Elections 2010 Dalili ya ushindi wa kushindo kwa chadema imekwishaonekana

dalili ya saba unajidanganya.wanaochangia CHADEMA NI WACHAGA TU, kwani wana maslahi na hicho chama chenu cha kikabila. dalili ya nane nayo ni uwendawazimu kuitilia maanani kwani wengi wanaopost comment zao humu ni washabiki wa CHADEMA ambao kuna ushahidi kuwa si wapiga kura( kumbuka hata Mrema alibebwa kama jeneza lakini aliangukia pua. CCM imewekeza kwa wazalendo wa hali ya chini ambao hawajui hata computer ina umbo gani na for sure wao ndio wapiga kura.
panua miguu na uwe tayari kufanyiwa tohata(kutahiriwa) kwa mara nyingine

Mkuu ili hoja yako ieleweke siyo lazima utumie lugha kali kama ilivyo kwenye sentensi yako ya mwisho.

Hapo kwenye uwekezaji ndipo ambapo ninaomba ufafanue, mmewekeza nini? The only way ya kuwekeza kwa watu wa chini/vijijini ni kwa kuboresha bei za mazao yao, hapo ni total failure. Kila kona bei ya mazao ni mbaya kuliko. Kuanzia kahawa, tumbaku, pamba, mpaka mahindi. Bado miundombinu ya vijijini ni zero, maji zero, afya zero, elimu ndo usiseme kabisaaaa. Hebu niambie huo uwekezaji unaousema ni upi?

Usiwatukane wakazi wa vijijini, sema ukweli kwamba mnatumia ujinga wao au kutojua kwao haki zao na ndio maana mnapata kura. Zikitokea NGOs kama HakiElimu zikaanza kuelimisha jamii serikali inakuja juu. Hata Zimbabwe ilikuwa hivyo hivyo, ushindi wa Mugabe ulikuwa unatoka vijijini, iko siku waliamka na kujua haki zao. Hata Tanzania ya leo mwamko upo, taratibu mtaondoka tu, maana wananchi wanaamka na kuelewa haki zao na kujua adui yao wa kweli ni nani.

Mwaka 2005 mlipeta kilaini, mwaka huu hali ni ngumu ndio maana mmeanza kutoa hata ahadi ambazo hazitekelezeki na kusema uongo juu. Mojawapo ya mambo ambayo mmesema uongo ni pamoja na JK kusema amepandisha mishahara halafu waziri wake anasema HAPANA, wote wako ndani ya serikali moja. Mnaahidi kugawia watu ardhi na kumbe mlishauza kwa wawekezaji, Kigamboni wamewabana mseme agenda yenu, JK kaingia mitini anasema ni jukumu la diwani, yaani maamuzi lifanye baraza la mawaziri, halafu umsukumie diwani? Hata aibu hana! Mmewadanganya wakulima wa mahindi wa Mby kwamba wakauze mahindi yao SGR na kumbe hakuna hela. Mamlaka ya Korosho baada ya kuona cheche za Prof Lipumba juzi wamejifanya kutangaza kufungua msimu wa kununua korosho, ajabu ni kwamba hawana hata senti wanategemewa wakanunue mali kauli!

Huo ndio uwekezaji wenu kwa kutumia ujinga wa watu wa chini kabisa ambao umewaelezea vyema kabisa kwamba hawajui hata computer, sema kabisa kwamba hawajui hata kusoma, maana ujinga wao ndio mtaji wenu! So sad ... na unasema kwa ujasiri kabisa kwamba mmewekeza kwenye ujinga wao!
 
Ndugu zangu, Hii siyo kificho tena. Kuna vituko vingi Dr. Slaa anafanyiwa ili mradi aonekane hana sifa. Lakini hata hao wanaotaka jamii ione kuwa hana sifa, wao wenyewe wanofanya mipango hiyo, wanajua kuwa Dr. Slaa ni moto wa kuotea mbali kwa habari ya sera na uongozi shupavu.

Jakaya mpaka sasa ahadi alizotoa 2005 hazikukamilika, ahadi anazotoa leo hazitekelezeki wala hazina manufaa kwa wananchi wa kawaida. mfano, JK amewaahidi wananchi wa Kigoma kuwatengenezea uwanja wa ndege wa Kimataifa, wananchi wa kawaida wa Kigoma watafaidikaje? watapanda ndege?

Ushindi upo, piga na linda kura yako isichakachuliwe na Chi Chi Em
 
[/QU
icon1.gif
Re: Dalili ya ushindi wa kushindo kwa chadema imekwishaonekana


Kuna Mtu kanipa theory hii, sikupenda kuiamini. Please take it as a Quizz:

Kuna wapiga kura makundi mawili: Kund A na Kundi B

Kuna vyama vitatu vyenye ushawishi: Chama A, Chama B na Chama C:

Inaaminika kuwa kura za Kundi A: Zitagawanyika kwa Chama A na Chama B na Chama C

Where as kura za Kundi A: Zitaenda Chama A na Chache Chama B

Kundi A ni nani na Kundi B ni nani?

Chama A, B na C ni nani?

Why?OTE]


Kundi A Wale wa mjini
Kundi B Wale wa vijijini

Chama A CHADEMA

Chama B CCM

Chama C CUF

Nimefaulu_
 
dalili hizi ni tosha kuwa chadema sasa imeshakamata nchi

dalili ya kwanza

ratiba ya kampeni ya ccm imebadilishwa ambapo mgombea urais sasa hatapumzika

dalili ya pil
ccm wameshaonesha kushindwa kujibu hoja za msingi na hivyo wameanza kutumia hoja za udaku

dalili ya tatu

ccm wameshindwa kupata sababu ya kumshitaki dr slaa na wanatumia watu wengine na magazeti yasiyo na status

dalili ya nne

hoja wanazotoa ccm ni za kigorilla ambao anayemvamia slaa hajitokezi wazi na hata akiulizwa anajaribu kukana

dalili ya tano

kampeni zinazoendelea zinaonyesha ccm wamekumbwa na zomeazomea hata kwenye maeneo wasiyokuwa wametarajia

dalili ya sita

vyombo vya habari vikuu kama televisheni na baadhi pia ya magazeti yanaogopa kuweka kampeni za chadema wazi wazi na hata wakiweka wanajaribu kuficha hoja zenye nguvu. Tbc kukatisha matangazo yake kuficha baadhi ya hoja zenye nguvu ni mfano mmojawapo

dalili ya saba

hadi sasa chadema ndio chama pekee ambapo wananchi wanachanga fedha zao japo sio wanachama

dalili ya nane

angalia polls zilizoendeshwa na dailynews na walipoona dr slaa anagongesha chart kwa ushindi wa kishindo walizitoa. Hapa jf utaona mwenyewe polls zipo wazi na matokea yapo wazi.

dalili ya tisa

hakuna ahadi zozote zenye mvuto toka ccm, na wananchi wameshashtuka kuwa wanafanywa mabwege

dalili ya kumi

uwezo wa kiuongozi wa dr slaa hakuna hata mmoja aliyeweza kuupinga, na ndio maana wanaleta hoja za magazeti ya udaku, na kuacha mambo ya msingi


nini maana ya hizi dalili

ccm watakuwa wanafikiri jinsi ya kuiba kura baada ya kukosa mvuto kwa umma, na hili ni hatari kwa taifa, kama wataendeleza tabia hii ya kitoto, isiyoonyesha kuheshimu demokrasia.



Dilili ya kumi na moja
Wanamtumia hata mama Kikwete ktk kampeni, badala ya UWT kama ilivyokuwa siku za nyuma. UWT kama wamegoma vile maana hawana kitu cha kuwaambia akina mama maskini wa Tanzania CCM HAWAAMINIANI. AGALIA HATA KIPINDI CHA KUSAKA KURA ZA WADHAMINI WA KIKWETE. alimtumia Ridhiwani.
 
Vijijini wameamka, mijini kuna matatizo ya watu kutaka kuuza kura. Leo kaika kijiji nilikozaliwa mgombea wa CCM alishindwa kuhutubia mkutano wa kampeni kwa kuzomewa na watu wengi, kijiji cha Haydom - Mbulu, mwaka huu vijiji vya kule watu wengi wamekataa kudanganywa. Kila kona ni mjadala. Chadema ina nafsi kubwa ya kushinda mbulu.

Napenda muelewe kuwa vijiji vingi watu wameamka ila wasomi wachache hawataki kuelewa ufisadi wa CCM;

Zaidi tuelimishe watu.
 
Back
Top Bottom