Dar Lux Bus jifunzeni ustaarabu

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
12,037
24,595
Kuna thread ilianzishwa, ilikuwa ikizungumzia kuhusu ujio wa mabasi ya Dar Lux Bus.
Mabasi haya yameshaanza kazi rasmi, mara baada ya kuanza route zao niliamua kutumia usafiri huo to different destinations.
Magari ni mazuri na ya kisasa ila Katika safari zote mbili nilizofanya ilikuwa ni kero sana, wafanyakazi wake ni kamapo kijiweni hivi, kwa tabia yao ionyeshayo kuwa wapo unorganised,
kero kubwa ni sauti ya radio humo ndani, huwa ya juu muda wote utadhani umepanda matatuu, huwez hata kusikiliza simu , wala kusikiliza muziki kwa earphone zako, ukiwaomba kupunguza sauti huishia kukuzungusha tu na kutoa majibu yasiyoeleweka.
Ukiwaangalia wafanyakazi wenyewe ni kama kila mmoja anajihisi ni boss wa mwingine, hawa ethics za kazi zao, labda hawazijui.
Naiona kama kampuni iliyopo mbioni kufa mapema.
Badilikeni.
 
Si nasikia hayo mabasi ni ya mtoto wa mkuu wa magogoni? Labda wafanyakazi nao wanajihisi ni watoto wa mkuu wa magogoni!! LOL

Suala la customer care kwa wafanyakazi na wafanyabiashara wabongo in particular wamatumbi ni tatizo kubwa sana, na usije kushangaa baada ya muda mfupi unasikia kampuni ya dar lux bus iko ICU.
 
ndo matatizo ya kuanzisha kampuni/biashara na kutizama faida bila kujali unayemhudumia. mmiliki alipaswa kuwapa ka-training cha customer care, kuwafundisha ustaarabu na jinsi ya kuhudumia wateja kutokana na standard zanazotaka.
ndio maana dar express ndo the best hata wakimfanyia majungu
 
Ah! Hao si wanatafuta cheap labor wale wakwere wa chalinze kule hata vidato hakuna usitegemee jipya ni uswazi kwa kwenda mbele.
 
Tatizo la wafanyikazi wa mabasi ni kuwa wanarotate walewale... Ukimfukuza huku anaajiriwa pale, kwa hiyo hakuna jipya analojifunza hapo...
Hivi abiria hamwezi kufanya kama mimi nilivyomfanyia kondakta wa Dar Express?
 
Twambie mkuu ulimfanyia nini huyo konda ili tuone kama kuna la kujifunza au .......
 
Kuna thread ilianzishwa, ilikuwa ikizungumzia kuhusu ujio wa mabasi ya Dar Lux Bus.
Mabasi haya yameshaanza kazi rasmi, mara baada ya kuanza route zao niliamua kutumia usafiri huo to different destinations.
Magari ni mazuri na ya kisasa ila Katika safari zote mbili nilizofanya ilikuwa ni kero sana, wafanyakazi wake ni kamapo kijiweni hivi, kwa tabia yao ionyeshayo kuwa wapo unorganised,
kero kubwa ni sauti ya radio humo ndani, huwa ya juu muda wote utadhani umepanda matatuu, huwez hata kusikiliza simu , wala kusikiliza muziki kwa earphone zako, ukiwaomba kupunguza sauti huishia kukuzungusha tu na kutoa majibu yasiyoeleweka.
Ukiwaangalia wafanyakazi wenyewe ni kama kila mmoja anajihisi ni boss wa mwingine, hawa ethics za kazi zao, labda hawazijui.
Naiona kama kampuni iliyopo mbioni kufa mapema.
Badilikeni.

Mkuu tumia mabasi ya GOMBE Bus, Ni mapya, safi, Nidhamu ya kumwaga...au Green Star hutakerekwa na wahudumu
 
nilipanda moja wakati wa hizi mvua nyingi za juzi juzi,
kondakta ana bonge la kitambi,
wanafanyakazi wanavyotaka wao,
jamaa anaomba wachukueni hao abiria walioko njiani
jamaa anasema msinipangie kazi,
kweli yana boa,
inawezekana kuna mkono wa mtu mkubwa.
 
Twambie mkuu ulimfanyia nini huyo konda ili tuone kama kuna la kujifunza au .......

konda alikuwa analeta jeuri, kwanza hakutupa soda zetu mpaka tunaenda kula Highway Korogwe...
Alipokuja kugawa maji, akawapa watu wachache wa viti vya mbele then akadai yamekwisha, mimi nikachukulia poa kabisa... Cha ajabu akaenda siti za nyuma akawakuta masela zake, si akaenda mbele kuwachukulia maji? Nilipomuuliza huyo kondakta akaniambia kuwa pale sio gesti, hivyo natakiwa niwe mpole...
Tulipofika pale Same, alipoingia yule mdingi mkaguzi, nikamchana live kila kitu... Akamwita nje, akamsema kama mtoto mdogo, jamaa akadai kama tatizo ni maji anaenda kunichukulia kwenye buti ya gari... Mkulu akamwambia kama maji yameisha, hayo anayotaka kunipa yanatoka'pi?
Msela akanichukia mpaka mwisho wa safari...
Nikajiona shujaa mwenyewe?
 
Hii kampuni imeshakufa miguu juu mmiliki wa hizi basi alikuwa bwana mdogo mmoja hivi sijui alizibamba wapi hela basi akakimbilia kuanzisha ofisi ya kisasa pale UBUNGO OILCOM na UBUNGO PLAZA akaenda VODA akapewa CODE ya M-PESA kwa abiria kulipia tiketi kwa M-PESA basi ile anakuja kuanzisha biashara rasmi hakuchukua hata miezi 3 chali. Biashara za mabasi Tanzania zinataka upate uzoefu kwanza na uende na jinsi wananchi wanavyotaka. kimsingi watanzania wengi hawapendi huduma safi safi sijui mabasi, ofisi safi, sijui kulipia Tiketi kwa M-PESA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom