David Kafulila: Rais 2015 Lazima Atokee Kigoma

Status
Not open for further replies.
Mbowe alishajaribu akashindwa, Slaa naye kajaribu kashindwa. Sasa cdm mpeni nafasi Zitto naye ajaribu, huenda atawapa raha wana cdm

Raha unatakiwa upewe na unayeamini ana uwezo wa kubadilisha mambo. Kama ni Zitto, si afadhali tufanye mabadiliko ya kumwongezea muda JK? Maana siamini kama tunaweza kupata chochote kutoka kwa Zitto zaidi ya mvurugano mkubwa wa kitaifa.
 
Akina Zitto ni Wakongoman. Kama anabisha aseme hapa hapa maana ni member humu. Kujua kupauyuka hovyo hovyo haina maana umependwa na Watz. Bora mkakomboe hiyo congo yenu. Alaaaaaaah

Kwani kijana ni Zitto tuuu. Hata sie wengine ni vijana pia na sio lazima tuwe marais.

Si heri unajua kuwa Zitto ni Mkongo,tafuta kujua na wewe wa wapi isije ikawa umetoka kuzimu!
 
Mkuu,
Mimi Jembe nitaliita Jembe(Spade is a Spade) na si vinginevyo. Kama unaona nabagua Mtu au Jamii then hapo utakuwa unatumia mtazamo wako binafsi.

Nilibahatika kufa
Miminya kazi (UN) maeneo ya KIGOMA mara kadhaa. Nikapata kuwaelewa vizuri sana kitabia hawa Jamaa zetu wa KIGOMA. Kuna mtu humu aliandika vizuri kuhusu ubinafsi wa hawa jamaa wa KIGOMA.
Na statement ya Mh. Kafulila anaposema "Safari hii lazima Rais na Makamu LAZIMA WATOKE KIGOMA" imekuwa ni moja ya vigezo vinavyozidi kunipa mawazo na fikra tofauti kuhusu hawa Jamaa zetu.

Mimi simbagui mtu kwa "style" yoyote, Ila I call it as I see it. Nasema ukweli ambao WaTanzania wengi tunaogopa kuongea hadharani.
Pamoja.

Mimi siafiki ubaguzi wa namna yeyote ile lakini ni lazima niseme ukweli kuwa watu wengi niliowahi kuongea nao, wengi husema kuwa hata kama unafanya kazi ofisini, unatakiwa ufanye kazi kwa tahadhari kubwa kama unayefanya naye ni mtu wa Kigoma. Wanasema kuwa ni vigeugeu, wabinafsi na wabishi. Na wengine wanaoyasema haya ni watu wanaoheshimika sana katika jamii. Sijui kama inakuwa ni coincidence ya tabia hizo mbaya na mtu atokako lakini ndivyo wengi wanavyowaona. Na mifano mingi tu hutolewa ambayo inakushawishi unayesikiliza. Lakini kuna ukweli pia kuwa mazingira na jamii inayokuzunguka hukuumba.
 
Mtu huonekana mpuuzi pale anapolazimisha jambo, unapozungumzia mtu kugombea urais usizungumzie mahali anapotoka zungumzia uwezo wake. hoja ya Kafulila haina mashiko na nadhani hoja za namna hii ndio zinatufanya tuwaone wale wote wanaoanza mapema yote hii kujinadi bado hawana uwezo wa kuiongoza nchi hii. Rais anatakiwa watu wamuone sio ajione sasa kujinadi kote huko kunatoka wapi wakati mwisho wa siku wanachama ndio watakaoamua nani anafaa hata wapige kelele vipi. sanasana mwisho wa siku tutawaona wavurugaji. Slaa alivyochaguliwa kuwa mgombea hakukuwa na hekaheka hizi na watu wengi walikuwa bado hawajui ni nani atakuwa mgombea sasa hizi heekaheka za sasa ni za wavurugaji mtu unaejiamini na kweli unaefaa kelel zote mapema hii za nini. hizi ndio tabia za ccm ambazo hatutazikubali ndani ya Chadema tunataka kiongozi wa watu sio anayejiona anafaa, watu wanapaswa kumuona kuwa anafaa.
maneno ya kafulila jana jioni hapa dodoma

" huu mjadala watu kukana hauna maana kabisa. wote wanaokana ndio wapiga debe wakubwa. waliyasema haya wanayoyakana. ni unafiki ndio unaowasumbua na uoga. kabla ya kuondoka, wote tulikaa pale sinza na kwa pamoja wakasema wanamuunga mkono, tukafika Kigoma wakarudia maeno yale yale ya kumuunga zitto. Iweje leo wanakana? Asilimia 85% ya wabunge wanamuunga mkono zitto kugombea urais. Wana kigoma tumeonewa sana. Muda umefika kuwepo usawa katika uongozi wa hii nchi. Hatuwezi kuwa wasindikizaji siku zote, wakati uwezo tunao. Tunaungwa mkono kila kona ya nchi na hata nje ya nchi, na kama ni demokrasia 2015 rais na makamu wake lazima watokee Kigoma. Rais wa Tanzania, Afrika Kusini, ujerumani na Malaysia wote wanataka umuona rais kijana Tanzania.Vyama vyote vya siasa humu nchini wanamtaka rais kijana, Kikwete mwenyewe anamtaka atakayemrithi awe kijana"

----------------------------------
Edward Lowassa For President 2015
 
hivi vijamaa bana sijui nani anavidanganya. Yani Zitto uwe rais wa nchi hii? Kweli Tz yetu inaelekea kubaya unadhani kusimama mbele ya lango la Bunge kutafuta kura ya kumuondoa Pinda ndo urais huo. CDM chama changu fukuza mara moja hii kitu inayoitwa Zitto . Kwa sasa Zitto huna mvuto tena sasaivi ni Mnyika,Lissu na Msigwa bila kumsahau kamanda Lema. Mgombea pekee kwa CDM ni Dr. SLaa period
 
Binafsi najilazimisha kuamini kwamba ni kweli Mh. Kafulila ameweza kusema maneno hayo, ni maneno ambayo sikuyategemea kuyasikia kutoka kwa mwananchi wa Tanzania mwenye akili timamu, kwani yanakinzana na vigezo rahisi kabisa vya sifa za mtu kuwa Rais, Mh. Kafulila anataka tumchague Mh. Zitto Kabwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vigezo vifuatavyo: ​
  1. Asilimia 85% ya wabunge wanamuunga mkono Zitto kugombea urais. (Bunge ambalo haliwezi hata kuisimamia serikali leo hii linataka kutupendekezea Rais....??? Bunge la Ovyo...!! Bunge la kupiga usingizi, Bunge la kudai nyongeza ya posho tu.., Bunge la kuitikia "Ndiooo" hata kwa hoja muhimu zinazogusa maslahi ya Watanzania ndio linalotaka kutupendekezea Rais leo hii Watanzania...???, nani anataka hata kulisikia Bunge hili la hovyo ...???!!!)
  2. Wana kigoma tumeonewa sana. Muda umefika kuwepo usawa katika uongozi wa hii nchi. Hatuwezi kuwa wasindikizaji siku zote, wakati uwezo tunao. Tunaungwa mkono kila kona ya nchi na hata nje ya nchi, na kama ni demokrasia 2015 rais na makamu wake lazima watokee Kigoma. (Sikuwahi kutegemea hata siku moja kwamba nafasi za juu kabisa za uongozi wa nchi zinaweza kufanywa za kupokezana kwa mkoa kwa mkoa au kabila kwa kabila, Mh. Kafulila na Mh. Zitto wanataka kutupeleka wapi..??, wanataka kutupeleka kwenye vita vya ukabila tena..??? mbona wana mawazo ya hatari na ya kipumbavu namna hii...??)
  3. Rais wa Tanzania, Afrika Kusini, ujerumani na Malaysia wote wanataka umuona rais kijana Tanzania. (Upumbavu mwingine wa Mh. Kafulila anatumia vigezo muflisi kuhalalisha utumbo wake, sisi hatuchaguliwi Rais wa nchi yetu na Afrika Kusini,Ujerumani au Malaysia, kama wao wanashida ya kuona kwenye Televisheni Rais kijana si nchi zao zinafanyaga uchaguzi, basi wachague Rais kijana kwenye chaguzi zao, Kafulila asitumie mawazo muflisi kufanikisha tamaa zake za madaraka, mjinga sana Kafulila...!!)
  4. Vyama vyote vya siasa humu nchini wanamtaka rais kijana (Hapa sitaki ku-comment sababu nina hasira sana ..)
  5. Kikwete mwenyewe anamtaka atakayemrithi awe kijana (nafikiri kwa mawazo ya Watanzania wengi wameshapoteza imani na uongozi wa Rais JK, kuwaambia Watanzania kwamba Rais Kikwete anamtaka atakayemrithi awe kijana ni sawa na kumwambia mtu mwenye akili timamu asikilize ushauri wa mwendawazimu, hakuna mwenye imani tena si na Rais Kikwete, si na serikali yake wala si na Chama anachokiongoza cha Mapinduzi (CCM))
NB: Mwisho nalazimika kusema kwamba Mh. Kafulila unatumika na Chama Tawala (CCM) ili kuleta mgongano ndani ya CHADEMA na kuzorotesha nguvu za upinzani (CDM) katika kuelekea uchaguzi mkuu wa 2012, naelewa kwamba kwenye siasa kuna mchezo mchafu na kulipa fadhila lakini zisikufanye ukawa mjinga kupita kiasi mpaka ukashindwa hata kutumia akili kidogo uliyonayo kufikiri vitu vya msingi.
 
I like this somuch na shangaa watanzania wa leo wanaogopa kusikia mtu anawekania ya kuwa rais he he hebu tazama kenya wangapi mpaka sasa wamesha tangaza nia zao.

tusiwe watu wa kulalamika let them do tutapima uwezo wao na tutampatia anayefaa zaidi so zitto is not a sin do what u want brother hatutaki siasa za kiimla na hapa ndio nitajua kama chama hiki ni cha kidemokrasia au maneno tu.
 
mimi naona watanzania wengi hasa viongozi wasiasa wamelewa madaraka. kuna haja ya kupunguza marupurupu ili kuondoa usongo wa watu kukimbilia siasa. imefikia wakati watanzania kujali kazi za kitaalamu !
 
Watu wa kigoma hakuna kitu kabisa ni kujisifia tu na majigambo mpaka wasanii wao kuisifia kigoma kila siku lakini ukifika kigoma yenyewe huwezi amini. Eti tumeonewa sana hakuna kwa kutunza wakimbizi au, zitto mwenyewe haeleweki tutajuta kama sasa hawa wanaoanza kutafuta urais mapema si wazuri kabisa, mpeni uraisi wa kigoma sio tanzania.
 
maneno ya kafulila jana jioni hapa dodoma

" huu mjadala watu kukana hauna maana kabisa. wote wanaokana ndio wapiga debe wakubwa. waliyasema haya wanayoyakana. ni unafiki ndio unaowasumbua na uoga. kabla ya kuondoka, wote tulikaa pale sinza na kwa pamoja wakasema wanamuunga mkono, tukafika Kigoma wakarudia maeno yale yale ya kumuunga zitto. Iweje leo wanakana? Asilimia 85% ya wabunge wanamuunga mkono zitto kugombea urais. Wana kigoma tumeonewa sana. Muda umefika kuwepo usawa katika uongozi wa hii nchi. Hatuwezi kuwa wasindikizaji siku zote, wakati uwezo tunao. Tunaungwa mkono kila kona ya nchi na hata nje ya nchi, na kama ni demokrasia 2015 rais na makamu wake lazima watokee Kigoma. Rais wa Tanzania, Afrika Kusini, ujerumani na Malaysia wote wanataka umuona rais kijana Tanzania.Vyama vyote vya siasa humu nchini wanamtaka rais kijana, Kikwete mwenyewe anamtaka atakayemrithi awe kijana"

----------------------------------
Edward Lowassa For President 2015

Hii inasababisha niandike yafuatayo:

1. Kama Mdee na Nassari walisema hayo yanayodaiwa na Zitto na baadaye kuyakanusha basi wataumbuka, ila Zitto ajue kuwa kuanzia sasa wamemjua yuko vp, watakuwa adui zake kimtindo. Hawatamuunga mkono tena kwenye mambo yake, hata ya kijamii. Hata akina Ester na Deo watashtukia mialiko mingine ya 'Mwasiti'.
Na hata leo wakiibuka Mdee, Nassari, Ester B, Deo Filiku na kupaza sauti kuhusu urais, so what? WaTz watachagua wenyewe, si kuchaguliwa na wabunge hao au wengine wowote.

2. Hiyo 85% ya wabunge kumuunga mkono Zitto kugombea urais haiwezi kuaminika. Kwa uzoefu tu wale wa CCM watamuunga mkono wa kwao, hao tayari ni zaidi ya nusu ya wabunge. Sasa hiyo 85% imetokea wapi? Mapishi...
Na wabunge hao si ndio waliopitisha Sheria kandamizi ya kukataa kutoa michango ya wafanyakazi kwenye mashirika ya hifadhi (PPF, GEPF, NSSF, LAPF etc) hadi eti wafikie umri wa kustaafu hata ukiacha au kufukuzwa ukiwa na miaka 25, 30 etc? Tatizo la mashirika haya ni kutoa pesa za michango ya wafanyakazi kwa serikali kugharamia miradi yake ya kisiasa. Hawafai.

3. Tanzania imetoa marais kutoka mikoa minne tu (Mara, Mjini Magharibi, Mtwara & Pwani) kati ya mikoa 30 iliyopo, hivyo mikoa 26 haijatoa Rais. Kwangu hii sio issue sana, ila what's so special with Kigoma?? Kwanini wao ndio eti lazima watoe Rais 2015? Tena eti pamoja na makamu wake?? Mbona Mbeya, Morogoro, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba, Lindi, Kagera, Dodoma, Tanga, Kilimanjaro, Singida, Simiyu, Arusha na mingine jumla yake 26 haijatoa rais wa jamhuri? Kafulila aache mambo ya 'umkoa'.

4. 'Rais kijana' si lazima awe Zitto. Na 'ujana' si lazima iwe ni 'a plus' kwa mgombea urais. Kuna uwezo, uadilifu, uchapakazi, uchungu na nchi n.k. Rais anaweza kuwa wa umri wowote ili mradi asiwe chini ya miaka 40 (kwa mujibu wa katiba ya sasa). 'Vijana' akina Ngeleja, Masha, Maige, Mwinyi mbona wamechemka?

5. Issue ya marais wa Tanzania (sic! ina maana Kikwete!), Afrika Kusini, Ujerumani na Malaysia kusema kuwa wanamtaka rais kijana Tanzania haina maana kwani wapiga kura wa Tanzania hawatafuata matakwa ya hao watu wanne. Inatakiwa chaguo la Watanzania kupitia kwenye kura.
Kama aliyezungumza ni kafulila basi kachemka kwani Malaysia haina rais bali ina mfalme na waziri mkuu mtendaji (mwenye madaraka, si kama wa Tz). Hawa ndio walitaka kutuuzia 'mvua ya Lowassa'.
Mbona Afrika Kusini haohao wanachagua wazee? Mandela, Mbeki, Zuma na kuwatosa vijana wasio na subira/ wenye papara akina Malema?

NOTE:
Watanzania tukumbuke kuwa wakati huu ni wa mapambano ya kuikomboa nchi yetu kutokana na udhalimu na ufisadi unaoendelea kuitafuna nchi yetu. Mambo ni mengi yanayohitaji nguvu ya umma kuyabadilisha kama hili jipya la sheria kandamizi ya Mashirika ya hifadhi kung'ang'ania michango yetu hadi tufikie umri wa kustaafu.

Hivyo kama Serikali hii haitaki kusikiliza wananchi basi wana haki ya kubadilisha uongozi. Hatuhitaji malumbano hasa ndani ya Chama kinachoonekana kama kinaleta matumaini ya kushirikiana na wananchi kuikomboa nchi yao.

Watanzania hawatamsamehe yeyote yule ambaye anatumika au atatumika kuvuruga harakati za ukombozi hasa kwa kujaribu kivuruga chama ambacho kimeleta matumaini kwa watanzania.

Aluta Continua...
 
Kama sikosei mwaka jana Zitto alienda Malaysia na kama kawaida media zika-report kuwa alialikwa na Waziri mkuu mstaafu wa Malaysia!!! yaani waziri mkuu wa Malaysia anamualika mbunge mmoja tu toka Tanzania!

images
 
  • Thanks
Reactions: FJM
maneno ya kafulila jana jioni hapa dodoma

" huu mjadala watu kukana hauna maana kabisa. wote wanaokana ndio wapiga debe wakubwa. waliyasema haya wanayoyakana. ni unafiki ndio unaowasumbua na uoga. kabla ya kuondoka, wote tulikaa pale sinza na kwa pamoja wakasema wanamuunga mkono, tukafika Kigoma wakarudia maeno yale yale ya kumuunga zitto. Iweje leo wanakana? Asilimia 85% ya wabunge wanamuunga mkono zitto kugombea urais. Wana kigoma tumeonewa sana. Muda umefika kuwepo usawa katika uongozi wa hii nchi. Hatuwezi kuwa wasindikizaji siku zote, wakati uwezo tunao. Tunaungwa mkono kila kona ya nchi na hata nje ya nchi, na kama ni demokrasia 2015 rais na makamu wake lazima watokee Kigoma. Rais wa Tanzania, Afrika Kusini, ujerumani na Malaysia wote wanataka umuona rais kijana Tanzania.Vyama vyote vya siasa humu nchini wanamtaka rais kijana, Kikwete mwenyewe anamtaka atakayemrithi awe kijana"

----------------------------------
Edward Lowassa For President 2015

Mmeenda mbali sana. Ni rahisi kwa Zitto kuchaguliwa na watanzania wote kuwa rais kuliko kuteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea wa Urais 2015.

Kwa hiyo la kwanza ilikuwa ni kujikita katika chama ili Zitto apate nafasi hiyo. Kumbuka huko kuna magwiji kama akina Slaa ambao wako tayari chama kife kuliko kuutoa uongozi wa juu kiasi hicho nje ya Kilimanjaro na Arusha. Likifanikiwa hilo, basi hii itakuwa ni turning point kubwa ya CHADEMA.

Sidhani kama hilo litatokea kabla ya 2020.
 
Kuna ubaya gani Zitto kuwa rais? kwani kuna degree ya urais? kama CDM hamumtaki mfukuzeni basi aje CCM tumpe urais huku waziri mkuu Nape.
 
nachoipendea cdm ni viongozi wake makini kuwastukia mamluki na kutoshughulika nao,.mfano mzuri ni shibuda na zitto..wanazidi kuexpose tamaa zao
 
Zito bado sana kwa urais kama anaemsukuma na kumshawishi kugombea urais alivyokuwa bado hadi anaingia madarakani alikuwa bado........
 
Itafikia pahala watu wa kaskazini watajiuliza kama ni kosa kwao kuwa watanzania!Kama ni kweli kuna watu wanaamini kuwa uongozi/urais hautakiwi kutokea kaskazini,yani kwamba hawakubali mtawala wa kaskazini,kutakuwa na ubaya gani kama watu wa kanda nyingine nao wakikataa kutawaliwa na watu wasiokuwa wa kanda yao?Mi naona haina haja ya kugombana,Kigoma chagueni rais wenu,Mbeya wafanye hivyo etc etc.Ni unafiki kwa wanaojiita watanzania kutoa kauli kama hizo.Hakuna haja ya kujiita mtanzania kama kuna watu wa kanda flani unaowaona si watanzania.
 
Binafsi najilazimisha kuamini kwamba ni kweli Mh. Kafulila ameweza kusema maneno hayo, ni maneno ambayo sikuyategemea kuyasikia kutoka kwa mwananchi wa Tanzania mwenye akili timamu, kwani yanakinzana na vigezo rahisi kabisa vya sifa za mtu kuwa Rais, Mh. Kafulila anataka tumchague Mh. Zitto Kabwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vigezo vifuatavyo: ​
  1. Asilimia 85% ya wabunge wanamuunga mkono Zitto kugombea urais. (Bunge ambalo haliwezi hata kuisimamia serikali leo hii linataka kutupendekezea Rais....??? Bunge la Ovyo...!! Bunge la kupiga usingizi, Bunge la kudai nyongeza ya posho tu.., Bunge la kuitikia "Ndiooo" hata kwa hoja muhimu zinazogusa maslahi ya Watanzania ndio linalotaka kutupendekezea Rais leo hii Watanzania...???, nani anataka hata kulisikia Bunge hili la hovyo ...???!!!)
  2. Wana kigoma tumeonewa sana. Muda umefika kuwepo usawa katika uongozi wa hii nchi. Hatuwezi kuwa wasindikizaji siku zote, wakati uwezo tunao. Tunaungwa mkono kila kona ya nchi na hata nje ya nchi, na kama ni demokrasia 2015 rais na makamu wake lazima watokee Kigoma. (Sikuwahi kutegemea hata siku moja kwamba nafasi za juu kabisa za uongozi wa nchi zinaweza kufanywa za kupokezana kwa mkoa kwa mkoa au kabila kwa kabila, Mh. Kafulila na Mh. Zitto wanataka kutupeleka wapi..??, wanataka kutupeleka kwenye vita vya ukabila tena..??? mbona wana mawazo ya hatari na ya kipumbavu namna hii...??)
  3. Rais wa Tanzania, Afrika Kusini, ujerumani na Malaysia wote wanataka umuona rais kijana Tanzania. (Upumbavu mwingine wa Mh. Kafulila anatumia vigezo muflisi kuhalalisha utumbo wake, sisi hatuchaguliwi Rais wa nchi yetu na Afrika Kusini,Ujerumani au Malaysia, kama wao wanashida ya kuona kwenye Televisheni Rais kijana si nchi zao zinafanyaga uchaguzi, basi wachague Rais kijana kwenye chaguzi zao, Kafulila asitumie mawazo muflisi kufanikisha tamaa zake za madaraka, mjinga sana Kafulila...!!)
  4. Vyama vyote vya siasa humu nchini wanamtaka rais kijana (Hapa sitaki ku-comment sababu nina hasira sana ..)
  5. Kikwete mwenyewe anamtaka atakayemrithi awe kijana (nafikiri kwa mawazo ya Watanzania wengi wameshapoteza imani na uongozi wa Rais JK, kuwaambia Watanzania kwamba Rais Kikwete anamtaka atakayemrithi awe kijana ni sawa na kumwambia mtu mwenye akili timamu asikilize ushauri wa mwendawazimu, hakuna mwenye imani tena si na Rais Kikwete, si na serikali yake wala si na Chama anachokiongoza cha Mapinduzi (CCM))
NB: Mwisho nalazimika kusema kwamba Mh. Kafulila unatumika na Chama Tawala (CCM) ili kuleta mgongano ndani ya CHADEMA na kuzorotesha nguvu za upinzani (CDM) katika kuelekea uchaguzi mkuu wa 2012, naelewa kwamba kwenye siasa kuna mchezo mchafu na kulipa fadhila lakini zisikufanye ukawa mjinga kupita kiasi mpaka ukashindwa hata kutumia akili kidogo uliyonayo kufikiri vitu vya msingi.
Mkuu, vita ya kuwatoa mafisadi kwenye kitumbua si ndogo, inahitaji uelewa na kujitoa haswa. Kumbuka mafisadi yana mbinu nyingi na yana mapesa, yalishajua bila kumuweka mtu wao pale magogoni yatakuwa kwenye hatari kubwa hapo 2015 kama raisi atakayeingia atakuwa moto, mfano halisi aingie Dr. Slaa. Pamoja na hayo, kuna makundi ndani ya chama tawala hayataki kushindwa ni kuharibiana tu huku yakitaka safe life baada ya matokeo. Na hawa vijana wa kigoma walishaonyesha udhaifu mkubwa tangia kwenye ile inshu ya Buzwagi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom