Tutazunguka weee lakini jibu ni simpo especially kwa Dsm watu hawajiandikishi na walijiandikisha huwa hawapigi kura......period. Kamvua kakinyesha kidogo tu basi ni kisingizio cha kutokupiga kura.
Arusha tuliwapiga chini CCM lakini tusahau kulinda kura za mheshimiwa Lema, F Mrema akisaidiwa na usalama wa taifa wakafanikiwa kuiba kura.Mwaka huu tulimchagua tena diwani wa TLP kata ya sombetini baada ya kazi nzito ya kulinda kura lakini tena jamaa wa CCM wakamwaidi nyumba ya kisasa eneo la njiro hapa jijini Arusha diwani wetu akajiuzulu.Wakaazi wa mjini Arusha tulishaonyesha njia siku nyingi nadhani mnakumbuka tulimchagua Makongoro Nyerere mwaka 1995.
Eti Mliwashinda CCM kisha wakaiba kura, sawa kama mngempigia 100% wangiba nini? ndugu zangu wa mjini hetbu tuna tatizo gani? huku ndiko magazeti mengi, uelewa wa kutosha, TV ............. za kumwaga, ni kwanini mageuzi haya yasianzie hapa mijini jamani? kuna tatizo gani jamani??????????????
Iweje CCM washinde mijini? jamani tunaamini huku mijini ndiko kuna uelewa mkubwa, magazeti mengi, Redio za kutosha na TV!!!!!!!!
Mijini ndiko kunafukuzwa wamachinga, watu kubomorewa majumba, hebu inakuweje jamani?
Waandishi wote wanaishi mijini.
Wasomi wote wanaishi mijini...................., jamani nielezeni kuna nini? ama CCM huku mjini wanafavya kamchezo gani? ina maana hata wewe uliwachagua ccm 2005?
JF nisaidieni kuna nini basi hatupati kufanya mapinduzi huku mjini na badala yake yake mapinduzi yanafanyika kule Karatu, Tarime,Mpanda na Bariadi?
Jamani kuna nini huku Arusha, Mwanza, Dar na hata hapa Mbeya?
wasomi na watu wamjini watakwambia kaelimisheni watu wa vijijini maana hawajui lile wala hili.
sijui watu wavijijini kwa kutokua na elimu yao wanawashikia kalamu wasomi na watu wa mjini kutochagua upinzani??
Tatizo la TZ ni tatizo la kitanzania si tatizo la chama.