Mkuu hii wengi wanaileta hii ya kuwa na vyama vingi katika uchaguzi kama sababu lakini ni uongo wa watu wasiofuatilia vizuri. Hii yetu ndio demokrasia ya kweli. Anayeshinda bila zengwe ndiye mshindi wa kweli na ndiye anakuwa chaguo la wengi.
Ni vizuri ieleweke kuwa ccm ni chama kama vyama vingine katika race hii na wananchi ndio wachaguaji. Kama wananchi wanahitaji ccm bado hata kama vingekuwa vyama viwili tu kingeshinda. Kuna ushahidi wa wazi ambao unaonyesha kuwa viliwahi kushiriki vyama vichache na ccm ikashinda na kuna majimbo viliwahi kushiriki vyama zaidi ya vitatu na ccm ikabwagwa chini. Hivyo basi wananchi kama wataelewa haki yao na hawatakubali kuraghaiwa kwa vizawadi na ahadi hewa za maendeleo yasiyokuwepo na pale katiba itakaporekebishwa ili kuiondoa hii tume ya wizi wa kura inayochaguliwa na mwenyekiti wa ccm, hapo ndipo kutakuwa na mwisho wa ccm. Bila hivyo hata kama ukiweka vyama viwili tu, itashinda ccm.
Fuatilia tangu Tanzania ianze mfumo wa vyama vingi vyama vya upinzani vinapata kura ngapi na CCM inapata kura ngapi. Utakataa ukweli tatizo la kuindoa CCM madarakani ni gumu kutokana na vyama vya upinzani kutokuwa na ushirikiano, mwelekeo wao upo kwenye RUZUKU zaidi,huwezi kupingana na serikali ambayo unaitegemea kukupa pesa ili ujiendeshe. Vyama vya upinzani vimeigeiuza ruzuku kama ni haki yao kimsingi, matokeo CCM ndiyo inayonufaika zaidi na ruzuku. Wapinzani wameng`ang`ania kuilaumu TUME YA UCHAGUZI ni mara ngapi wamashauriwa kususia uchaguzi ili kusishinikiza serikali kuunda tume huru? Ili CCM iondoke madarakani wapinzani wanapaswa kuwa kitu kimoja na RUZUKU lazima iondolewe.
Chama
Gongo la Mboto DSM