Dar es Salaam: Manispaa zake wanafanya wanayotakiwa?

kimatire

JF-Expert Member
Nov 27, 2008
371
93
Swali hili najiuliza mara kwa mara na sipati m jibu muafaka, kama kweli Jiji kwa maana ya City Council na Manispaa zake yani Ilala,Temeke na Kinondoni,Wanatimiza wajibu wake kwa Wananchi wake katika nyanja zote wanazotakiwa?

Nia hasa ya kuligawa JIJI la Dar Es Salaam katika Manispaa tatu ilikuwa ni kurahisisha utendaji wa kazi kwa watendaji wake pamoja na kuhakikisha mapato yanakusanywa kikamilifu.Lakini inashangaza jinsi mambo yanavyokwenda kienyeji kila kona ya Jiji,Si taka,wala mitaro ya maji machafu,Ujenzi wa kiholela,barabara mbovu achilia biashara kila pahala!

Kwamba hakuna mipango,au iliyopo haina mikakati ya kuifanikisha?
Wizara yenye dhamana sawa iko Dodoma lakini haya yote watoa maamuzi wako wapi?Usafi wa mazingira , fukwe kuvamiwa,vyoo vichafu kila kona ya Jiji-Uchafu nk

Kila kukicha porojo mpya kuhusu mwendelezo wa JIJI na harakati zake kumwezesha raia kuishi mahali safi ,salama,na kupata huduma nzuri iwe ya matibabu au shule au usafiri kutoka mahali pamoja kwenda mahali pengine nk.HIVI HIVI MPAKA WAPI NA LINI????Halafu tunajigamba Eti BANDARI SALAMA??Vivutio vya utalii ni uchafu uliozagaa kila mahali au ni bonde la Jangwani lilojaa mifuko ya plastiki?
 
mkuu kimatire nakusoma kwa shida kidogo jaribu ku edit maandishi yako yawe makubwa kidogo....
 
Yoyo

Utakuwa na matatizo ya Macho mbona maandishi makubwa na yanasomeka kabisa......au ulikuwa unamaanisha kivingine
 
Pamoja na yote hayo lakini Manispaa ya Temeke ndio kiboko yao ni chafu kupindukia iko nyuma kwa kila kitu sina uhakika kama kweli kuna Uongozi wa kueleweka katika Manispaa hii wa kufuatilia maendeleo yake
 
Pamoja na yote hayo lakini Manispaa ya Temeke ndio kiboko yao ni chafu kupindukia iko nyuma kwa kila kitu sina uhakika kama kweli kuna Uongozi wa kueleweka katika Manispaa hii wa kufuatilia maendeleo yake
Chocolate, Manispaa ya Temeke siyo kiboko ya uchafu kama ulivyodai ila kwa ujumla Manispaa zote ni chafu mno mno...
(1)Ilala...
Maeneo ya ( City centre,Kariakoo,Ilala Area,Buguruni,Vingunguti nk)
(2)Kinondoni...
Maeneo ya (Magomeni,Tandale,Manzese,Mabibo,Sinza,Mlalakuwa nk)
Ni machafu kuliko maeneo mengi ya Temeke...
 
Uchafu uliokithiri katika manispaa hizi ni kukosekana kwa usimamizi mzuri wa watendaji wanaohusika na usafi. Kampuni zilizopewa kazi ya kusomba taka hazina uwezo mkubwa wa kufanya kazi hiyo licha ya wakaazi kulipia huduma hiyo kila mwezi. Magari yao yote ni mabovu, yanashindwa kufanya kazi kwa ufanisi kwani muda mwingi yapo matengenezoni.
Taka zinazozalishwa kwa siku ni nyingi kuliko uwezo wa hayo makampuni kusomba kwa siku.

Jambo jengine ni kuwa uchafu umekuwa kama kitu cha kawaida katika macho ya watu, utakuta majalala mengi yapo mitaani katika makaazi ya watu huku yakitoa harufu mbaya, lakini hakuna kinachofanyika kuondoa usumbufu huo. Kuna Madiwani, Serikali za mitaa lakini wao huishia kwenye maofisi yao wakitafuta mambo yatakayowapatia wao fedha lakini syo kwa masilahi ya mitaa.

Waliopewa kazi ya kusimamia usombaji wa taka, wachunguzwe utakuta wengi wao ni wachafu, kuanzia nyumba wanazoishi ambazo ukitazama mazingira yake nyasi zimejiotea ovyo rangi pengine haijapakwa kwa miaka kumi na tano, sasa ingia ndani ya nyumba hizo kwanza utakuta kama kuna vioo basi vipo nusu nguo zimetundikwa mpaka sebuleni huko kunakoitwa ****** basi bora usiende utachoka mwenyewe na jiko halijagusa rangi labda tokea nyumba ijengwe vipi unampa mtu kazi ya kusimamia takataka ikiwa yeye mwenyewe taka ni kitu cha kawaida?

Tutegemee uchafu kuedelea kuzidi tu au tubadilishe tabia ya kuona uchafu ni kitu cha kwaida. Uchafu ni uchafu tu hata filter ya sigara ni uchafu makaratasi ya maofisini yanayotupwa ovyo ni uchafu, lakini wengine uchafu huo wanauokota na kuutumia tena.
Tukibadilisha tabia na kuona uchafu ni uchafu kuanzia majumbani mwetu mpaka sehemu za kazi na mashuleni basi jiji la Dar es Salaam litakuwa safi.
 
Viongozi wa Manispaa pamoja na Halmashauri zake wako kwa ajili ya kuangalia maslahi yao binafsi na sio kuhudumia/kutumikia wananchi. Kila shughuli inayotakiwa kufanywa wao huangalia kama kuna manufaa binafsi na sio umuhimu wa shughuli hiyo kwa jamii.
 
Chocolate, Manispaa ya Temeke siyo kiboko ya uchafu kama ulivyodai ila kwa ujumla Manispaa zote ni chafu mno mno...
(1)Ilala...
Maeneo ya ( City centre,Kariakoo,Ilala Area,Buguruni,Vingunguti nk)
(2)Kinondoni...
Maeneo ya (Magomeni,Tandale,Manzese,Mabibo,Sinza,Mlalakuwa nk)
Ni machafu kuliko maeneo mengi ya Temeke...

Tusker Bariiiidi,

Manzese iondolewe! sii chafu tena siku hizi WB wamefadhili miradi mikubwa ya mitaro ya maji machafu hadi kule Uwanja wa fisi! Maeneo kama Tiptop kuna mahoteli mazuri ya nguvu..na taa za barabarani karibu kila mtaa! Barabara ziko fresh na Manzese kuna biashara kubwa za Kimataifa sasa..wafanyabiasha wakubwa wa Kongo, Zambia, Malawi siku hizi hushukia Masenze kwa vile ni karibu na Ubungu stendi ya Mkoa!


Lini umefika Manzese?

Manzese sii ile ya zamani! Hata juzi tu Mkurugenzi Mkuu IMF alienda Manzese!
 
Naona mmeacha kujadili mada, mnajadili kwa kupendelea kila mtu anakotoka. Naona anayetoka Temeke anasema Temeke poa hali kadhalika kwa wale wanaotoka Ilala na Kinondoni
 
Tusker Bariiiidi,

Manzese iondolewe! sii chafu tena siku hizi WB wamefadhili miradi mikubwa ya mitaro ya maji machafu hadi kule Uwanja wa fisi! Maeneo kama Tiptop kuna mahoteli mazuri ya nguvu..na taa za barabarani karibu kila mtaa! Barabara ziko fresh na Manzese kuna biashara kubwa za Kimataifa sasa..wafanyabiasha wakubwa wa Kongo, Zambia, Malawi siku hizi hushukia Masenze kwa vile ni karibu na Ubungu stendi ya Mkoa!


Lini umefika Manzese?

Manzese sii ile ya zamani! Hata juzi tu Mkurugenzi Mkuu IMF alienda Manzese!
Heshima mbele Mzalendohalisi!!
Mimi ni mkazi wa Dar Es Salaam tena katika kiunga kimojawapo ambacho nimekitaja hapo juu nacho ni kichafu sana kilichopo katika wilaya ya Kinondoni (Wenyeji wa huku wanakiita KWA WAJANJA!!) nadhani umenipata WB imefanya kazi kubwa sana kuboresha mitaa ya Manzese kwa kuweka taa na mifereji na sehemu nyingine kuweka Lami,lakini hoja yetu je tunatunza tuliyowekewa na WB...
 
N wakina mzee Pinda wawe wanaibuka tu bila taarifa kuwatembelea hawa waheshimiwa, vinginevyo hata akitembelea mahali akakuta pachafu ajue kuwa wameshafanya usafi kweli kweli ndio maana akapakuta hivyo. angevamia bila taarifa angedondoka kwa maradhi ya moyo.....
 
Nimefurahi sana kuhusu mada hii. Mimi huwa najiuliza hivi tangu 1961 tulipopata uhuru hadi leo 2009 bado mitaa yetu kwenye wilaya zote hamna "sewege system" yakueleweka? Majira ya mvua ni hatari tupu - uchafu, mbu, inzi, harufu mbaya - halafue eti kuna Meya wa Jiji, eti kuna viongozi kwenye kila manispaa - eti kuna ma-bwana/bib afya - hizo fedha zinazotolewa kila mwaka kwenye kila manispaa ni za nini? zinakwenda wapi? nchi hii ni WIZI mtupu!!!!!! mafuruko kila mahali - jamani hivi hata Raisi wetu hajui hayo?? hao viongozi wanaogopewa au kwanini hawafanyi kazi? HIVI KUJAZA VIFUSI KWENYE BARABARA ZA MITAANI NI GHARAMA SANA AU BASI TU VIONGOZI WAMEAMUA KUTUTESA? KWA KWELI NI AIBU TUPU - KAMA KUNA MTU AMBAYE ANA ACCESS YA MEYA BASI AMHABARISHE KINACHOENDELEA. SHIDA NI KUWA HAWA VIONGOZI WANATAKIWA WATOKE KWENYE OFISINI, WATEMBEE WAONE - PIA WABUNGE - NAWASHANGAA SANA - HALAFU ETI TUNAPIGA KURA TUNAWAPA NDIYO - I sometimes dont understand -
 
Jamani JIJI ni chafu kila kona!!!!Mbona baadhi ya miji inajitahidi sana?Hili JIJI ndiyo limeshindikana kabisa???Kampeni ya mtu ni Afya iko wapi tena?Huku kutunza mazingira tunakokusema ni wapi??Je viongozi wa JIJI na Manispaa zake wanaiona hali hii.Taa za barabarani,Mitaro ya maji machafu,ujenzi wa kiholela,matumizi mabaya ya fukwe za bahari,Matumizi mabaya ya barabara yote haya ni mambo ya msingi kwa JIJI letu,Achilia mbali mahospitali ,shule za msingi na Sekondari nk.
Wananchi tunahitaji elimu ya umma,jamii inahitaji kupewa fursa ya kuhamasisha mwamko wa viongozi wa JIJI wanaochapa usingizi.
 
Back
Top Bottom