David Jairo wa IKULU

Aliyekuwa Katibu wa Rais Bwana David Jairo ambaye wiki iliyopita amechaguliwa kuwa Katibu mkuu wa wizara ya Nishati na Madini amekuwa akimtisha Mbunge wa Ilala Mussa Azzan maarufu kama Zungu ambaye ni mwenyekiti wa kamati inayoshughulikia majengo ya Machinga Complex.

Jairo anataka apewe kazi ya zabuni ya matangazo kwenye majengo hayo bila kufuata taratibu zinahusika.

David Jairo alipotakiwa kufuata taratibu kwa kampuni yake kuomba tenda kama kampuni nyingine amekuwa mbishi na kumtisha Zungu kuwa yeye(jAIRO) ni mtu wa karibu sana wa RAIS JK hivyo kama atakosa basi Zungu ajue kuwa kakalia kuti kavu.

Maswali kwa David Jairo kwani hajui kuwa IKULU Iko jimbo la Ilala ambako Zungu ni mbunge? Zungu ni mbunge wa Rais.

Na kama rais ana jambo lake atawasiliana na Zungu moja kwa moja sio wewe Jairo.

Zungu kachaguliwa na wananchi sio wewe Jairo,lakini lazima uelewe kuwa Majengo haya ni ya wamachinga wewe Jairo unataka nini? kwani wewe ni mmachinga?

Mheshimiwa Rais Mtizame kwa macho mawili Jairo anatumia vibaya jina lako.wewe ni rais wa watanzania wote wanaoweza kutuzidi kimapenzi kwako ni familia yako na watu wa jimbo lako la Chalinze walitupa fursa ya kukupata.kwani bila wao kukuchagua kama mbunge wao sisi kama watanzania tusingeweza kufaidika na uwezo wako.

Kama JAIRO anawatisha watu kwa vitangazo vya Machinga Complex na sasa umempeleka Madini na Nishati ikitokea dili za Richmond anaweza kuwa na roho ngumu na kutenda haki?

Shame on you Jairo.
 
zungu hawezi kutishiwa na jairo...si ndio SAIGON wenyewe hao,?

kama ni hayo majengo ya machinga yamejaa madudu kibao kibao....na hata huyo zunngu mwenyewe amejigawia yeye na anataka kuutumia majengo ya machinga kama mtaji wa kisiasa kwa kuwapa kipaumbele vijana wake wanaomfanyia kampeni[anamuogopa spfia simba],ndo maana haachi kuuza sura hata asikohusika .

si vema jf ikatumika kuendeleza chuki binafi dhidi ya mtu........kama walivojigawia maduka ya benjamin mkapa school,ubungo station ambako vigogo wote walipata..ndio wanavyogombea the so called machinga complex............
 
sana sana iejulikana kuwa zungu ni miongoni mwa wanaosambaza maneno dhidi ya jairo.....lakini hadi hapo tutapojuwa chanzo cha ugomvi wao ndo tutadandia gari lao...
 
Hapa kuna hoja tofauti na sio tenda ya majengo maana wakuu hawa kwa wamama balaa,labda wamegongana sehemu.
 
si tu kuna ajenda binafsi kati ya zungu na jairo bali mleta mada kuna kila dalili ana ajenda binafsi......!
This is JF bwana.....!
 
Kanda2, kama unampenda Zungu mwambie atulize boli.
Ugomvi wake na Jairo inaelekea ni personal.Tenda za jengo la Machinga haiwezi kuwa sababu.
Watu wana mikanda vilevile ya Zungu na miradi inayoendelea jijini Dsm, ikitolewa hadharani patakuwa hapatoshi.
Kanda2 wakutanishe hao wakanywe chai pamoja
 
Yaani Kanda 2 ametufanya sisi mazoba kweli! yaani unaibuka na kisirani chako na kukileta hapa bila hata ya source yoyote! mie nilifikiri Zungu kalalamika sehemu kumbe wewe unaongelea umbea tu! Acha kuiharibu JF ungekuwa na hoja ungejipanga ukaileta
 
Sakata la matangazo ya jengo la Machinga Complex. David Jairo analazimisha kampuni yake ipewe Tenda.
 
David Jairo ni katibu mkuu wa nishati na madini kabla ya appointment hiyo alikuwa msaidizi wa Rais JK.ana kampuni yake ambayo anataka ipewe tenda ya Matangazo kwenye jengo la Machinga Complex. Mwenyekiti wa mradi huo ni mbunge wa Ilala mheshimiwa Zungu.alipotakiwa Jairo afuate utaratibu wa kampuni yake kuomba tenda kama kampuni nyingine. Jairo akaanza kumtisha Zungu kuwa yeye ni mtu wa IKULU. jAIRO KASHINDWA KUELEWA KUWA ZUNGU NI MBUNGE WA IKULU KWANI ILALA IKO ILIKO IKULU.
jAIRO DILI NDOGO ZA MATANGAZO ZINAKUTOA ROHO UNAWEZA KUVUMILIA RUSHWA ZA RICHMOND HUKO MADINI?
 
Ni nani huyo? David Jairo!!!

achana nao yeye na zungu [mzee wa ku supply hewa]..a.k.a IBSON..wamekazian basi ishakuwa tabu ...

LETENI ishu za maana tukate....hapa ..haya kama ni huyo jairo ukitupa nondo za maana tunampiga nyundo..tatizo nondo zako hazina uzitoo...mwambie huyoo retired.coplo.zungu [form four leaver..tunajuwa hajuwi kutumia compyuta ndio maana amekutuma]...
mwakani mutoto wa mujini Sophia anamsubiri...nadhani kishapata kiwewe...
 
Sasa hili jasusi limepelekwa kufanya nini hapo nishati na maadini?
 
jairo ndio huyooooo

8D6U2462.JPG

http://2.bp.blogspot.com/_HO8ijU76ZcQ/St8DMdRn4yI/AAAAAAAAyxg/hCnchh4xLX8/s1600-h/8D6U2462.JPG
 
JK ni Saigon, Zungu ni Sagon pia na Iddi Simba alikuwa Saigon. Jairo sio mwanamtandao wa JK, bali ma close pals, sasa inapokuja mgongano wa kimaslahi kati ya Saigoni na ma pals, JK atakumbatia ma pals kwa sababu Saigon haina nguvu tena kama ilizokuwa nazo, kama Simba aliangunguka, itakuwa Zungu, mtaji pekee wa Zungu Ilala yeye ni mtu wa watu, Simba aliwategemea sana wapambe, Zungu ni mwenyewe mpambe.

Hiki kilio cha Zungu dhidi ya Jairo, ni dalili ya mfamaji na hakitamsaidia Zungu, sana sana kitatifua tuu maroroso yote ya Machinga Complex ambayo Zungu ndiye main player. Masikini wamachinga, hilo jengo lao, wao wataishia kuliona kwa macho tuu.
 
JK ni Saigon, Zungu ni Sagon pia na Iddi Simba alikuwa Saigon. Jairo sio mwanamtandao wa JK, bali ma close pals, sasa inapokuja mgongano wa kimaslahi kati ya Saigoni na ma pals, JK atakumbatia ma pals kwa sababu Saigon haina nguvu tena kama ilizokuwa nazo, kama Simba aliangunguka, itakuwa Zungu, mtaji pekee wa Zungu Ilala yeye ni mtu wa watu, Simba aliwategemea sana wapambe, Zungu ni mwenyewe mpambe.

Hiki kilio cha Zungu dhidi ya Jairo, ni dalili ya mfamaji na hakitamsaidia Zungu, sana sana kitatifua tuu maroroso yote ya Machinga Complex ambayo Zungu ndiye main player. Masikini wamachinga, hilo jengo lao, wao wataishia kuliona kwa macho tuu.
sasa nani msafi?
 
Back
Top Bottom