armanisankara
JF-Expert Member
- Jul 15, 2011
- 283
- 49
Taasisi ya utafiti na kuibua matatizo yanayowakabili wakazi wa Jiji la Dar es Salaam (Sikiliza) imebaini kwamba jiji hilo limekithiri kwa rushwa, vurugu, pamoja na wizi kwa asilimia 55.
Akitoa tathmini hiyo jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Sikiliza, William Kihula, alisema mambo hayo yanaendelea kukua kwa kasi jijini humo.
Alisema sehemu kubwa ya matokeo ya utafiti huo, inaonyesha kuwa kati ya matukio manne yaliyokithiri, ni ya rushwa, ambayo yanasababishwa na askari wa usalama barabarani.
Pia alisema utafiti huo umebaini kuwa sio tu kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri wa barabarani, bali hata kwa wasiomiliki.
Kihula alisema wizi na vurugu ni miongoni mwa aina za uhalifu wa mara kwa mara unaoathiri maisha ya mamilioni ya wakazi wa jiji hilo.
SOURCE: NIPASHE