Daniel Ole Njolay kugombea ubunge Arusha mjini

kuna tetesi kuwa ccm inamuandaa aliyewahi kuwa R.C wa arusha ndg Daniel Ole Njolay kuingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa arusha mjini iwapo chadema watashindwa rufaa yao.

ndio takataka gani hiyo hiyo njolai...? Anamjua lema kweli huyo jamaa? Kwanini asingechukua ushauri kwa pinda kwanza kabla ya kuingia uwanjani?
 
Njolaay yupi mnamzungumzia? Ni huyu mwenye kesi ya kuuza viwanja mara mbili?
Hahaaaaaaaaaaaaa asante magamba kwa kurahisisha M4C through the ballot box!

After all kusema ukweli hakuna uchaguzi Arusha!

Mkuu mungi ni kweli hiyo??nimecheka sana'ccm wamekosa mwelekeo Arusha'swala la udhaifu wa mwenyekiti wao litawamaliza'wa,simamishe mkapa
 
Yawezekana ccm hawana inteligensia yenye weledi wa kutosha, vinginevyo wangetumia influence yao kama chama ili kuhakikisha kwamba matokeo yoyote ya ubunge ya 2010 katika maeneo ambayo hawana sapoti ya kutosha hayatenguliwi. kwa sababu uchaguzi wowote wa halali katika seheme kama Arusha ama Mwanza ni maumivu matupu kwao. na kadiri wanavyoshindwa kwa sasa, inasensitaizi kushindwa kwao 2015. Wainfuluensi lema arudishiwe ubunge wake kwa kufuata taratibu zozote (mf. rufani) na waachane na kesi zote katika maeneo hatarishi.
 
Naomba agombee NAPE NAUYE ili ajipime kama akiongea anaeleweka au huwa anapiga domo tu. AKISHINDWA basi agombe Mkapa, Malechela Au Sumaye ili wajue nguvu ya Lema ikoje! AU wampe Asha rose migiro Au Mwamtumu mahize. Da Nilimsahau Mery Chatanda. Lakini CHADEMA MAHAKAMA IKICHELEWA KUTOA MAJIBU YA RUFAA IPOTEZEENI MUWENDE KWENYE UCHAGUZI TUNATAKA TUMUONE LEMA BUNGENI TEna kwa nguvu ya uma na c ya mahakama.
 
Kama CCM wanajitakia mema basi wangepiga simu kwa majaji wa high court ili wamrudishie Lema ubunge wake. Bila Lema Arusha CCM watafutika 2015.

Njolay Arusha ni utani mbaya. Pandora box yake bado haijafunguliwa. Achukue fomu.
 
Kama ccm hakina namna yoyote ya kupata mrejesho wa wananchi wa jinsi wanavyoichukulia ccm hapa Arusha, basi tunawaruhusu wasaidiwe na UWT kabisa, wapewe full information, huenda wakalipunguzia taifa gharama!
Njolai Ana kibri sana na wana Arusha hawajamsahau kwa kauli zake tata, na kuonyesha wazi kuwa alihongwa na AFGEM ili awanyanyase wananchi.
Kwanini ccm wamtafutie mwenzao kifo cha mapema kwa kumpima na Lema?...au ni namna ya kum'eliminate kama adhabu?
Kama kuna Ndugu zake wanaonufaika na huyu mzee bora wamkataze...amwambie mapema Kikwete kwamba ana KISUKARI kibaya sana na hawezi hiyo kazi ya aibu!
 
mwenye historia ya njolay kwenye tasnia ya utalii atuwekee
Mm nilisikia alliambiwa akasome aache kuchunga tena ilikuwa Umasaini leo akashindane na mgombea kijana atagalagazwa Arusha mji wa wageni tangu mbunge askari Magereza mpare na sio tena mji wa Wamaasai
 
Sasa huyu mtu kawa Mbunge Miaka Mingapi? hawezi kuachia Sura Mpya, Mtizamo Mpya, Siasa Mpya?

Amesha kuwa Mbunge, Waziri Mdogo, Mkuu wa Mkoa - Acha afurahie Uraia kabla ya kufariki
 
kuna tetesi kuwa ccm inamuandaa aliyewahi kuwa R.C wa arusha ndg Daniel Ole Njolay kuingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa arusha mjini iwapo chadema watashindwa rufaa yao.

Hata akiletwa Jaakaya na Chadema wakaweka jabali-jiwe hakika mshindi atakuwa jabali-jiwe.Arusha ccm huku Kama wapo ni kidogo sn na hao kidogo wananufaika kimaslahi kuwa kwao ccm.Peoplesssss powerrrrrrrr.
 
bado sijajua yuko kundi gani.
Inawezekana ikawa ni option ya lowassa.
Au inawezekana ikawa ni option ya jk akitaka kumuondolea machungu.

Aendeleze biashara yake ya mabasi na shule asijesumbua na ubunge wa Arusha. Akitaka ajaribu Longido.
 
kuna tetesi kuwa ccm inamuandaa aliyewahi kuwa R.C wa arusha ndg Daniel Ole Njolay kuingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa arusha mjini iwapo chadema watashindwa rufaa yao.

Ole Njolay ana akili sana hawezi kutolewa kafara kwa mara nyingine, labda kama kaharibikia Rukwa.
 
mwacheni akajitengenezee mazingira ya kuongeza sukari na bp
ili atangulie mapema.
 
kuna tetesi kuwa ccm inamuandaa aliyewahi kuwa R.C wa arusha ndg Daniel Ole Njolay kuingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa arusha mjini iwapo chadema watashindwa rufaa yao.

Labda wamfufue Sokoine tu... Wengine wote hawatoki
 
Back
Top Bottom