Dar Express #T844 BDR la Nairobi to Dar es salaam 23/10/2012 kidogo lituuwe

Watu

JF-Expert Member
May 12, 2008
3,231
1,470
Asilimia kubwa ya chanzo cha Ajali ni uzembe wa dereva na wahusika wa wa Basi lenyewe, tulijaribu kuwapigia simu maajenti wa Arusha wakasema kama ni Gari ya Robert (driver) huo ndio mwendo wake na wakenya ndio maana wanaipenda. Tuliriport kwa Inspector wao wa Same akamuonya ila baada ya kutoka Korogwe speed iliendelea na hatimae alipofika Mkata likatokea la kutokea na tulipowajulisha maajenti wa Arusha walichouliza kwanza ni kama gari lao limeumia sana badala ya kuuliza hali ya wateja wao. Huu ni mwanzo wa mwisho wa enzi ya Dar Express wanaandaa kaburi lao soon,siku chache zilizopita Benzi lao liliteketea lote kwa MOTO na mengine kila siku yanafia njiani,uzembe wa madereva na huduma hafifu ndani ya gari na mengineyo meengi ndio mwanzo wa mwisho wao

Photo0118.jpg

Photo0119.jpg

Photo0121.jpg

Hiace baada ya kugongwa na kurushwa zaidi ya mt tano na Dar express #T844 BDR

Photo0120.jpg

Dereva wa hiace Iliyogongwa hoi
 
dar express ni basi zuri sana,hiyo ajali apo ni kawaida kama nyingine,bus zote uwa zinakimbia ni kuwa mwangalifu tu,uwezi jua labda uyo dereva apo ndio mzembe
 
Hiyo hiace ilikuwa inafanya nini huko? Yeye hakuona kama kuna gari inakuja? Akasubiri mpaka agongwe aende polisi?
 
Kinachoiponza hii kampuni ni management yake mbovu-sijui ni kuzeeka kwa yule mzee?? siku hizi kuna mtei, kilimanjaro, nk waache wakishafulia kama akamba watajifunza
 
Hiyo hiace ilikuwa inafanya nini huko? Yeye hakuona kama kuna gari inakuja? Akasubiri mpaka agongwe aende polisi?

afterall hiyo bus ni ya masafa marefu ni lazima itembee ipasavyo!kama hutaki speed ungepanda royal au meridian
 
Hao jamaa limebaki jina tu.
Hata gari zao nyingi zimechoka mno, cha ajabu nauli bado juu. Halafu wanakwambia eti gari full AC wakati ndani kama incubator.
 
afterall hiyo bus ni ya masafa marefu ni lazima itembee ipasavyo!kama hutaki speed ungepanda royal au meridian
Mkuu hapo pekundu umekosea.
Meridian ndo gari zinazoenda sambamba na Ngorika zile mbaya mbaya na Chakito kwa kukimbia katika njia hiyo ya kaskazini.
 
Maximum speed ya barabara ya Arusha-Dar ni ngapi?

mi nakumbuka nilipanda hiyo dar express ya nairobi,dereva alikuwa anamaliza kiplate 120km/hr,akipunguza ni 100 au 110 lol!!marcopollo inalalamika saa 2 kasoro tunaitafuta nairobaa
 
Barabara za Tanzania zote maximum speed ni 80kph. Kwenda zaidi ya hapo ni kuvunja sheria.
Duh! Wengi wanavunja sheria hiyo! Ila nadhani kuna baadhi ya maeneo speed inafika 120kph, otherwise barabara hizi zimejengwa kwa malori na mabasi.
COURTESY Msome Mkeshaji naona unashangilia uvunjaji wa sheria!
mi nakumbuka nilipanda hiyo dar express ya nairobi,dereva alikuwa anamaliza kiplate 120km/hr,akipunguza ni 100 au 110 lol!!marcopollo inalalamika saa 2 kasoro tunaitafuta nairobaa
Kwa mara la kwanza kupanda basi nikaona likienda kwa spidi ya KM 120 kwa saa, ilikuwa katika miaka ya tisini mwanzoni. Safari ilikuwa ni kutoka Arusha kwenda Dar, basi Tawafiq (Nissan Diesel)..! Na Dereva mpaka leo namkumbuka! Akiitwa Onesmo! Nilihama kiti cha mbele..
 
Last edited by a moderator:
Barabara za Tanzania zote maximum speed ni 80kph. Kwenda zaidi ya hapo ni kuvunja sheria.

Sehemu za limit zinaonyeshwa na ni 50km/hr au 80km/hr..na zingine hakuna limit ni kukanyaga tu hivyo ni umakini wa driver na gari lake..
 
Asilimia kubwa ya chanzo cha Ajali ni uzembe wa dereva na wahusika wa wa Basi lenyewe, tulijaribu kuwapigia simu maajenti wa Arusha wakasema kama ni Gari ya Robert (driver) huo ndio mwendo wake na wakenya ndio maana wanaipenda. Tuliriport kwa Inspector wao wa Same akamuonya ila baada ya kutoka Korogwe speed iliendelea na hatimae alipofika Mkata likatokea la kutokea na tulipowajulisha maajenti wa Arusha walichouliza kwanza ni kama gari lao limeumia sana badala ya kuuliza hali ya wateja wao. Huu ni mwanzo wa mwisho wa enzi ya Dar Express wanaandaa kaburi lao soon,siku chache zilizopita Benzi lao liliteketea lote kwa MOTO na mengine kila siku yanafia njiani,uzembe wa madereva na huduma hafifu ndani ya gari na mengineyo meengi ndio mwanzo wa mwisho wao

View attachment 69176

View attachment 69177

View attachment 69179

Hiace baada ya kugongwa na kurushwa zaidi ya mt tano na Dar express #T844 BDR

View attachment 69178

Dereva wa hiace Iliyogongwa hoi
Umelichochea sana hili basi la Dar express kwani wewe ni competitor wa ruti hiyo nini. Kwa uzoefu wangu wa ruti nyingi za masafa marefu kama dar-nai lazima dreva awe na pressure ya kufika mapema na nimaranyingi wanapiga hiyo 120 na siye tunajuwa na tunataka kufika mapema. hiki ndo kitu pia kinatokea ruti ya dar-mbeya yani ni ligi kule na siye wenyewe abiria tunawaambia basi lako likichelewa kufika zaidi ya saa mbili sipandi tena. Sasa unategemea nini hapo lazima dreva aaaendeshe kiligi aweze kufika kabda ya saa 2 usiku alafu hapo lazima apige maesabu ya mamizani na diversions za vipande barabara zinatengenezwa.
Alafu mimi pia nashangaaa kwanini tanzania mizani ni mingi kama kila kawilaya humo porini unakuta mizani mbona kenya nimetoka nairobi hadi mombasa hamna mzani? nimetoka mombasa hadi tanga ndo nikaona tena mambo ya mizani. Au ilikuwa ni project ya kuwapa ajira wale watoto wa vigogo wapate mitaji ya biashara alafu hayo mamizani yaachwe yaoze kama kawaida baada ya wengine kupata mitaji ya biashara
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom