Mzee23
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 1,696
- 3,472
PUMU NI NINI?
Ni ugonjwa unaoathiri njia ya hewa kwenda/kutoka katika mapafu.
Mtu mwenye pumu huwa na mcharuko-mwili sugu(chronic inflammation) katika mirija yake ya kupitishia hewa unaosababisha kuvimba kwa kuta za mirija ya hewa na kujaa ute kamasi hivyo kuminya njia ya hewa na kusababisha mtu kupumua kwa shida!
DALILI ZA PUMU
-Kuishiwa pumzi na kupumua kwa shida
-Kutoa sauti kama mluzi(wheezing)
-Kukohoa sana usiku/asubuhi
-Kubanwa kifua mara kwa mara
-Anayepatwa na shambulizi kubwa hushindwa kuongea na kuonesha kuchanganyikiwa
TANBIHI:
Mwenye pumu sugu siku zote huwa na njia nyembamba ya hewa na huzidi kuwa nyembamba kadiri anavyopata shambulio la pumu!
FANYA HIVI..
1. Tembelea duka la viungo/sokoni, nunua unga wa mdalasini, unga wa tangawizi na unga wa uwatu. Kisha tafuta asali mbichi. Changanya uwatu,mdalasini kwa uwiano sawa halafu miminia asali inayotosha kulainisha huo mchanganyiko vizuri, kisha changanyia unga wa tangawizi kidogo kidogo hadi uhisi ukali unaostahimili wewe wa tangawizi. kisha lamba kijiko kikubwa kutwa mara 3 kwa wiki 3.
2. pamoja na hiyo, tafuta karafuu ukishapata kila siku jioni chukua punje 6-8 toa vichwa halafu loweka ktk maji nusu kikombe, funika usiku mzima. Kesho yake asubuhi unywe maji yake tu kwa wiki 3.