hekimatele
JF-Expert Member
- May 31, 2011
- 9,884
- 2,781
Nimeona watu wametoa michango mingi sana ila kuna wale wanapotosha, eti kuna mbinu ya kupunguza kilo moja kwa siku. Huo uwongo tu, ifahamike kilo moja ni grams 1,000 hilo haliwezekani.
Binafsi mimi nilikua mnene sana kupindukia, unywaji wa pombe ulichangia pakubwa, zikiwemo hata konyagi ambazo kuna wengine wanadanganya eti inapunguza uzito kisa ina ukali. Ifahamike Konyagi kama pombe zingine ina wanga.
Kilichonisaidia mimi hadi nikawa napunguza kilo moja kwa wiki
- Nilianza kula tango, ifahamike tango ina calories kidogo zaidi ya vyakula vyote. Hivyo kabla sijaanza kula chakula, ilikua naanza na tango kadhaa, kiasi kwamba nahisi nimeshiba halafu sasa hapo nabugia msosi. Hivyo najipata nakula chakula kidogo maana tango zimejaza tayari.
- Nikapunguza wanga, ugali nakula kidogo lakini pembeni najaza vyakula visivyokua na wanga kama mamboga mboga
- Nikaacha pombe kabisa
- Nikaendelea na mazoezi, ifahamike nilikua napenda mazoezi tangu hapo awali japo sikua napunguza uzito hata nikifanya mazoezi makali kiasi gani.
Hivyo vitu vichache tu, baada ya miezi mitatu watu wakaanza kunishangaa. Halafu huna haja ya mazoezi mazito, tembea kilomita tano kwa siku basi.
Great msaada mkuu. Thanks