Dawa ya asili ya ugonjwa wa moyo

Kasuku Mdogo

Member
Jun 2, 2016
14
23
Ugonjwa wa moyo unajumuisha matatizo ambayo yanaathiri muundo na kazi za moyo. Ugonjwa wa moyo mara nyingi huhusishwa na kujibana au kukazika kwa mishipa ya damu, au mkusanyiko wa taka katika kuta za mishipa ya damu ambako hupelekea kupungua kipenyo cha mishipa ya damu na hivyo kuzuia mzunguko ulio huru wa damu, na hatimaye kukupa hatari ya kupata shambulio la moyo na stroke.

Ugonjwa wa moyo unahushisha matatizo kama matatizo ya mishipa ya moyo, matatizo ya kurithi ya moyo, mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida, moyo kufeli kufanya kazi, matatizo ya valve za moyo, moyo mpana au mkubwa na matatizo mengine mengi katika moyo.

Chanzo na dalili za ugonjwa wa moyo hutofautiana mtu mmoja hadi mwingine kutegemea na ania ya ugonjwa wa moyo. Baadhai ya dalili za kawaida ni pamoja na pumzi fupi, maumivu ya kifua, mapigo ya chini ya moyo, kichwa kizito, utovu na udhaifu wa mwili kwa ujumla.

Vitu vingine vinavyo weza kuongeza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo ni pamoja na :

1) Shinikizo la juu la damu

2) Kolesto

3) Kisukari

4) Uzito kupita kiasi

5) Uvutaji sigara

6) Unywaji pombe kupita kiasi

7) Matumizi yaliyozidi ya kaffeina

8) Utumiaji wa madawa ya kulevya

9) Uzee

10) Kurithi

11) Mfadhaiko wa akili

Wakati unataka kujitibu ugonjwa wa moyo ni muhimu kutofanya lolote wewe mwenyewe peke yako bila ushauri au uangalizi wa karibu wa daktari au muuguzi wako. Unaweza pia kutumia baadhi ya dawa za asili na kubadili namna unavyoishi ili kuimarisha afya ya moyo wako.

Baadhi ya hizi dawa za asili zinaweza zisipatane na baadhi ya dawa za hospitalini kama upo uantumia dozi ya ugonjwa fulani wakati huu. Kwa hivyo, pata ushauri kwanza toka kwa mtaalamu wa afya aliye karibu na unayemwamini kabla hujaamua kutumia baadhi ya hizi dawa.

1. Mafuta ya Habbat soda

Moyo usio na afya unaweza kuwa ni matokeo ya sababu nyingi sana lakini chanzo kikuu cha sababu zote hizo ni kimoja, nacho ni kutokuupa moyo vurutubishi muhimu unavyovihitaji kila siku ili ubaki na afya.

Mafuta ya asili ya Habbat Soda yana kiililishe muhimu sana kwa afya ya moyo ambacho ni asidi amini Mmega 6 na 9 na kiilishe kingine kijulikanacho kwa kitaalamu kama ‘ Phytosterols’. Viinilishe hivi muhimu husaidia kuzuia mishipa kujikaza na hivyo kuwa msaada mkubwa hata kwa ugonjwa wa shinikizo la juu la damu. Biinilishe hivi kwenye mafuta asili ya habbat soda husaidia kushusha kolesto na sukari katika damu pia.

Kwa karne nyingi mafuta ya asili ya habbat soda yamekuwa yakitumika kutibu ugonjwa moyo.

Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chakula cha mafuta gaya kutwa mara 2 kwa majuma hata miezi kadhaa. Unaweza kuchaganya mafuta haya kwenye glasi moja ya juisi yoyote uliyotengeneza nyumbani ili kuupata radha.

2. Kitunguu saumu

Tafiti kadhaa zimeonyesha kitunguu saumu kuna na ufanisi mkubwa sana katika kutibu magonjwa kama shinikizo la juu la damu, Kolesteroli na magonjwa ya mishipa ya moyo. Kitunguu saumu huzuia kujikaza au kuzibika kwa mishipa ya damu. Kitunguu saumu pia huongeza msukumo wa damu. Ili kujitibu au kujizuia usipate ugonjwa wa moyo kwa kitunguu saumu fanya hivi.

Kula punje moja au mbili za kitunguu saumu kila siku. Ikiwa inakutokea radha yake au harafu yake inakuwa kali sana unaweza kunywa glasi moja ya maziwa freshi baada ya kuwa umekula hizo punje za kitunguu saumu.

Muhimu: Kitunguu saumu kinaweza kisipatane na ania nyingi ya dawa hospitalini sababu ya baadhi ya dawa hizo hukaza mishipa ya damu. Wasiliana na daktari wako kabla ya kuanza kutumia hii dawa.

3. Bizari (manjaro)

Tafiti zinaonyesha kwamba bizari inao uwezo wa kuzuia mishipa ya damu kujikaza. Bizari inayo kirutubishi muhimu sana kijulikanacho kwa kitaalamu kama ‘curcumin’ ambacho husaidia kutunza afya ya moyo kwa kuzipunguza taka taka za kolesto, takataka nyingine zozote kwenye mishipa ya damu na kuzuia kuganda kwa damu kwa ujumla.

Bizari pia inasaidia kushusha msongamano wa chini wa lipoprotini lolesto (LDL) na kuzuia uundwaji wa uvimbe. Inao uwezo mkubwa pia wa kuondoa sumu mwilini na hivyo kuzuia kujijenga kwa vijidudu nyemelezi vya magonjwa (free radicals) na kama matokeo yake ya pili husaidia kutozeeka mapema na magonjwa mengine sugu.

Tumia bizari mara nyingi au kama kiungo kwenye vyakula vingi unavyopika.

Unaweza pia kuchemsha kijiko kikubwa kimoja cha chakula na maji nusu lita au na maziwa nusu lita (vikombe viwili). Kunywa kikombe kimoja asubuhi na kikombe kingine jioni siku kwa wiki kadhaa.

4. Uwatu

Uwatu una sifa kuu ya kuondoa sumu mwilini na kuulinda mfumo mzima wa upumuaji. Uwatu husaidia kupunguza uwezekano wa ateri za damu kuzibika (atherosclerosis), hurekebisha na kuweka sawa uswa wa mafuta katika damu (blood lipid).

Uwatu pia husaidia seli damu za damu kutokuumana na kukaribiana sifa ambayo ni muhimu sana katika kuzuia damu kuganda na hivyo kupunguza hatari kugandana au kushikana kwa seli za damu kusiko kwa kawaida kunakohusiana na shambulio la moyo, kushusha kolesto, sukari katika damu na mafuta yaliyozidi.

1. Loweka kijiko kidogo kimoja (kijiko cha chai) cha mbegu za uwatu kwa siku mzima.

2. Siku inayifuata kula hizo mbegu za uwatu zilizokuwa zimeloweka wakati tumbo likiwa tupu.

3. Fanya hivyo kila siku kwa miezi kadhaa.

5. Chai ya kijani(Green Tea)

Chai ya kijani maarufu kama ‘Green Tea’ ina viondoa sumu vya muhimu sana mwilini ambavyo husaidia kuimarisha afya ya seli ainazounda sehemu ya ndani kabisa za moyo na mishipa ya damu. Husaidia kushusha kolesto na kiwango cha mafuta katika damu. Chai hii pia husaidia kudhibiti sukari katika damu (blood sugar) na kuimarisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Katika utafiti uliofanywa na Japani mwaka 2008, watafiti waligundua kuwa kunywa vikombe vitano vya chai hii ya kijani kwa siku kulisaidia kupunguzza hatari ya kupatwa na vifo vinavyotokana na ugonjwa wa moyo au stroke kwa asilimia 26.

Kunywa vikombe vinne kila siku vya chai hii ya kijani (kumbuka usiongeze ndani yake yale majani mengine meusi ya chai ili kuepuka kaffeina).

6. Mazoezi

Utanishangaa mazoezi nayo ni dawa? Ndiyo mazoezi ni dawa kwa magonjwa mengi sana mwilini tofauti na unavyodhani. Tatizo watu wengi hawajishughulishi na mazoezi labda mpaka waambiwe au washuriwe na daktari. Mazoezi ni muhimu kwa mtu yeyote uwe unaumwa au huumwi chochote.

Mazoezi ya mara kwa mara yakiambatana na kula lishe sahihi inaweza kusaidia kuzuia na kuudhibiti ugonjwa wa moyo. Mazoezi kama ya kutembea kwa miguu, kukimbia pole pole (jogging), kuendesha baiskeli na kuruka kamba ni mazoezi ya muhimu sana katika kuuongezea nguvu moyo wako na mfumo wa upumuaji, kuimarisha mzunguko wa damu na kushusha shinikizo la juu la damu.

Mazoezi husaidia pia kudhiti uzito na unene kupita kiasi wa mwili na hivyo kupunguza msongo wa mawazo (stress) vitu ambavyo vina uhusiano wa karibu kati ya ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine mengi.

Chama cha madaktari wa magonjwa ya moyo cha Marekani kinashauri kila mtu kufanya mazoezi ya walau nusu saa kila siku mara tano kwa wiki ili kuimarisha afya ya moyo na kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo. Ongea na daktari juu ya mazoezi gani yanakufaa kwa mujibu wa uzito wako.

7. Magnesimu na Potassium

Utafiti mmoja umeonyesha kuwa kutumia madini ya magnesimu kunaweza kupunguza shinikizo la juu la damu na kwamba ni madini mazuri kwa ufanyaji kazi wa jumla wa moyo.

Utafiti mwingineumeonyesha utumiaji wa potassium unasaidia kuboresha kazi za moyo vile vile husaidia kupunguza shinikizo la juu la damu kutokana na utumiaji uliozidi wa chumvi.

Unaweza kuwa umeshaambiwa kuwa utumiaji wa chumvi ya mezani (sodium chloride) ni jambo baya, lakini kwa kutumia chumvi yenye magnesium na potassium badala ya chumvi ya mezani kunaweza kusaidia sana kushusha shinikizo la juu la damu kama inavyoelezwa kwenye utafiti huu.

Mambo ya muhimu kuzingatia;

1) Punguza mafuta, kolesto na chumvi kwenye chakula chako.

2) Epuka mafuta magumu hasa yale yatokanayo na wanyama (polyunsaturated and monounsaturated fats). Mfano unaweza kutumia mafuta ya zeituni badala ya kutumia siagi, margarine na mafuta mengine yatokanayo na wanyama.

3) Acha kuvuta sigara na pungguza kunywa pombe

4) Punguza uzito, hakikisha una uzito kulingana na urefu wako.

5) Punguza mawazo na (stress) na tumia mbinu mbadala na kurelax (kupumzika)

6) Epuka ugonjwa wa kisukari

7) Pata vitu vyenye omega 3 na vitamin D

8) Pata usingizi wa kutosha kila siku

9) Fanya vipimo vya juma juu ya afya yako kila mara
 
Uzi nzuri sana huu

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom