Dalili 10 za mwanamke asiyekupenda

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
Kwanza ifahamike mapema ninapozungumza dalili za asiyekupenda kwa dhati, sina maana nachonganisha watu katika ndoa zao, ila kuwatanabahisha kaka zangu kugutuka katika maisha yao ya kila siku, kumekuwa na ulahai wa hali ya juu katika ndoa nyingi hapa kwetu Zanzibar na hii yote inachangiwa na ugumu wa maisha kwa ujumla.

Nitajaribu kuziweka bayana dalili za Mwanamke asiye kupenda kwa dhati lakini hii haimaaanishi kuwa ufarakano katika mapenzi yenu bali ukae na kufikiri na kuyapima kwa kina haya ninayoyaandika humu isiwe kuporotoka na kuanza mtafaruku.

1 : Hataki kuambatana na wewe katika matembezi na kama ikiwa lazima anakuwa mtu wa masharti mara akuambie tangulia nakuja au kutembea nawe kwa mbali.

2: Anapata kigugumiza kukutambulisha kwa rafiki zake na jamaa zake.

3: Haonyeshi kubana matumizi kwa ajili ya maendeleo, kwake ni kufuja na kwenda mbele na huwa mfujaji mkubwa wa pesa na anapokosa kununa kabisa.

4: Anaahirisha kukutana na wewe mara kwa mara, tena bila kukueleza sababu za msingi, au kukutungia uongo wa dhahiri.

5: Anapokuwa akitoa maelezo ya mwanamme amtakaye sifa zake zinakuwa hazilingani na wewe, kwa mfano atakwambia napenda mwanamme mwenye mwili mkubwa , sifa ambazo wewe huna.

6: Hacheki kwa furaha, hata kama ukimchekesha haonyeshi furaha ya moyoni, ukimwambie twende tukatembee forodhani atakujibu ''Aaah, nimechoka mie nipo nyumbani'

7: Huwa hana wivu kabisa, hudiriki hata kukushawishi uwende Disco peke yako.

8: Hasamehi na kusahau, kosa la mwaka juzi analijengea hoja.

9: Humsisimui katika mambo ya faragha.

10: Mwepesi wa kutoa kauli ya TALAKA, ''kama vipi bora kila mtu akae kivyake vyake'' tena hataki kuambiwa ukweli na anapotokea akaambiwa hujitetea kwa kumtaja mwanaume mwingine '' Mbona Al-Udii (si jina halisi) anamfanyia hili , hamfanyii hivi mkewe''
 
MziziMkavu nawe ukisha gunduwa hayo yote ya kukosa amani ndani ya nyumba hamkai mkayazungumza tu...!
 
hazi aplly..
wanaume tukichoka tunasema tu,
mama eh tuachane,nimechoka.
 
hazi aplly..
wanaume tukichoka tunasema tu,
mama eh tuachane,nimechoka.

Mhh! Haya bwana... naona avatar zinabadilika kila uchao ndio matokeo ya lile tangazo kule kwa wakubwa nini? akipatikana nijulishe naweza kuwa matron....:)

Annina
 
akikosekana...
hata wewe utaziba pengo...
karibu.....
 
akikosekana...
hata wewe utaziba pengo...
karibu.....

Boss, I'm sorry but I hv to say this, kwa kauli hii (ya hapo kwa red)itakuwa ngumu sana hata kama mazingira yangeruhusu.......! Sikubaliani na wazo la kuwa second best - NIMEKATAA.

ha ha ha ha
how do u know u are second best?
 
Kwamba ukikosa umtakae........waswahili wanasema simba akikosa nyama hata nyasi anakula.......sipendi kuchukua nafasi ya nyasi!

Annina

labda we ndo nyama yenyewe hasa...
niliyokuwa naitafuta...
 
how????
nakutisha tena??????

Jinsi nilivyokuwa elevated kwa kasi ya ajabu kutoka second best mpaka chaguo la kwanza! Kwa flexibility uliyoonyesha nahofia wengine wakilalamika watakuwa elevated pia

hakuna wengine
jihakikishie nafasi yako baby....
need i say more?????
 
Kwanza ifahamike mapema ninapozungumza dalili za asiyekupenda kwa dhati, sina maana nachonganisha watu katika ndoa zao, ila kuwatanabahisha kaka zangu kugutuka katika maisha yao ya kila siku, kumekuwa na ulahai wa hali ya juu katika ndoa nyingi hapa kwetu Zanzibar na hii yote inachangiwa na ugumu wa maisha kwa ujumla.

Nitajaribu kuziweka bayana dalili za Mwanamke asiye kupenda kwa dhati lakini hii haimaaanishi kuwa ufarakano katika mapenzi yenu bali ukae na kufikiri na kuyapima kwa kina haya ninayoyaandika humu isiwe kuporotoka na kuanza mtafaruku.

1 : Hataki kuambatana na wewe katika matembezi na kama ikiwa lazima anakuwa mtu wa masharti mara akuambie tangulia nakuja au kutembea nawe kwa mbali.

2: Anapata kigugumiza kukutambulisha kwa rafiki zake na jamaa zake.

3: Haonyeshi kubana matumizi kwa ajili ya maendeleo, kwake ni kufuja na kwenda mbele na huwa mfujaji mkubwa wa pesa na anapokosa kununa kabisa.

4: Anaahirisha kukutana na wewe mara kwa mara, tena bila kukueleza sababu za msingi, au kukutungia uongo wa dhahiri.

5: Anapokuwa akitoa maelezo ya mwanamme amtakaye sifa zake zinakuwa hazilingani na wewe, kwa mfano atakwambia napenda mwanamme mwenye mwili mkubwa , sifa ambazo wewe huna.

6: Hacheki kwa furaha, hata kama ukimchekesha haonyeshi furaha ya moyoni, ukimwambie twende tukatembee forodhani atakujibu ''Aaah, nimechoka mie nipo nyumbani'

7: Huwa hana wivu kabisa, hudiriki hata kukushawishi uwende Disco peke yako.

8: Hasamehe na kusahau, kosa la mwaka juzi analijengea hoja.

9: Humsisimui katika mambo ya faragha.

10: Mwepesi wa kutoa kauli ya TALAKA, ''kama vipi bora kila mtu akae kivyake vyake'' tena hataki kuambiwa ukweli na anapotokea akaambiwa hujitetea kwa kumtaja mwanaume mwingine '' Mbona Al-Udii (si jina halisi) anamfanyia hili , hamfanyii hivi mkewe''

Kwa kifupi yuko na wewe kwa ajili tu ya maslahi, au kwa kuwa hana mwanaume mwingine anayemtaka yeye. Siku akimpata anasepa! Cha ajabu unakuta mwanaume hizi dalili zote anaziona kwa mwanamke aliyenaye ila unakuta bado anamng'ang'ania kwa kuwa anampenda!

Wahenga walisema;
''Giving someone all your love is never an assurance that she/he will love u back. Don’t expect love in return, just wait for it to grow in his/her heart but if it doesn’t, be content it grew in yours''. Mwisho wa kunukuu!!
icon10.gif
 
Back
Top Bottom