tafiti zao ni mapema sana kuitolea conclusions. anyway tuendelee kuomba Mungu tusaidiwe, manake wagonjwa ni sisi wenyewe
 
Back
Top Bottom