kaka siasa tu, kigamboni kuna nini cha kumvutia mtalii? Yaani bado tunaishi kwa ndoto? Nani siku hizi akujengee mji ndugu yangu? Trilion 13 zinahitajika kama ukikuwa hujui ili kukamisha huo mji serikali yako inazo?
Jibu zuri sana BIG up kaka nadhani mleta mada atakuwa amekuelewa na kufunguka macho naomba tufunge mjadala.
Jibu zuri sana BIG up kaka nadhani mleta mada atakuwa amekuelewa na kufunguka macho naomba tufunge mjadala.
yote yana umuhimu wa kipekee na hayashirikiani ila cha kutazama kwanza kinatakiwa kiwe wapi kuna shida zaidi au wapi wanateseka zaidi na uchumi na shughuli za kijamii unaathirika kwa kiasi gani. We inalinganisha daraja la kigamboni na reli hebu linganishana kujenga kiwanja cha ndege kikubwa pale msalato dodoma kwa sasa kama kuna mahitaji muhimu lukilinganisha na reli ya kati.hivi vyote ni muhimu kwa maeneo yake, lakini kama unataka kipaumbele kati ya vitu hivyo, hakuna ubishi kuwa kuimarisha reli ya kati inazidi umuhimu wa kujenga daraja la kigamboni. Lakini hiyo haimaanishi kuwa daraja la kigamboni si muhimu.
Tatizo lipo miongoni mwa wanaofanya maamuzi. Tungeweza kuimarisha reli ili ituletee fedha za kutosha kuweza kujenga si tu daraja la kigamboni, bali na madaraja mengine pia. Sidhani kama daraja la kigamboni linaweza kuzalisha fedha za kutosha kuimarisha reli ya kati
Zote ni huduma kwa jamii na zipo sawa kabisa pasi na moja kuwa juu ya nyengine bali inategemea vipaumbele vya Serikali katika kutoa huduma kwa jamii ya watu wake.