Damu za Watanzania Hazitapotea Bure

Ernesto Che

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,114
293
Wapendwa katika mapambano ya ukombozi wa Tanzania. Kila kukicha askari polisi wanazidi kuua raia wasio na hatia katika nchi yetu. Wamesahau Haki zetu za kuishi waka kuandamana kufikisha ujumbe, wao wanachojua ni kutuua tu. Nawasikitia kwa kuwa wanadhani wanatutisha kumbe wanazidi kutufanya tuwe na sababu zaidi ya kudai ukombozi wa nchi yetu. Kuna msemo usemao "Amani haiji ila kwa ncha ya upanga" Hili tukio la mauaji ya Songea limezidi kudhihirisha kuwa watawala wetu hawana nia nzuri na sisi. Nikirejea matukio kadhaa ya nyuma ambayo Polisi waliua wananchi bila sababu za msingi ni haya.

1. Mwembechai. 2. Zanzibar 3. Arusha 4. Wafanyabiashara wa Madini (Zombe). 5.Mbarari (Mbeya), 6. Mbeya 7. Songea na mengine mengi sikuyataja.

Hakika si wakati wa kuacha hali hii ipite hivihivi ila Watanzania tuamke na kudai haki zetu ili utawala huu ambao hauna uwajibikaji kwa mauaji uone athari. Nchi nyingi zimepitia hali hii na kupata ukombozi kama vile Palestina, Libya, Sudani Kusini, Kosovo, n.k. Tuamke ili wajue kwamba tumechoka kuuwawa bila sababu.
 
Back
Top Bottom