Damu nzito

FYATU

JF-Expert Member
Dec 7, 2011
5,392
4,468
Kuna bwana anomba msaada wa ushauri.

Miaka kama kumi na saba iliyopita, akiwa kidato cha tatu, jamaa alipewa taarifa na Dada wao wa kazi kuwa ni Mja mzito....baada ya Dada kuona jamaa anakodoa macho kodo akamwambia 'usishtuke Wewe soma siwezi kukuingiza kwenye majukumu mazito mapema hii'...kama utani na kweli Dada wala hakumuuliza tena.

Jamaa anakiri kuwa ni kweli kwa wakati huo wote mapenzi kati yake na Dada yalikuwa moto moto ile mbaya, wanakula na kupakuwa hapo ndani kama Wenye nyumba.

Ila kwa wakati huo huo kulikuwa na Kijana aliyekuwa anaishi jirani yao, alikuwa ni Kijana kufikia, na tofauti kati yake na Watoto wa familia ile ilikuwa dhahiri...alionekana zaidi kama House boy pale.

Kijana wa Watu alikuwa anamsumbua sana Dada, na Dada na Jamaa walikuwa kama vile wanashirikiana kumdhihaki Kijana yule, Jamaa alikuwa anavizia njiani na kumuita dada, basi Dada anamtolea nje alafu anakuja na kumuadithia Jamaa hivyo huishia kucheka sana. Kijana yule alikuwa tayari na umri wa kuoa, hivyo alikuwa seriou na hakukata tamaa kwa Dada, alikuwa Mlokole na Mchapa kazi kwelikweli na wala hakuhitaji kutembea na Dada yeye alikuwa anataka wakapange Nyumba waishi....Kufupisha hii stori ni kuwa Dada aliishia kuishi na yule Kaka.

Baada ya miaka kama kumi na hivi Jamaa alifanya utafiti na kugundua Dada anapoishi na yule Bwana, wakati huo tayari Dada na Bwana wake wana Watoto Watatu..Jamaa akafanya jitihada kukutana na Dada a.k.a x wake, akajaribu kumkumbusha kuhusu lile suala la Mimba Dada alimchenjia balaa, akamwambia hakuna kitu kama hicho na wala hakuwahi kumwambia kama ana mimba yake, na kumuonya Jamaa asimfuatilie tena...Sasa yapata miaka kama kumi na saba na Jamaa anatamani japo aambiwe tu kama yule Mtoto ni wake, Ndoa ya Dada ni imara na Wameshajijenga kimaisha mambo yao safi, Wana Nyumba kadhaa, Usafiri n.k..Jamaa bado ni Mlokole na Mke naye alishakuwa Mlokole.

Inavyoonyesha dada hana imani kama akimwambia yule ni mwanae yataishia hapo hapo...sasa afanyeje na DAMU NI NZITO? na jamaa na uhakika wa asilimia tisini kuwa yule Binti mrembo ni wa kwake.
 
Kuna bwana anaomba msaada wa ushauri.

Miaka kama kumi na saba iliyopita, akiwa kidato cha tatu, jamaa alipewa taarifa na Dada wao wa kazi kuwa ni Mja mzito....baada ya Dada kuona jamaa anakodoa macho kodo akamwambia 'usishtuke Wewe soma siwezi kukuingiza kwenye majukumu mazito mapema hii'...kama utani na kweli Dada wala hakumuuliza tena.

Jamaa anakiri kuwa ni kweli kwa wakati huo wote mapenzi kati yake na Dada yalikuwa moto moto ile mbaya, wanakula na kupakuwa hapo ndani kama Wenye nyumba.

Ila kwa wakati huo huo kulikuwa na Kijana aliyekuwa anaishi jirani yao, alikuwa ni Kijana wa kufikia, na tofauti kati yake na Watoto wa familia ile ilikuwa dhahiri...alionekana zaidi kama House boy pale.

Kijana wa Watu alikuwa anamsumbua sana Dada, na Dada na Jamaa walikuwa kama vile wanashirikiana kumdhihaki Kijana yule, Jamaa alikuwa anavizia njiani na kumuita dada, basi Dada anamtolea nje alafu anakuja na kumuadithia Jamaa hivyo huishia kucheka sana. Kijana yule alikuwa tayari na umri wa kuoa, hivyo alikuwa seriou na hakukata tamaa kwa Dada, alikuwa Mlokole na Mchapa kazi kwelikweli na wala hakuhitaji kutembea na Dada yeye alikuwa anataka wakapange Nyumba waishi....Kufupisha hii stori ni kuwa Dada alikuja kuishi na yule Kaka wa Jirani.

Baada ya miaka kama kumi na hivi Jamaa alifanya utafiti na kugundua Dada anapoishi na yule Bwana, wakati huo tayari Dada na Bwana wake wana Watoto Watatu..Jamaa akafanya jitihada kukutana na Dada a.k.a x wake, akajaribu kumkumbusha kuhusu lile suala la Mimba Dada alimchenjia balaa, akamwambia hakuna kitu kama hicho na wala hakuwahi kumwambia kama ana mimba yake, na kumuonya Jamaa asimfuatilie tena...Sasa yapata miaka kama kumi na saba na Jamaa anatamani japo aambiwe tu kama yule Mtoto ni wake, Ndoa ya Dada ni imara na Wameshajijenga kimaisha mambo yao safi, Wana Nyumba kadhaa, Usafiri n.k..Jamaa bado ni Mlokole na Mke naye alishakuwa Mlokole wala hawana neno na Mtu.

Inavyoonyesha dada hana imani kama akimwambia yule ni mwanae yataishia hapo hapo...sasa Jamaa afanyeje na DAMU NI NZITO? na jamaa anasema ana uhakika wa asilimia tisini kuwa yule Mtoto/Binti mrembo ni wa kwake.
 
Member ...

Ila mkuu mwambie jamaa ako asiende kudai mtoto atavunja ndoa ya watu pia ni dhambi kubwa sana. ..
Anavyojitetea ni kuwa anataka tu ahakikishiwe kama Mtoto ni wake kwa kuwa siri yote anayo Mama....sasa ni vigumu kumuamini kama kweli akishaambiwa ataishia hapo hapo.
 
Kuna bwana anaomba msaada wa ushauri.

Miaka kama kumi na saba iliyopita, akiwa kidato cha tatu, jamaa alipewa taarifa na Dada wao wa kazi kuwa ni Mja mzito....baada ya Dada kuona jamaa anakodoa macho kodo akamwambia 'usishtuke Wewe soma siwezi kukuingiza kwenye majukumu mazito mapema hii'...kama utani na kweli Dada wala hakumuuliza tena.

Jamaa anakiri kuwa ni kweli kwa wakati huo wote mapenzi kati yake na Dada yalikuwa moto moto ile mbaya, wanakula na kupakuwa hapo ndani kama Wenye nyumba.

Ila kwa wakati huo huo kulikuwa na Kijana aliyekuwa anaishi jirani yao, alikuwa ni Kijana wa kufikia, na tofauti kati yake na Watoto wa familia ile ilikuwa dhahiri...alionekana zaidi kama House boy pale.

Kijana wa Watu alikuwa anamsumbua sana Dada, na Dada na Jamaa walikuwa kama vile wanashirikiana kumdhihaki Kijana yule, Jamaa alikuwa anavizia njiani na kumuita dada, basi Dada anamtolea nje alafu anakuja na kumuadithia Jamaa hivyo huishia kucheka sana. Kijana yule alikuwa tayari na umri wa kuoa, hivyo alikuwa seriou na hakukata tamaa kwa Dada, alikuwa Mlokole na Mchapa kazi kwelikweli na wala hakuhitaji kutembea na Dada yeye alikuwa anataka wakapange Nyumba waishi....Kufupisha hii stori ni kuwa Dada alikuja kuishi na yule Kaka wa Jirani.

Baada ya miaka kama kumi na hivi Jamaa alifanya utafiti na kugundua Dada anapoishi na yule Bwana, wakati huo tayari Dada na Bwana wake wana Watoto Watatu..Jamaa akafanya jitihada kukutana na Dada a.k.a x wake, akajaribu kumkumbusha kuhusu lile suala la Mimba Dada alimchenjia balaa, akamwambia hakuna kitu kama hicho na wala hakuwahi kumwambia kama ana mimba yake, na kumuonya Jamaa asimfuatilie tena...Sasa yapata miaka kama kumi na saba na Jamaa anatamani japo aambiwe tu kama yule Mtoto ni wake, Ndoa ya Dada ni imara na Wameshajijenga kimaisha mambo yao safi, Wana Nyumba kadhaa, Usafiri n.k..Jamaa bado ni Mlokole na Mke naye alishakuwa Mlokole wala hawana neno na Mtu.

Inavyoonyesha dada hana imani kama akimwambia yule ni mwanae yataishia hapo hapo...sasa Jamaa afanyeje na DAMU NI NZITO? na jamaa anasema ana uhakika wa asilimia tisini kuwa yule Mtoto/Binti mrembo ni wa kwake.
Mwambie ajitahidi apate kitu chenye DNA ya huyo mtoto na mimi nitamfanyia kipimo cha DNA bure. Hakuna haja ya kuvunja ndoa ya watu kwa jambo dogo kama hili.
 
Jingaa kabisa MTU alishindwa kutunza ,Leo anataka mtoto watu tumeowa primary mpaka tukafukuzwa home,,Leo tumemeki life na watoto wetu wanatuita kaka,, Japo mi ni me kwa kweli wanaume wa jinsi hiyo wananikera sana maana uwezo wakufikiri ni zero alijua atakuwa mtoto milele,,Amuache mama wa watu aendeleee na ndoa yake
 
Kuna kigogo wa serikalini alikufa na usongo, mtoto ambae hakumlea amekuja kuwa na mafanikio makubwa na anatumia ubin wa baba mwingine, eti kijana ameoa na maisha yake anampigia simu kuwa mimi ndiyo baba yako, kijana akamwambia usirudie tena maneno hayo.
 
Aisee mkuu
 
Hawa dada wa kazi wamefanywa sana training ground ya ngono yani kwetu kama mzee alijua, alikua analeta wamama tu niwaogope
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom