David Kafulila ajivua uanachama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Hili igizo tamu sana, lakini chungu. Dr. Slaa na kikaa walimuamuru Kufulila kuomba radhi na kukanusha hizo taarifa. Jamaa akakataa wewe ungekuwa maneja na mtumishi anakataa maagizo ya kikao ungefanyaje?

Ningemfuta kazi mara moja
 
Kitila,
Acha kumchafua kijana Kafulila, maana mchawi hapa anaonekana wazi kuwa ni Mbowe. Kafulila hakutaka kuondoka CHADEMA ila Mbowe ndiye aliyesisitiza kuwa aondolewe uongozini na kwenye chama. Kama una sababu za kutetea uamuzi wa Mbowe ziweke wazi, lakini usimpake kijana wetu matope.

Kama mtu anapigania maendeleo/ukombozi wa nchi yake, lazima siasa iwe ni kazi. Niambie ni msomi gani anayeweza kukubali kudhalilishwa na kihiyo kwa vile tu ana pesa na madaraka?

Kama Kafulila angekuwa anataka kukaa mjini kwa starehe si angekuwa ameshakimbilia CCM kuliko na madaraka yenye marupurupu kibao?

Kwa hiyo unataka kutuambia Kafulila kilichokuwa kinamuweka CHADEMA ni mshahara? Unafikiri kwa elimu yake hangeweza kupata mshahara mnono kuliko wa CHADEMA au NCCR? Shame on you Kitila. You should apologize to Kafulila.

Eti CHADEMA ni taasisi? What a joke? Taasisi gani yenye kufuata maamuzi ya mtu mmoja tu, Mbowe/Mtei?

Kitila, Kama wewe hujakatishwa tamaa na yanayoendelea ndani ya CHADEMA, basi una sababu nzito za kukumbatia uongozi wa Mbowe/Mtei.

Lakini dalili za hapa mtandaoni kama zitakuwa ni sambamba na Watanzania walioipenda Chadema, ni wazi kuwa wengi wameshaanza kukata tamaa. Hii ni pamoja na watu kama Mwanakijiji (angalia article yake ya jana juu ya upinzani) ambaye kwa mbali ameanza kuikosoa CHADEMA, kitu cha kushangaza kidogo.

Kuweweseka kwa CHADEMA ni kilio cha taifa. Na kama CHADEMA itafifia kama ilivyokuwa NCCR, wa kulaumiwa ni watu kama wewe Kitila ambao mnaweka maslahi binafsi mbele badala ya kuongea ukweli juu ya madudu ya Mbowe.

I am sure Zitto is next on the guilotine.

Leave Kitila alone
teh teh teh
 
Ha ha ha! Umekosa ulichokuwa unakitegemea kutoka kwa Doc sasa Mapovu yanakutoka LoL!
 
Hili igizo tamu sana, lakini chungu. Dr. Slaa na kikaa walimuamuru Kufulila kuomba radhi na kukanusha hizo taarifa. Jamaa akakataa wewe ungekuwa maneja na mtumishi anakataa maagizo ya kikao ungefanyaje?

Kama ni kweli Kafulila alifukuzwa kwa sababu ya hayo maneno, then Dr. Slaa ni mjinga na mnafiki. Kwa sababu, kabla ya hayo mahojiano na gazeti, Mbowe tayari alishatoa matakwa yake kuwa Kafulila afukuzwe uongozi na uanachama, kisa eti mjeuri. What a joke for a leader?
 
Aliyatoa kwenye Platform gani? Nahisi kama wewe ndiye huyo Mwandishi kwenye hilo Igizo! LoLo
 
Kwa wanaonifahamu nawaomba wamwambie huyo kijana anitafute nitakuwa namlipa mshahara aendelee kukaa hapa town.

Kitila,

Mshitue kijana anitafute. Unajua pa kunipata
 
Kama ni kweli Kafulila alifukuzwa kwa sababu ya hayo maneno, then Dr. Slaa ni mjinga na mnafiki. Kwa sababu, kabla ya hayo mahojiano na gazeti, Mbowe tayari alishatoa matakwa yake kuwa Kafulila afukuzwe uongozi na uanachama, kisa eti mjeuri. What a joke for a leader?

Hayo Matakwa yalitolewa na Gazeti kwa niaba ya Mbowe, unajua nyinyi Waandishi ni Bajanja sana, Mmempa kijana Sababu ( Bila ya yeye kujua hila zenu) awatukane Viongozi wenzake yaani tunasema Kijana amekuwa Triggered bila ya yeye kujua ila mmefanikiwa aisee!
 
Kitila,
Acha kumchafua kijana Kafulila, maana mchawi hapa anaonekana wazi kuwa ni Mbowe. Kafulila hakutaka kuondoka CHADEMA ila Mbowe ndiye aliyesisitiza kuwa aondolewe uongozini na kwenye chama. Kama una sababu za kutetea uamuzi wa Mbowe ziweke wazi, lakini usimpake kijana wetu matope.

Kama mtu anapigania maendeleo/ukombozi wa nchi yake, lazima siasa iwe ni kazi. Niambie ni msomi gani anayeweza kukubali kudhalilishwa na kihiyo kwa vile tu ana pesa na madaraka?

Kama Kafulila angekuwa anataka kukaa mjini kwa starehe si angekuwa ameshakimbilia CCM kuliko na madaraka yenye marupurupu kibao?

Kwa hiyo unataka kutuambia Kafulila kilichokuwa kinamuweka CHADEMA ni mshahara? Unafikiri kwa elimu yake hangeweza kupata mshahara mnono kuliko wa CHADEMA au NCCR? Shame on you Kitila. You should apologize to Kafulila.

Eti CHADEMA ni taasisi? What a joke? Taasisi gani yenye kufuata maamuzi ya mtu mmoja tu, Mbowe/Mtei?

Kitila, Kama wewe hujakatishwa tamaa na yanayoendelea ndani ya CHADEMA, basi una sababu nzito za kukumbatia uongozi wa Mbowe/Mtei.

Lakini dalili za hapa mtandaoni kama zitakuwa ni sambamba na Watanzania walioipenda Chadema, ni wazi kuwa wengi wameshaanza kukata tamaa. Hii ni pamoja na watu kama Mwanakijiji (angalia article yake ya jana juu ya upinzani) ambaye kwa mbali ameanza kuikosoa CHADEMA, kitu cha kushangaza kidogo.

Kuweweseka kwa CHADEMA ni kilio cha taifa. Na kama CHADEMA itafifia kama ilivyokuwa NCCR, wa kulaumiwa ni watu kama wewe Kitila ambao mnaweka maslahi binafsi mbele badala ya kuongea ukweli juu ya madudu ya Mbowe.

I am sure Zitto is next on the guilotine.

KITILA MNAFIKI MKUBWA ALIKUWA KUNDI LA ZITTO KABWE WAKATI WA UCHAGUZI AMEONA KUNA CHEKECHO LINAKUJA KUWABANA WATU WA ZIITO NDIO ANAJIWAHI KUTENGENEZA KINGA.

ANASEMA KUWA NCCR INAMNUNUA KAFULILA KWANI YEYE KITILA ALIPOENDA NCCR ALIPEWA KIASI GANI?
UZURI ULIOUONA WEWE KITILA NDIO ANAOUFUATA KAFULILA.

KITILA KABADILISHA VYAMA SANA HAKUNA ALIYEMSEMA KWANI NI DEMOKRASIA YAKE. NILIWAHI KUSOMA MAONI KUWA KITILA ALIBADILISHA VYAMA KAMA ANAVYOBADILISHA NGUO NDOGO.JEE KITILA ULIKUWA UKO KWENYE AJIRA au ULIKUWA HUNA CHUMBA?

CHADEMA WAMEMNUNUA LWAKATARE NA KUMPA AHADI NYINGI TU.KAMA KAFULILA ATAPEWA MAHITAJI HAYO NA CUF AU TLP HAKUNA TAABU.
BY THE WAY SUALA LA KITILA MKUMBO NA DOMESTIC VIOLENCE UMEFIKIA WAPI?

KITILA UMUOGOPA DJ KIASI HIKI? UNAOGOPA KUVULIWA UANACHAMA?

MKANDARA.

NIMEKUONYA MARA NYINGI KUWA MAKINI NA VYAMA KAMA HIVI USIBABAIKE NA KAMPENI ZAO HAPA JF WAONE WATU KAMA KINA KAFULILA WAKUELEZE ADHA ZINAZOPATIKANA HUKO.ULIONA WAPI MWENYEKITI NDIO MTIA SAINI WA HUNDI ZA CHAMA. PIA KOMU NA MBOWE NI NDUGU WA DAMU.

MIMI NILIWEKA MADA YA KINA KAFULILA KUFUKUZWA UANACHAMA HAPA HAPA JF MJADALA ULIHAMISHWA KWA HARAKA SANA UKAPELEKWA SEHEMU YA UDAKU.LEO KIKO WAPI?
ACHENI MAPENZI YA UPOFu.
 
Chama wameanzisha wenyewe kwa pesa zao, wamehangaika nacho mpaka kimekuwa maarufu sasa mnataka ujiko wachukue watu wengine! Hata mimi ningekuwa Mwenyekiti Mbowe nisingekubali.

Kafulila alitakiwa ajifunze kutoka kwa Mapalala, Mrema, Wangwe (RIP) Nyaruba, Akwilombe, Lamwai, Marando nk.

Somo la leo ni kuwa USIONE VYAELEA VIME UNDWA!
 
We Masatu umesahau Kumtaja Kolimba!
 
Swahiba wa Zitto Kbwe ajitoa uanachana Chadema
Na Ramadhan Semtawa
MSHIRIKA wa mkubwa kisiasa wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, David Kafulila, ametangaza uamuzi mzito wa kujitoa katika chama hicho huku akidaiwa kujiandaa kukimbilia NCCR Mageuzi.

Wakati uamuzi huo umeibua hisia na misimamo tofauti ndani ya Chadema huku wenyeviti 11 wakidaiwa kumpinga Dk Slaa, jana Kafulila aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kutangaza msimamo huo wa kujitoa Chadema na kumshambulia Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na Dk Slaa.

Ingawa alisita kuweka bayana wapi atakimbilia, lakini habari zilizotufikia zilidokeza kwamba, anajianda kukimbilia NCCR-Mageuzi, ambacho kina nguvu Kigoma Kusini anakotarajia kuwania ubunge mwakani.

Hata hivyo, Kafulila alisema alifikia uamuzi huo baada ya kuona lengo lake la kujenga upinzani imara linahujumiwa na Dk Slaa kwa kumwekea uzio asiweze kuchaguliwa.

Akitangaza uamuzi huo alisema: "Kwa dhamira yangu binafsi, baada ya kukaa kufikiria na kisha kujiridhisha na kupata ushauri kwa watu ninaowaheshimu sana, nimeamua kujitoa Chadema kuanzia leo, ... mimi si mwanachama wa Chadema," alitangaza Kafulila na kufanya ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kuzizima na kuongeza:

“Ni uamuzi mzito, lakini roho yangu ni nyeupe, sina kinyongo na mtu nimefanya uamuzi huu kwa nia ileile na sitatoka nje ya mstari,... lengo ni kujenga Strong Opposition (upinzani imara) nchini.

"Sijasukumwa na mtu, ni uamuzi ambao umeanzia katika nafsi yangu mwenyewe, ikaja ngazi ya familia na kuendelea juu.

"Nimeondoka Chadema, ila natoa rai kwa wanachama hasa vijana wenzangu kwamba, uhai wao ndani ya chama hicho utategemea sana utiifu wao wa, zidumu fikra za Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu Slaa.

“Nataikumbuka Chadema kwa kuwa mnamo Desemba7, 2008, damu yangu ilimwagika wakati wa utumishi wangu katika kazi ya ujenzi wa chama hicho."

Kafulila mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja, kuchapa kazi, alisema uamuzi huo umeangalia mbali kutokana na kuona dhahiri amenyang'anywa fursa ya kuchaguliwa na kubakiziwa ile ya kuchagua tu.

Kafulila ambaye aliwahi kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Taifa la chama hicho (Bavicha) katika uchaguzi wa chama hicho hivi karibuni ambayo matokeo yake yalibatilishwa, alidai kuwa hatua ya Dk Slaa ilimuondolea nafasi ya kuchaguliwa na kufifisha ndoto yake ya kujenga upinzani imara nchini.

"Lengo langu limekuwa ni kujenga upinzani imara, lakini niliondolewa fursa hii ndani ya Chadema, katiba ya Chadema inataja mwanachama anaweza kuondoka kwa kujiondoa au kuondolewa kwa kifo kama Chacha Wangwe, sasa mimi nimejiondoa mwenyewe siyo kifo," alifafanua Kafulila.

Alidia kwamba, alifukuzwa uanachama kwa siri ikiwa ni kwasababu ya uongozi mbovu Mbowe. " Si mwanasiasa (Mbowe) ni mfanyabiashara, yuko radhi abaki na wabunge wawili ili aangalie biashara zake, lakini si maslahi ya chama."

Kafulila aliongeza kwamba, kiutaratibu wanachama wote wa Chadema wako chini ya uongozi wa chama, lakini yeye akatakiwa awe nje ya uongozi wa chama.

Alisema kuwa chuki na baadhi ya viongozi hao wa juu, kwamba inatokana na msimamo wake wa kuhoji matumizi ya fedha za chama, zikiwemo Sh35 milioni, za ruzuku ya Desemba ambazo mpaka sasa hazijulikani zilipo.

Alifafanua kwamba, watia saini katika hundi za kuchukua fedha za ruzuku ya chama ni Mbowe, Dk Slaa na Anthony Komu, na kuhoji Mwenyekiti kuwa mtia saini wakati yeye ndiye anapaswa kuiwajibisha Sekretarieti endapo itafanya ufisadi.

Kafulila alimtaka Mbowe kujiondoa kwenye orodha ya watiaji saini, kwani huko ni kukiuka taratibu za uendeshaji taasisi.

Ajifunze kwa CCM, NCCR, CUF. mbona Lipumba (Ibrahim), Mbatia (James) si watia saini; kwanini yeye ang'ang'anie?" alihoji na kudai:

"La kushangaza watia saini katika fedha za mfuko wa kuchangia chama kwa njia ya SMS pia ni Mbowe na Komu tu; hata hivyo, watu hawa wawili hawakuteuliwa na kikao chochote kufanyakazi hiyo".

Alisema Mkurugenzi wa Fedha (Komu), ndiye mwamuzi kwa kiasi kikubwa katika hatua zote za kuandaa bajeti, kuchukua fedha benki, kuidhinisha matumizi na kufanya maamuzi.

" Hii ni kinyume na utaratibu wa kanuni za matumizi ya fedha za taasisi," alidai

Kijana huyo ambaye aliwahi kuanguka kutoka ghorofa ya kumi akifanya kazi ya kuimarisha Chadema, alisema aliwahi kuhoji fedha hizo, lakini akazimwa na kuelezwa kwamba, yeye ni mwandishi wa muhtasari wa vikao na si mjumbe hivyo akae kimya.

"Nilimwambia Dk Slaa, siwezi kukaa kimya kuzungumzia mambo ya msingi, ni bora niende kuwa mfagiaji kuliko kuzuiwa kusema ukweli unaohusu chama," alidai.

Kafulila aliongeza kwamba, alishangazwa pia na mwendelezo wa chuki dhidi yake ambao ulikuwa ukifanywa na Dk Slaa, kwa kutaka kumchukulia hatua kwa madai ya kumpigia kampeni Zitto, wakati uchaguzi ulikwishapita.

"Dk Slaa alinihoji na kutaka kunichukulia hatua kwasababu nilishiriki kumfanyia kampeni Zitto Kabwe. Lakini John Mrema, John Mnyika, Komu na Benson Kigaila waliokuwa wakimfanyia kampeni Mbowe hawakuhojiwa," alidai na kuongeza:

"Haki haikutendeka kwa kuwa sisi sote tulikuwa watendaji wa makao makuu ya chama. Moja ya sababu kuu iliyonishawishi kumuunga mkono Zitto ni hoja yake aliyotoa bungeni kutaka CAG akague matumizi ya fedha za ruzuku za vyama vya siasa. Ni Ukweli usiopingika inawezekana Chadema kuwa kati ya vinara katika taasisi zenye matumizi mabaya ya ruzuku".

Hii ni hatua nyingine ya Chadema kupita katika wakati mgumu kisiasa, baada ya kukumbwa na hali kama hiyo wakati wa akina Dk Amani Walid Kabourou ambaye alijitoa Chadema kutokana na kutoelewana na baadhi ya viongozi wa juu.

Kujitoa kwa Kafulila ni matokeo ya majeraha ya uchaguzi wa Septemba, ambayo Baraza la Wazee wa chama hicho wakiongozwa na mzee Edwin Mtei, ambao waliokoa jahazi katika uchaguzi uliopita kwa kumshauri Zitto amwachie Mbowe nafasi ya uenyekiti taifa.

Source: Gazeti la Mwananchi

Kafulila kafukuzwa au kaachia ngazi mwenyewe? Moja linaloonekana hapa, kama ilivyokuwa kwa marehemu Wangwe, tatizo ni lile lile, Mbowe na Ruzuku. Hivi haya hayatatuliki kukiokoa chama?
 
chama wameanzisha wenyewe kwa pesa zao, wamehangaika nacho mpaka kimekuwa maarufu sasa mnataka ujiko wachukue watu wengine! Hata mimi ningekuwa mwenyekiti mbowe nisingekubali.

Kafulila alitakiwa ajifunze kutoka kwa mapalala, mrema, wangwe (rip) nyaruba, akwilombe, lamwai, marando nk.

Somo la leo ni kuwa usione vyaelea vime undwa!
mie nimechoka pale aliposema kuwa chadema ina njia mbili za kumuondoa mtu uanachama ya kwanza kujiuzulu mwenyewe au ya pili unatafutiwa kifo kama alivyofutwa uanachama chacha wangwe kwa njia hii ya pili.

kafulila kaona aanze kwa kutumia njia ya kwanza kuliko kusubiri ajali.

nimeona kale kazee ka chadema kako online sijui katajibu hapa?
 
Kafulila kafukuzwa au kaachia ngazi mwenyewe? Moja linaloonekana hapa, kama ilivyokuwa kwa marehemu Wangwe, tatizo ni lile lile, Mbowe na Ruzuku. Hivi haya hayatatuliki kukiokoa chama?

interview ya mbowe imeishia wapi?
 
ni kama ilivyotokea kwa kolimba, kabeho, kibona, mama mbatia nk
 
Kafulila kafukuzwa au kaachia ngazi mwenyewe? Moja linaloonekana hapa, kama ilivyokuwa kwa marehemu Wangwe, tatizo ni lile lile, Mbowe na Ruzuku. Hivi haya hayatatuliki kukiokoa chama?

Soma hapa ulipo highlight Mwenyewe

Akitangaza uamuzi huo alisema: "Kwa dhamira yangu binafsi, baada ya kukaa kufikiria na kisha kujiridhisha na kupata ushauri kwa watu ninaowaheshimu sana, nimeamua kujitoa Chadema kuanzia leo, ... mimi si mwanachama wa Chadema," alitangaza Kafulila na kufanya ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kuzizima na kuongeza:

Au ulikuwa hauelewi nini?
 
"Nimeondoka Chadema, ila natoa rai kwa wanachama hasa vijana wenzangu kwamba, uhai wao ndani ya chama hicho utategemea sana utiifu wao wa, zidumu fikra za Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu Slaa.

Kwa ushauri huu nakubali kabisaa kuwa CHADEMA ya Mbowe ni NGO.

Mbowe and Mtei have to go for CHADEMA to survive.
 
Samahanini jamani, nasikitika kuwataarifu kuwa yule aliyekuwa Ofisa
Habari wa Chadema Kafulila kajivua uanachama leo. Chakujiuliza chama
hiki kinaelekea wapi?

nenda mwana kwenda..tuachie chama chetu
 
Kwa ushauri huu nakubali kabisaa kuwa CHADEMA ya Mbowe ni NGO.

Mbowe and Mtei have to go for CHADEMA to survive.

Hivi mbona mnaisakama sana CHADEMA..si na wewe uanzishe chama chako ...ndio kafukuzwa na kama ni NGO ya Mbowe then what??nenda chama ambacho sio NGO ya mtu..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom