David Kafulia kuzungumza yaliyojiri NCCR: LIVE ON STAR TV

Asante Yahya kwa kuuliza maswali yangu sawia. Ombi la mwisho ...hapa jf kuna waraka wa kafulila alipokuwa akimshauri marehemu Chacha Wangwe kuwa demokrasia bila nidhamu ni kupotea. Hapa ulikuwa ukimwonya wangwe Kupingana na viongozi waandamizi cdm.,leo hii umepingana na kamati kuu nzima ya nccr,sasa mh.unaweza kufuta waraka wako ili wafuasi wenu tujue msimamo wako kwa kuwa waraka uliouandika umekugeukia mh? Samahani kwa kumhusisha marehemu wangwe kwenye mjadala,namuombea mapumziko mema wangwe!
 
Kafulila:Ikitokea maamuzi ya Mahakama yakafanana na NCCR' kwamba uanachama wako umethitishwa rasimi' vyp utasimama wapi?
 
KAFULILA,kwa nini hujajibu swali lililokuuliza kuna mapungufu gani kwenye katiba NCCR MAGEUZI?Je unamgogoro binafsi na MBATIA NA RUHUZA?,Na kwa nini kafulia umekuwa mtu ambaye unahoja za msingi lakini hufuati taratibu za chama/tasisi?
 
Kafulila wewe ni muungwana ,nikiangalia tofauti ya Mada ya week iliyoisha kati ya viongozi wa NCCR Mageuzi kwanza walikuwa wakiongea kwa Jazba kubwa wakikukandamiza na wewe kuonekana unamakosa makubwa mtovu wa nidhani na kila lawama kwako ,Lakini kwako imekuwa tofauti unaongea kwa umakini bila kumchambua mtu yoyote vibaya na umesimamia kwenye point zaidi ,.. all the best mie ni msikilizaji na imani haya malumbano yenu yataisha na ujipange vyema sasa

Nakuunga mkono mtoa hoja. Huyu kijana ni mpiganaji bali kuna wale ambao bado wana fikra za zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wanasumbua. Machali kijana mdogo lakini ana mambo ya kizamani na ni mroho wa madaraka
Thanks Yahya M
 
Nachangia hoja hii kwa kuangalia changamoto na matarajio ya Siasa huria kuanzia mwaka 1961-1965 na kujirudia 1992-na kuendelea.
Lazima tuelewe kwamba mfumo wa chama kushika hatamu,haukuruhusu wigo mpana kwa wanachama kuweza kutoa mawazo tofauti na meza ya mwenyekiti.Ulikuwa ukipingana na meza ya mwenyekiti basi utachukuliwa hatua ya kufukuzwa uanachama lakini hata uraia,kwa mfano haya yalimkuta Kambona,Kolimba na wengi wengine ndani ya CCM.
Nasote tunaelewa kwamba mwanadamu yeyote amekulia katika taasisi mbalimbali za kijamii na kuweza kufinyanyangwa na taasisi hizo kimaadili na kifikra,yaani kama familia,dini,shule na jamii inayomzunguka,kwa hiyo ni lazima watu wawili waliokulia katika mazingira tofauti ya kisiasa,kijamii na kiuchumi kuwa tofauti.
Viongozi wa vyama vya siasa lazima wafike pahala wasiendelee kukariri njia moja tuu katika kukabiriana na changamoto za hoja ndani ya vyama vya siasa baadala ya kukwepa hoja na kuishi kihisia kwa kufukuzana fukuzana.
Huwezi ukatofautiana kimawazo na mtoto wako au rafiki yako na suruhu ikawa ni kuachana urafiki,au kumkana mtoto.
 
Mh. Machali alisema hapo Star Tv wiki ilopita Kuwa hoja hizo za Kumshinikiza Mbatia kufungua Kesi dhidi ya Mh.Mdee ulizitoa kwenye mikutano yenu ka Halmashauri kuu. inakuwaje hiv sasa unakana kwamba hazikuwa hoja zako?

Swali la Pili: tatizo lilikufukuzisha Chadema zinafanana na Hizi zilikufukuzisha NCCR-Mageuzi?
 
Kafulila, hivi ni kweli wewe ndiye nguzo ya NCCR mageuzi kule Kigoma? Wewe eti ndiye uliyempa Machali ubunge na sasa ameota mapembe?
 
kafulila kwanini ulitaka kufanya mkutano na chama kingine wakati wewe bado upo nccr mageuzi? polisi wasingekukataza ungepanda kwenye jukwaa la chama kingine cha siasa?
 
Nitoe shukrani zetu za dhati kwa wachangiaji wote jamiiforumns kwa michango yenu na busara zenu. Mmeendelea kuwa msaada na nyenzo muhimu kuboresha mijadala yetu kila JUMAPILI.
Fukuyama JUMAPILI ijayo katika muendelezo wa mijadala hii.
Ahsanteni na JUMAPILI njema
 
naona bwana kafulila ame-apply kikamilifu ile dhana maarufu inayosema kwamba "denial is the best defence" ; sidhani kama tutapata ukweli kwa utaratibu huu unless pande zote mbili zinazopingana ziletwe mezani pamoja na evidence ya tuhuma au utetezi wao
 
Nimefatilia mtanange huu wa David kafulila on star tv mwanzo hadi mwisho....nafikiri Kafulila anapoint kiasi fulani....
na inaonyesha huyu jamaa ni hazina kubwa sana kwenye siasa za Tanzania ila chama alichokwenda hakiendani na yeye.
Ningewashahuri viongozi wa Chadema wamtafute huyu jamaa na waongeenae na ikiwezekana ajiunge na CDM as soon
as he can! ....kwani kwa sasa CDM ndicho chama kilichobeba matumaini ya watanzania na ndicho chama makini kwa sasa.
Big up Kafulila!
 
kafulila anafurahisha genge!!!nashindwa kumuelewa huyu kijana toka alivyoside na HR kuzuia cdm wasiongoze oversite commitee za bunge hali akijua cuf =ccm:lol: na njia pekee ya kuwa na oversite yenye meno ni lazima ziongozwe na chama ambacho kimedhamilia kweli kuleta mabadiliko(cdm),:shock:nasita sana kumkubali huyu kijana inaonekana anaweza kuwa tempted kirahisi sana hana msimamo kabisa ni kigeugeu
 
Kumbukeni vyama vyote viongozi hawapendi kukosolewa. Chacha wangwe wa chadema alipohoji matumizi ya pesa (chadema) yaliyomkuta mnayajua.
Hashimu rungwe alionywa na mbatia katika kampeni za uraisi asikishambulie chama cha ccm. Huyo(mbatia) ni mpinzani?. Kafulila hawezi siasa za woga ndio maana anatimuliwa.
 
huyu dogo tangu alipopiga magoti na kushinda anaomba na kulia asivulie ubunge wala sitaki kusikia habari zake tena hana cha kutueleza maana kama alipopiga magoti akasamehewa akafunga mdomo sasa kwa kuwa ametimuliwa anabwawaja tu!!
 
Yahya,
Hongera kwa kipindi kizuri lakini huku kwetu Mugumu hatuwapati kabisa, rekebisheni kama kuna tatizo mzee........
 
Swali kwa Kafulila, NCCR Mageuzi, wakikusamehe upo radhi kurudi?
ritz, Rejao, Faiza Fox,mafiriri, Pasco .....................mkifukuzwa usalama wa CCM mtakuwa radhi kuirudishia TANU uhai wake?
 
Yahya,
Hongera kwa kipindi kizuri lakini huku kwetu Mugumu hatuwapati kabisa, rekebisheni kama kuna tatizo mzee........

Sasa na wewe Bukanga huko Mugumu siutoke uwaachie wenyewe wagumu! Karibu hapa Bukanga, tunanasa bila mawimbi. lol
 
Ndugu Yahya hii ni njia nzuri ya kuwafanya wadau wachangie na kuchambua hatima ya wabunge vijana kwenye mfumo wa siasa.Nionavyo mimi, ni vema StarTv at some point mkawaleta wazee (wanasiasa wasio-mahafidhina) na vijana - wenye mwamko wa kisiasa -sio wana wenye jaziba,wenye kutulia na kuona mambo kwa upana zaidi. Kisha tuwe na mjadala kuhusu siasa. Nionavyo mimi kuna mgongano wa vizazi kwa hiyo ni zaidi ya madaraka. Suala la Kafulila ningependa lipanuliwe zaidi badala ya kuwa la NCCR nipewe mtazamo wa kikatiba zaidi. Kwa hali ilivyo sasa tutakuwa tunamhoji Kafulila, lakini take it from me, hakuna ambako atakwenda na kusafishwa endapo chama kimemfukuza! Hivyo hata kama Bunge na Mahakama wangemwambia aendelee kuwakilisha wananchi wa jimbo lake, katiba ya sasa haitambui mbunge/mwakilishi binanafsi. Hivyo mjadala ningependa uvuke NCCR/CUF uende zaidi kwa kuhusisha watu wengine. Nina imani wakati mwingine mawazo haya mtayafanyia kazi, vijana na wazee kwenye mjadala wa pamoja na pia mjadala wa kikatiba kuhusu mgombea binafsi na hatima ya uwakilishi endapo chama kimemfukuza uanachama mwakilishi wa wananchi
Habari za JUMAPILI wanaforum,
Tumefanya mabadiliko kidogo katika muendelezo wa vipindi hivi kujadili na kusaidia kutanzua Migogoro ya kisiasa NCHINI na wimbi hili la fukuzafukuza. Badala ya kuwa kwa pamoja David Kafulila na Moses Machali Leo, tumeonelea ni vela haki waliyoipata Vongozi tu ilkuwa nao JUMAPILI iliyopita, anastahili ndugu Kafulila pia ili KUTOA wigo mpana kwa watanzania kujadili vema na kupendekeza njia mbadala kupitia media.

Kafulila atazungumza na watanzania mud a si mrefu, Maswali tuliyoyahifadhi wiki iliyopita tu Shari za hadi JUMAPILI ijayo tukifanikiwa kuwaweka meza Moja pande zote mbili.

Karibuni katika mjadala
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom