Kweli? Wakati mheshimiwa anataka kuchimba mafuta mpaka mlangoni? Mchina mwaka jana kafungua bwawa la tatu kwa ukubwa duniani katika kuzalisha umeme. na la pili pia liko kwake na karibia kuanza kazi.
Ni ukweli tunahitaji kutanua vyanzo vyetu vya nishati na sio kutegemea sana mabwawa. Lakini study zinaonyesha "...the trend in both Canada and the United States has been to micro hydro because it has negligible environmental impacts and opens up many more locations for power generation...".
Kama tuna maporomoko tuyatumie vizuri. Tatizo hapa ni namna gani ya kufanya hii miradi iwe ya faida kwa kizazi chetu na cha baadae. Hapo mimi ndio naona lipo tatizo.
View attachment 2207
Tukumbuke na maji (hydro) ni kati ya renewable source of energy.
Wakuu,
Hii Ruhudji ni wapi...
Tanesco na Wizara ina wahandisi wazuri ambao nina uhakika wana uwezo wa kufikiri zaidi yetu sisi wa kuropoka kwenye mitandao.
Kuzalisha MW 358 kwa kutumia upepo na uweze kuhifadhi huo umeme ambao unapatikana kipindi fulani alafu kipindi fulani unapungua sio jambo rahisi.
Kuongeee tu.... lakini tujue kwamba kuna wenzetu wanafanya hizi kazi wako gado zaidi yetu...
Kutikisika kwa uchumi wa dunia kutokana na matumizi ya mafuta, mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yamesababisha ama kutokuwepo kwa mvua za kutosha au nyingi kupita kias, ndiko kunakofanya watu wafanye tathmini ya kutafuta source alternative za nishati.
Kwa nchi masikini kama Tanzania, ni muhimu tukiwa mstari wa mbele kwenye hii "green energy revolution innitiative" kwa kuwa tuna maeneo makubwa sana ambayo yatanufaika na kutupunguzia gharama.
Just imagine kama waki-demonopolize Tanesco na kuruhusu local authority kujitegemea kwa nishati.
Umeme wa Kidatu na Mtera unapita Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga na hautoshelezi wala kufikia wananchi katika vijiji hata mail tatu nje ya makao makuu ya mkoa au wilaya.
Sasa kwanini sisi ambao tunataka maendeleo na nishati ya umeme ndio kitu kikubwa kutusaidia tusitumie nguvu zetu kutumia njia rahisi za kuzalisha umeme na zenye gharama nafuu?
Kuna mtu kauliza kwa nini tusinunue mitambo ya kutumia gesi kumi ili tuwe na umeme wa kutosha na kuachana na mabwawa ambayo yametushinda kutokana na kushindwa kuyatunza, mvua ndogo kutokana na ukame ambao unatokana na kukatwa kwa miti ovyo?
Sikatai it is great to have hydropower lakin experience yetu ya Mtera, Kidatu na Nyumba ya Mungu zinatuonyesha kuwa hatuna uwezo wa kutunza hayo mabwawa yakishajengwa na ni kutokana na kuharibika kwa mabwawa au kupungua maji kulikotupeleka kukimbilia umeme wa ziada na dharura ambao umehujumu uchumi wa nchi kama IPTL na Richmond!
Huu ni wizi mkubwa sana, Richmond Saga.
Kwa nini wasinunue Turbine 20 za MW 100 kila moja tungeweza kupata MW 2000 (ELFU MBILI) badala ya MW 358. Na gharama ya MW 100 ni sawa na $40 million. ambazo zinatumia gesi asilia ya hapa Tanzania. Pia tungeweza kuuza umeme mwingi sana nje na kurudisha gharama zetu.
Majizi wakubwa hawa.
......tunaomba kasheshe na wahandisi wake makini waje hapa wajibu hilo swali la kokolo,gas turbine ni cheap na gas yetu wenyewe kibao mpaka hatuwezi kuitumia lakini sijui mambo kama haya hawafikirii...10% ni sumu wakuu,lakini at the end of the day lazima focus yetu iende kwenye wind & solar power maana ndio the next frontier in energy na ndio itatuokoa kwenye haya matatizo ya nishati chanzo number one wa umaskini na ufukara wetu
Ukiiitia rioti ya Mwakyembe on Richmond utakubali anachosema Kasheshe ni sahihi kabisa. Wataalam wa Tanesco waliikataa Richmond kabisa lakini masinikizo ya wakubwa (you should know who by now) ndio yaliyopelekea mambo kwenda mrama.
Huko wizarani kuna malundo ya maripoti kuhusu nishati m-badala lakini hakuna mtekelezaji
Hivi mnajua ni kwa nini Solar na Wind Power zimechukua muda kukubalika katika nchi zilizoendelea? It is not about science, but politics, lobbying and dirty games through Capitalism.
Ni sawa na madawa ya Ukimwi, wanabana kutoa techknowhow kwa ajili ya kulinda faida.
Leo hii Marekani, makampuni ya mafuta yanatoa hongo kwa Serikali na Bunge kuzuia miswaada ya kuleta nishati safi inayopunguza carbon au kupunguza dependency ya mafuta. hata kuongeza kwa fuel efficieny ya magari imechukua muda na ni hili wimbi la kuongezeka kwa bei za mafuta mpaka Marekani tukaanza kununua chakula kwa resheni, ndipo Wanasiasa wa Marekani wamekubali msukumo kuleta energy efficient policies kwa wanotengeneza magari. Lakini this is after Exxon mobile kutangaza faida marudufu!
Leo hii third world mkianza kutumia nishati ya Jua na Umeme ambayo ni rahisi baada ya ile initial cost, woga wa nchi za magharibi ni kuwa Mnaoitwa Masikini mtaanza kujiendeleza na mtakuwa tishio!
Hivyo IMF, WB wataendelea kutushinikiza tujenge mitambo ambayo tutakimbila kwao kuomba misaada ya kutengeneza na kununua mitambo mipya huku tukiendelea kukopa kununua mafuta na mitambo!
Nafikiri tungefanya research kwanza kabla ya kutoa contribution. Mtu anayefikiria kuwa mahitaji ya Tanzania ya umeme yanaweza kuwa satisfied kwa kutumia solar and wind power naamini haelewi anachosema. While solar and wind power can contribute small amounts of power at different times of the day to the power grid they cannot however be the solution- hata huko scandinavia au uingereza ambako wana uwezo wa kitechnologia mkubwa sana kuliko sisi hili haliwezekani.
Sasa hivi nafikiri TZ tuna generate a total of about 500MW toka hydro [Kidatu;Mtera; Kihansi; Pangani na Nyumba ya Mungu]. Toka gas nafikiri capacity yetu sasa imefikia au itafikia by end of 2008 to 400 MW. Linganisha hii na Uganda Nile 250MW wanaongeza hili kwa kujenga Bujagali yenye another 250MW; Zambia & Zimbabwe huko Kariba about 700 MW.
Kwa hiyo nafikiri hio programme ya Ruhudji ni timely provided inatekelezwa bila ufisadi. Mradi wenyewe unaelekea ni mkubwa at over 380 MW compared to Kidatu about 100MW; Mtera 80MW; and Kihansi 180 MW. Swala kwangu ni sijui haya maporomko ya Ruhudji yapo mto gani na Mkoa gani? Kuna mwana JF anayeweza kunielimisha kwa hili - samahani nimekuwa nje ya Bongo kwa muda sasa.
Ruhudji Hydro Power Project
- This buyer is a part of the Songo Songo Gas Development Project.
Ruhudji Hydro Power Project operates in Tanzania.
The Ruhudji hydropower project will be designed with the capacity of 358 MW to generate 2000 Gwh of electricity per annum. The Ruhudji hydropower project will be located on the Ruhudji River and the Project Cost is estimated to be in the region of USD 700-800 million. The projects financial closure is projected to be achieved within 3 years as a public-private partnership (PPP).
.......
Kwa nini hatuelekezi kwenye nguvu za nishati kutumia Upepo na Jua ambazo gharama za muda mrefu si kubwa kama kilichotokea kutokana na mabwawa ya maji ambayo yamejaa tope na kukosa maji kutokana na ukame?
Mkandara,
Right on the money! Tuanze kwa kuangalia ni nini mahitaji yetu ndipo tuanze sambaa.
Tayari kuna project ya umeme Singida na Dodoma kutumia nguvu za upepo na wanasema itakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 50 na kutosheleza Singida na Dodoma hata gridi ya Taifa kwa 10%
Wakuu,
Hii Ruhudji ni wapi...
Ipo mkoani Kagera
Huu mradi wa Ruhudji, kwa mujibu wa ripoti ya Bw Leonard Kassana (2007) inatarajiwa kuanza mwaka 2012. Na kwa uzoefu wangu wa miradi ya hydro huu mradi utakamilika si chini ya miaka mitano tangu kuanza kwake. Afadhali kama tungeanza na mradi wa umeme wa gesi!
Hii miradi ya upepo nayo haiko salama kiasi hicho, ingawa inapigiwa chapuo sana. Wind projects ziko subject na noise, visibility problems na masuala mengine ya kimazingira, ikiwemo kuharibu madhari ya eneo husika.
Hali kadhalika, kuhusu ufisadi, huku nako RA na Mwakyembe washaanza kupigna vikumbo asubuhi subuhi. Si kwema sana.
That is mere politics. Tungeanza na upanuzi wa miradi ya umeme wa gesi, ambayo tunayo ya kutosha kule Mnazi bay na Songosongo
Somethings is coming over this project... Keep your eye on this topic