David Kafulila ahamia NCCR Mageuzi akitokea CHADEMA

<A class=footernote href="http://mail.mwananchi.co.tz/">Email
Advert Rates
chifupa.jpg
menuarrow.gif
Burudani
menuarrow.gif
Makala
menuarrow.gif
Habari nyingine
menuarrow.gif
Hadithi
menuarrow.gif
Kolamu
menuarrow.gif
Maoni ya wasomaji
menuarrow.gif
Habari na Picha
menuarrow.gif
Nafasi za kazi
menuarrow.gif
Kona ya Marafiki Habari zingine za mbele Date::11/14/2009Chadema hali tete wenye viti mikoa 11 wapinga uamuzi wa Dk Slaa
walimu%20mgomo.jpg
Walimu wa shule ya msingi na sekondari jijini Dar es Salaam wakiingia kwa maandamano katika uwanja wa Uhuru kusherekea maadhimisho ya siku ya walimu Duniani
broken-heart.jpg
Ramadhan Semtawa na Fidelis Butahe

UAMUZI wa katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa wa kuwatimua maafisa wawili wa sekretarieti, umekifanya chama hicho kugubikwa na wingu zito baada ya wenyeviti wa mikoa 11 kumpinga, akiwemo katibu wa Kigoma, Msafiri Wamarwa ambaye amejitokeza kutangaza kuwatambua waliotimuliwa.

Wiki iliyopita, Dk Slaa, ambaye kwa cheo chake ni mkuu wa sekretarieti ya chama hicho, alitangaza kumtimua David Kafulila kwenye nafasi ya afisa habari, sambamba na Danda Juju ambaye alikuwa akihusika na mambo ya Bunge kwa madai kuwa wawili hao waliofananishwa na sisimizi walionyesha utovu wa nidhamu na kuvujisha siri za chama.

Jana, wenyeviti wa mikoa hiyo 11, ambayo baadhi iko nyanda za juu kusini, mashariki na kaskazini (majina yao tunayo), waliweka bayana kwamba uamuzi wa Dk Slaa haukubaliki hadi atakapotoa sababu za msingi za kuwafukuza maafisa hao.

Viongozi hao wakiweka sharti la kuhifadhiwa majina ili wajipange vema kwa ajili ya mkutano wa Kamati Kuu uliopangwa kufanyika Novemba 27 na 28, walisema uamuzi huo unaonekana kulenga watu ambao walikuwa upande wa naibu katibu mkuu, Zitto Kabwe na kutaka usitishwe mara moja.

"Hatuwezi kuendesha chama kwa visasi... mambo ya uchaguzi wa Septemba yalishapita, sasa tunavyoanza kuleta chuki za kipuuzi tunataka chama kife," alihoji mwenyekiti wa moja ya mikoa ya kaskazini.

Mwenyekiti mwingine kutoka moja ya mikoa wa kusini aliweka bayana kwamba Chadema ni chama ambacho kipo kwa ajili ya makundi ya watu wote si tabaka fulani.

"Angalia Dk Slaa anamwita Kafulila sisimizi, hii ni dharau ya hali ya juu. Ina maana kuna sisiminzi na tembo ndani ya chama... hivi kweli tutafika kwenye uchaguzi kama watu wanakuwa na roho mbaya na dharau za kiasi hiki," alihoji mwenyekiti huyo kutoka kusini.

Mmoja wa wenyeviti kutoka moja ya mkoa wa mashariki aliweka bayana kwamba chama hicho kwa sasa kinaelekea kugawanyika rasmi kama kutakuwa na mwendelezo wa majeraha ya uchaguzi wa Septemba.

Aliongeza kwamba mambo yaliyotokea wakati wa uchaguzi yaliisha hivyo kambi za mwenyekiti Freeman Mbowe na Zitto hazitakiwi kuendelea, bali kujenga chama kiwe kimoja kinachotakiwa kushinda uchaguzi mwakani.

Wenyeviti hao wengine waliisisitiza kwamba kimsingi wanapinga vikali uamuzi huo wa Dk Slaa, lakini hawataki kuanza kunukuliwa majina kwenye vyombo vya habari kwani wanamsubiri Dk Slaa kwenye Kamati Kuu aeleze sababu za msingi na kutosha.

Wakati wenyeviti hao wakiweka msimamo wao kwa nyakati tofauti, Wamarwa ambaye anatoka mkoani Kigoma ambako Kafulila ameonyesha nia ya kutaka kuwania ubunge wa jimbo la Kigoma Kusini, aliweka bayana kwamba hatambui uamuzi wa kuwavua madaraka wawili hao.

Kwa mujibu wa Marwa, mkoa haujapewa taarifa na makao makuu juu ya uamuzi huo na hivyo bado wanawatambua kama watendaji wa Chadema.

â&#8364;&#339;Habari hizi tumeziona kwenye vyombo vya habari, lakini mimi kama katibu wa mkoa, ofisi yangu haijapewa taarifa zozote za kimaandishi zinazoeleza juu ya kufutwa nyadhifa kwa Kafulia na Danda, hivyo sisi bado tunawatambua,â&#8364; alisema Wamarwa.

Mwananchi imedokezwa kuwa hadi jana jioni, Kafulila hakuwa amepewa barua rasmi ya kumvua wadhifa wake.

â&#8364;&#339;Hata kama tutapewa taarifa na makao makuu, tutakaa kama uongozi wa Chadema mkoa na kujadili maamuzi hayo na tutatoa maamuzi yetu,â&#8364; alisisitiza Wamarwa.

Alifafanua kwamba hivi sasa chama kimejaa mamluki ambao kazi yao ni kuhahakikisha wanawagombanisha baadhi ya viongozi wa juu ili kuhakikisha Chadema haifanyika vizuri uchaguzi wa 2010.

â&#8364;&#339;Haya mambo yakiendelea chama kitakufa kama ilivyokuwa kwa vyama vingine vya upinzani. Umefikia wakati wa kuwatimua wale wote wanaoendeleza mambo yaliyozimwa katika uchaguzi mkuu wa chama Septemba mwaka huu,â&#8364; alisema Wamarwa.

Wamarwa pia alisema kuna haja ya kuitishwa haraka kikao cha Baraza Kuu la Taifa ili kujadili mwelekeo wa chama hicho.

"Siwezi kusema tutaamua nini kwa sababu ni lazima tukae uongozi mzima wa mkoa... lakini pamoja na hayo Baraza Kuu la Taifa inabidi likutane mara moja kwa sababu hali inaonekana inakwenda vibaya kila siku zinavyozidi kwenda," alisema Wamarwa.

"Hata katika uchaguzi wa serikali za mitaa, Chadema tumeshinda Kigoma kwa asilimia 70, na Kigoma Kusini ambako Kafulila atagombea ubunge tumeshinda kwa asilimia 80, hivyo ipo haja ya kulizungumza hili kwa umakini mkubwa."

Tayari Zitto ameshaeleza bayana athari za maamuzi hayo hasa katika kipindi ambacho Chadema imetoka katika mtikisiko uliosababishwa na uchaguzi wa viongozi wake.

Zitto, ambaye yuko nje ya nchi, alisema chama kilitakiwa kuwa makini katika kufikia uamuzi huo, hasa kwa kuzingatia kuwa Kafulila atagombea ubunge wa Kigoma Kusini na mustakabali wa chama kwa sasa.

Lakini, Dk Slaa aliliambia gazeti hili kuwa uamuzi huo ni kwa maslahi ya chama na haulengi kundi fulani na kutamba kwamba kutimuliwa kwa wawili hao hakutasababisha mpasuko. Alisema ni bora chama kupasuka kuliko kufa.

Wakati chama kikijiweka sawa baada ya kuwatimua wawili hao, Kafulila atakuwa mmoja wa wachangiaji kwenye mkutano wa taasisi ya Mo Ibrahim, kwa mujibu wa barua ya mwaliko.

Taasisi ya Mo Ibrahim imekuwa ikijihusisha na utekelezwaji wa dhana ya utawala bora barani Afrika na imekuwa ikitoa tuzo kwa rais mstaafu kwa kuangalia jinsi alivyotekeleza dhana hiyo wakati akiwa madarakani.

"Hii si heshima kwangu tu, bali kwa taifa na chama changu cha Chadema," alisema Kafulila akizungumzia mwaliko huo.

"Nitatumia nafasi hii kutowaangusha Watanzania kwa ujumla katika kujadili mambo ya msingi yanayohusu bara la Afrika." Kafulila ni mmoja wa vijana wa Chadema ambao wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika chama. Aliwahi kuanguka ghorofani akiwa katika harakati za kujenga chama.
 
Wakuu
DAVID Kafulila yule jamaa aliyejivua uanachama CHADEMA na kuhamia NCCR amekataa kukabidhi kadi ya CHADEMA na kudai kwamba ni mali yake. Pamoja na kuktaa kukabidhi kadi hizo pia Kafulila alionekana amevaa sare ya CHADEMA kwa jina maarufu la kombati katika kikao na waandishi wa habari alipokuwa akikabidhiwa kadi ya NCCR.Alipohojiwa kwanini amevaa vazi la CAHDEMA alidai kwamba lile sio vazi la CADEMA bali ni mali yake.Kwa hali hii nina mashaka na kijana huyu huenda akawa ana siri nyuma ya pazia na bado anaipenda sana CHADEMA.

Wakati mwingine ni 'utoto' tu unaosumbua:rolleyes:!
 
kijana unaonekana upo nyuma sana na maisha halisi ya tanzania...
unavyoonekana wewe ni mchaga unayetaka eidha hao waandishi waandike kusu mbowe au kilimanjaro...
kinachokuuma wewe sasa hapo ni nini?..mbona mwandishi ameandika habari ya kueleweka?,,tena ni ripoti ya tukio lililotokea wala hata hakuandika mawazo yake binafsi...
vipi ndugu umetumwa nini...
mbona mwanahalisi na nipashe kipindi yalipowakomalia kina zitto,kafulila,mtemelwa na wenzake hukunyanyua mdomo wako?
this is JF na sio uwanja wa majungu dogo!!!!!!!!!.
kama huna issue you better keep quet???
 
Sioni kosa la gazeti la Mwananchi hata kidogo pengine mleta hoja aje na matoleo mengine kuthibitisha anachodai.Kwangu mimi gazeti la Mwananchi linaendelea kushika nafasi ya kwanza kwa kuandia habari kwa kufuata misingi ya uandishi wa habari.

Gazeti la Tanzania daima ndiyo gazeti la hovyo kupita hata gazeti la Uhuru na Mtanzania.
 
tatizo linalosumbua hapo ni ushabiki na si kitu kingine chochote?....
mbona mimi sioni tatizo la mwananchi kuripoti habari ambazo mnazilaumu?....
mbona absalom kibanda alishakuja na udaku wake akimpaqmba bosi wake?...
lakini mboni hamsemi lolote kuhusiana na magazeti ya wachaga kama vile MWANAHALISI na NIPASHE ambayo kila leo yalikuwa yanawachafua wapigania haki hao?...
hivi haujui UHURU WA KWELI HAUWEZI KUPATIKANA TANZANIA KAMA HATA HAO WENYEWE CHADEMA WAMESHINDWA KU-PRACTICE?...
 
Kuhusu kupoteza mwelekeo si Mwananchi pekee ni magazeti yooote sioni ambalo unawezasema lina afadhali. Yoote yamekuwa na upande na yanaandika kwa manufaa binafsi ya waandishi. Angalia Mtanzania? T.Daima, Nipashe WAPI NI WAPI. Afadhali hata majira na Habari Leo
 
Yaani kuiandika Chadema katika namna msiyoipenda ndio gazeti kupoteza mwelekeo?

Hamjalazimishwa kulisoma after-all magazeti yapo mengi nendeni mkasome TanzaniaDaima au magazeti ya Shigongo ebo!
 
someni hapa,

Takwimu za matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Oktoba, zinaonyesha kuwa NCCR ni chama chenye wafuasi wengi katika jimbo la Kigoma Kusini ikifuatiwa na Chadema.
NCCR inashikilia vijiji 11 ambavyo vingi viko katika tarafa ya Nguruka ambayo ina asilimia 40 ya wapigakura wote katika jimbo hilo huku Chadema ikiwa na vijiji 12
eneo la mwambao wa Ziwa Tanganyika likiwa na wakazi wachache, lakini nguvu hiyo pia ikielezwa kutokana na ushawishi na juhudi binafsi za Kafulila.
soma na hii,
"Hata katika uchaguzi wa serikali za mitaa, Chadema tumeshinda Kigoma kwa asilimia 70, na Kigoma Kusini ambako Kafulila atagombea ubunge tumeshinda kwa asilimia 80, hivyo ipo haja ya kulizungumza hili kwa umakini mkubwa."

Hili ni gazeti moja , alipokuwa CHADEMA waliandika hivyo alipoenda NCCR wakaandika ndio chama chenye nguvu , jadilini hoja.
 
kijana unaonekana upo nyuma sana na maisha halisi ya tanzania...
unavyoonekana wewe ni mchaga unayetaka eidha hao waandishi waandike kusu mbowe au kilimanjaro...
kinachokuuma wewe sasa hapo ni nini?..mbona mwandishi ameandika habari ya kueleweka?,,tena ni ripoti ya tukio lililotokea wala hata hakuandika mawazo yake binafsi...
vipi ndugu umetumwa nini...
mbona mwanahalisi na nipashe kipindi yalipowakomalia kina zitto,kafulila,mtemelwa na wenzake hukunyanyua mdomo wako?
this is JF na sio uwanja wa majungu dogo!!!!!!!!!.
kama huna issue you better keep quet???

Wale wale, badala ya kujadili hoja unataka kuonyesha kuwa mleta hoja ndio tatizo, Nchi hii inahitaji miaka .... na nyie ndio mnajiona middle class ya Tanzania .
 
mti wenye matunda ndio huwa unarushiwa mawe...CHADEMA MSIYUMBISHWE na wapumbavu...
 
unataka kutuambia kuwa nikivaa shati la kijani nitakuwa mwana CCM? yeye ndie aliyevaa na bahati nzuri kaulizwa na katoa jibu kuwa ni mali yake so nini cha kujadili?
Wewe jifanye kuvaa kombati inayofanana na ya jeshi halafu uwaambie ni ya kwako uone cha moto!!
 
[
Na leo wameandika tena uongo mwingine ,
maswali ya kujiuliza ni kama yafuatayo;
1.Je? Gazeti la Mwananchi lina masilahi gani?
2.Wanaandika kwa masilahi ya nani?
3.Wametumwa na nani?
4.Waandishi wa habari hizi kila siku ni ama Ramadhani Semtawa au Fidelis Butahwe.
5.Gazeti la Mwananchi mara nyingi limekuwa likiandika kuwa CHADEMA wana nguvu kubwa Kigoma kusini , leo wanasema ni NCCR je? wanataka kutrupeleka wapi?

Nimekuwa nikijiuliza maswali haya sana kwani linaonekana linafanya kazi maalum na haswa linapokujua suala la CHADEMA .
Wanaojua watuelimishe hapa,.[/QUOTE]

Kiranja
Mawazo kama Yangu.Kuna siri kubwa hapa.
 
sijakuelewa unapolazimisha kuwa kombati ni vazi la CHADEMA!!

Kigogo
Kombati ni vazi la CHADEMA hata ukibisha.Nido vazi lao rasmi la chama popote ukipita ukiwa umevaa hivyo unatambulika wewe ni CHADEMA kama unabisha vaa siku moja kombati ya khaki halafu pita barabarani au nenda ofisi za CCM uone.
 
kombati hata kama haina maandishi ya CHADEMA,CHADEMA ni vazi la CHADEMA? au fafanua

Msasa
Komabti za CHADEMA zijawahi kuona zinamaandishi labada kama zipo ila ninavyofahamu ni kwamba hazina maandishi,kwahiyo ukivaa tu wewe ni CHADEMA
 
au nae anajaribu kuharibu upinzani? juzi alikuwa anahojiwa kwenye mlimani tv alionekana hana uungwana na alikili alikuwa nayafanya hayo akijua ni kwa maslahi ya chadema......huyu dogo(sijui dogo kweli au umbile?) atakuwa na matatito lakini pia zitto atakuwa nyuma ya huyu bwana kwani ni swaiba wake..............
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom