Danganya toto ya barabara feki za manispaa za jiji letu la Dsm inatupeleka wapi?

lonyorengai

Member
May 12, 2008
71
35
Wadau naomba tujadili hili kwa mapana zaidi. Barabara zinazojengwa na manispaa zetu kwa sasa zina kiwango duni kwa mfano katika manispaa ya Kinondoni, Kijitonyama barabara ya Akachube, Kipande cha Sinza Uzuri, na nyinginezo nyingi ambazo hata mwaka hazijamaliza lakini tayari zimeumuka na mahandaki pia yamejitokeza. Kimsingi huu ni ufujaji wa fedha za walipa kodi na pia kuna kila dalili za teni pasenti kwa kuwa siamini kwamba madiwani na mameya hawaoni ubovu huu wa barabara kiasi cha kuzikubali.

Hii inatokea katika maeneo mengi ya nchi yetu kama Arusha, Dodoma n.k.

Siasa katika miradi kama hii itatupeleka shimoni. Mheshimiwa Jerry Slaa, naomba majibu yako!
 
Nilishawahi kusema Hapa katika ufujaji Mkubwa wa hela za walipakodi upo ndani ya manispaa!! No one is responsible!! Kinondoni inaongoza!!
 
Kuna barabara ya Mombasa – moshi ukonga yaani kwanza ilikuwa ifanyiwe upanuzi lakini imeachwa hivyo hivyo na sasa wanasema wanajenga mita 800 kiwangoi cha lami lakini barabara kama kauchochoro. Jerry jibu hapo huo si usanii mkubwa hamna akili ya kesho jamani. Bora mgeacha kuliko kufuja pesa zetu za kodi. Huu ujinga ili mradi mnapata ten percent basi
 
Back
Top Bottom