Dar is set for Ruhudji hydropower station

Hili ni suala la collective responsibility. Wananchi nao wanatakiwa kupunguza uzazi. Na vilevile kuangalia matumizi ya NUKE. Lazima nchi iwe na source mbalimbali.
 
....Hili ni suala la collective responsibility. Wananchi nao wanatakiwa kupunguza uzazi....

Kaka,
hii itakuwa ngumu kiasi kwa maeneo ya Tanzania vijijini ambako watoto ni sehemu ya nguvukazi katika uzalishaji mali. Tuwaongezee elumi ya uzazi wa mpango, ingawa hii inachukua muda mrefu matokeo yake kuonekana.

Kwa mjini inawezekana kabisa kupunguza kuzaana, staili ya maisha ni justification tosha ya suala hili.


.... Na vilevile kuangalia matumizi ya NUKE. ...

Suala la nyuklia kwa mpango wa nishati wa muda mfupi na wa kati sishauri kabisa, litatuletea maafa sana. Sisi ni wazembe na hatuwajibiki. Kama tumeshindwa kuzima moto wa kawaida kabisa hapa mijini (penye miundombinu ya kuzimia moto) hadi nyumba zinateketea, itakuwaje kwa kinu cha nyuklia kikivuja? Ningependa suala la nyuklia liwe ni mpango wa muda mrefu (30 years and beyond). Tusije tukawa tunakaribisha Chernobyl ya kujitakia.

... Lazima nchi iwe na source mbalimbali...

Ni kweli, nakuunga mkono, ila sio nyuklia.
Vyanzo vingine mwafaka kwa hapa kwetu kabla ya kukimbilia katika nyuklia viwe ni hivi:-

1. Gesi asilia (tunayo kiasi cha meta za ujazo giga 45
2. Umeme wa nguvu ya upepo
3. Umeme wa nguvu ya jua
4. Umeme wa nguvu ya maji (bado tuna vyanzo vingi vidogo vya nishati hii
5. Umeme utokanao na makaa (kwa njia za kisasa zisizoharibu mazingira
6. Umeme wa mawimbi ya bahari
nk.

Slide 6 .O {color:#40458C; font-size:149%;} a:link {color:#6F89F7 !important;} a:active {color:#B2B2B2 !important;} a:visited {color:#CFDBFD !important;}
 
Tanesco na Wizara ina wahandisi wazuri ambao nina uhakika wana uwezo wa kufikiri zaidi yetu sisi wa kuropoka kwenye mitandao.

Kuzalisha MW 358 kwa kutumia upepo na uweze kuhifadhi huo umeme ambao unapatikana kipindi fulani alafu kipindi fulani unapungua sio jambo rahisi.

Kuongeee tu.... lakini tujue kwamba kuna wenzetu wanafanya hizi kazi wako gado zaidi yetu...
Nafikiri ingekuwa busara pia kuanza investment kwenye renewable energy. Na hawa wahandisi walio makini Tanesco na kwingine wakawa mstari wa mbele katika kuwezesha hilo. Hydro power plant, kama ilivyo kwa renewable energy nazo zina limitation. Mara nyingi ili kuwa safe, diversification inakuwa kitu kizuri zaidi.
By the way hata humu jamvini kuna wahandisi na fani nyingine pia, ingawa siasa zinawashabiki wengi zaidi
 
Hivi hatujajifunza kutokana na makosa ya Kidatu, Nyumba ya Mungu na Mtera?

Kwa nini hatuelekezi kwenye nguvu za nishati kutumia Upepo na Jua ambazo gharama za muda mrefu si kubwa kama kilichotokea kutokana na mabwawa ya maji ambayo yamejaa tope na kukosa maji kutokana na ukame?

Mzee tuna Uranium na Makaa ya mawe kwanini tusitumie kuzalisha umeme wetu!!?...ama mpaka waje wajanja tuingie mikataba ile ya kina Sultani Mangungo?
 
Tanesco na Wizara ina wahandisi wazuri ambao nina uhakika wana uwezo wa kufikiri zaidi yetu sisi wa kuropoka kwenye mitandao.

Kuzalisha MW 358 kwa kutumia upepo na uweze kuhifadhi huo umeme ambao unapatikana kipindi fulani alafu kipindi fulani unapungua sio jambo rahisi.

Kuongeee tu.... lakini tujue kwamba kuna wenzetu wanafanya hizi kazi wako gado zaidi yetu...

Trusting experts is what got us where we are.

Kama una counteragruments kuhusu points zilizotolewa, zitoe.Siku hizi access to information is no big deal, kama unataka kufanya research karibu kila kitu kipo mtandaoni.
 
Umeme wa uhakika ni wa makaa ya mawe. Nchi nyingi zilizoendelea wametumia sana na wengine bado wanatumia kwa wingi zikiwemo Marekani, Australia, China etc na Wajerumani wanapanga kujenga mitambo zaidi ya kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe. Wazungu wamehamishia viwanda vyao vingi China kwasababu ya cheap labour na umeme wa uhakika.

Hivi sasa kuna teknolojia za kuweza kuyatumia makaa ya mawe in an environmental friendly manner kukwepa mambo ya climate change yanayosababishwa kwa kiasi kikubwa na gesi ya carbon dioxide ambayo huzalishwa kwa wingi zaidi na mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe.

Nafikiri makaa ya mawe tunayo reserve ya kutosha kwahiyo yatupasa tuelekeze nguvu zetu huko kama tunataka umeme wa uhakika na kuharakisha juhudi za kuleta maendeleo.
 
damn 350MW for 800m USD?....huo ni wizi wa mchana kabisa na hiyo project bora ife maana hii ni IPTL nyingine tuu naona,nafikiri 800m USD zinaweza kufanya mambo makubwa sana kwenye energy sector kuliko hizo 350MW,yaani nchi imejaa vilaza na wezi tuu!
 
Solution wawaachie watu binafsi wazalishe na wauze umeme sio hizi blah blah za serikali na TANESCO zinazotutia hasara za mabilioni kilna umeme wenyewe hakuna!
 
Solution wawaachie watu binafsi wazalishe na wauze umeme sio hizi blah blah za serikali na TANESCO zinazotutia hasara za mabilioni kilna umeme wenyewe hakuna!

Mkuu Koba uko sahihi kiaina.
Hii sheria ya Independent Power Producers (IPP) imekuja juzi juzi tu, baada ya kuona kuwa serikali haina uwezo wa kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya nishati.
Kimsingi inabidi nafasi wapewe wazalishaji binafsi, hapo ndipo tutakapoondokana na tatizo la baadhi ya mikoa kutokuwa na umeme wa gridi kwa karibu nusu karne nzima.
TANESCO inatakiwa wanunue umeme na kuwauzia walaji, wajiondoe katika suala la kuzalisha.
 
You people are not being reasonable. Sasa mnalalamika umeme unakatika mpaka muhimbili alafu mkitaka kujengewa Power station hamtaki.. lol.. Kula lazma watu wale lakini kiwe cha one time alafu tuwe na umeme wetu..
 
You people are not being reasonable. Sasa mnalalamika umeme unakatika mpaka muhimbili alafu mkitaka kujengewa Power station hamtaki.. lol.. Kula lazma watu wale lakini kiwe cha one time alafu tuwe na umeme wetu..


Suala sio kujengewa tu, halafu basi! Suala ni: Tunajenga kwa gharama gani?
 
Back
Top Bottom