Dalili za kudhulumiwa

Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
7,123
26,605
Wakubwa natarajia mko wazima.

Msaada wa kisheria (Ki mawazo) unahitajika jamani. Ninaona dalili za kudhulumiwa haki yangu zinaninyemelea naombeni mawazo yenu wakuu.

Nina kadaladala kangu kanakimbia-kimbia hapa Dar, baada ya kukatoa tu bandarini mama mmoja jirani yangu alinifuata akimuombea mwanae kazi ya udereva na alimdhamini. Yule bwana akaomba alaze gari karibu na kwake awe anawahi trip za alfajiri. Baada ya uchunguzi wangu wa awali baada ya wiki chache nikagundua yule bwana ni muhuni japo yeye na mama yake ni walokole pyua. Akaja na stori tairi zimeisha tubadili nikampatia pesa, akaja na stori stata inasumbua nikampatia pesa hiyo haikutosha akaja na stori anaenda kuinua gari iko chini sana nikampatia pesa na kila nikimuukliza haya mambo anadai nitafanya kesho nitafanya keshokutwa. Baada ya kupita muda nikashindwa nikasimamisha gari maana hatekelezi haya yote japo pesa nimeshampatia na kudai pesa nilizokuwa nampa, akawa ananikwepa nikaona isiwe tabu nikaenda serekali ya mtaa akaitwa yeye na mama yake (mdhamini) wakakubali deni na wakasema atalipa baada ya miezi 3. Muda umefika wako kimya nimewafuata wanasema hawana hela watalipa February mwishoni!

Waungwana ni hatua gani stahiki naweza chukua sasa?
 
kama mliandikishana vizuri kwa mweneykiti wa mtaa, nenda polisi, watie ndani, toa kitu kidogop asiachiwe kwa siku japo tatu, ikishindikana mpeleke mahakamani atakulipa japo kidogo kidogo ila haki yako itapatikana.
 
Back
Top Bottom