Dar Bana.....Nusura Nife!!

Ni sawa, lakini ni vema kujuzana. Kimsingi ni vema kumfahamu nyoka aliyekuuma. Ila huduma ya kwanza mbali na kufunga juu ya eneo uliloumwa, unashauriwa kuchanga na kujaribu kukamua sumu (wengine hushauri mtu afyonze sumu -endapo hana kidonda mdomoni). Hii ya kuchanga na kulazimisha damu kuchuuzika/kutoka hupunguza kiwango cha sumu kinachoelekea kwenye moyo
Loh. . . pole sana.

Mi najua huduma ya kwanza kabisa ni kufunga juu kidogo ya ulipogongwa ili sumu isisambae, au hata hiyo tu walishindwa?
 
Pole sana mkuu, yaani badala ya kukutibu wao wanakazana umeumia ukiwa wapi? Kama walitaka Police RB c wangekwambia?
 
Pole sana mkuu, yaani badala ya kukutibu wao wanakazana umeumia ukiwa wapi? Kama walitaka Police RB c wangekwambia?
Kweli kabisa kaka hawa jamaa sijui vipi, niliwamaindi sana tu basi maumivu ndio yalinizuia kuwafanyia kitu mbaya..
 
Pole sana mkuu zahanati nyingi wamejipanga kuwahudumia wahanga wa bodaboda tu.Inabidi ukainunue hiyo sindano ili ukipita tena kitaa uwe umejiandaa kabisa
 
Pole sana ungewaona wenzetu wamasai wangetoa hayo meno na wangepatia ugoro huwa inasaidia.
 
mishemishe za vichakani siyo nzuri ndugu yangu, kwanini usitafute nyumba za wageni?
 
Pole Ndugu, Mshukuru sana Mungu kwa kukuacha mzima. Nyoka wengine sumu yao yaweza kumuua mtu ndani ya dakika 30 tu! Na hizi foleni za Dar, kufika Muhimbili ilikuwa neema ya Mungu! Umejaribiwa Mkuu, Keep on Praying!!
 
Nilikumbwa na adha kama hiyo! Sindano inaitwa anti snake, muhi2 na mnazi 1 hosp inatolewa bure! Tmj laki 3
 
Kisa chako kinafanana na jamaa mmoja Dar aligongwa na nyoka lakini hakujua kama kagongwa na nyoka. Ikafikia mahali akazimia kutokana na sumu kupanda, ilipikuja kugundulika na nyoka ndiye aliyemng'ata ilikuwa issue kupata ile sindano ya sumu!!!

Kidogo afe jamaa!!!

Hiyo ndiyo Dar.
 
kijana au ulikutana na nge? Sumu ya nyoka sio ya kitoto ujue

kuna vinyokanyoka vingine hata kikikung'ata haishtui sana....kama huyo wa jamaa ambae alimruhusu kuzunguka kwenye mahospital.....kuna minyoka bana...ikikutia jino....unaanza kugawa urithi mida hiyo hiyo.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom