dalai lama akaribishwe tanzania

Andrew Nyerere

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
3,007
2,429
Mkutano wa amani uliopangwa kufanyika SA ,umefutwa,kwa ajili Serkali ya SA haitaki Dalai Lama aende kule. Kwa nini SerIkali ya Tanzania isipendekeze kwamba huu mkutano ufanyike hapa Dar es Salaam? Ni ajabu kuona kwamba SA ambayo inaongoza Afrika kwa ujambazi,na labda pia kwa ukimwi,inaweza kumfukuza kiongozi wa dini. Afrika ina matatizo mengi ya vita,kwa hiyo siyo vizuri kuwazuia viongozi wa dini kuja hapa. Afrika pia ina matatizo ya mmong'onyoko wa maadili. Tuko tayari kumsikiliza kiongozi yoyote wa kidini,kama anao ushauri wowote. Benedict XVI alikuwepo hapa wiki iliyopita. Vatican inasikitika kwamba maneno aliyosema kuhusu Afrika hayakusikilizwa,badala yake umetokea ubishi mkubwa kuhusu maneno yake aliyosema kuhusu condom. Pope Benedict aliongea kuhusu matatizo ya Afrika. Serikali ya SA inasema kwamba Dalai Lama akienda kule,basi watu wataongea kuhusu Tibet,na hiyo ni makosa,kwa sababu watu wakiwa Afrika,wanapaswa kuongea kuhusu Afrika. Hawa Waaafrika Kusini walipokuwa wanapigania uhuru,matatizo yao yalikuwa yanazungumzwa Duniani kote. Hivyo ndivyo walivyopata ushindi,pamoja na juhudi zao wenyewe. Dalai Lama pia anaweza kuzungumzia kuhusu Darfur na Somalia,lakini kama nchi yake haiko huru,matatizo yake lazima yaje kwanza. Miaka yote hapa Tanzania tulikuwa tunapinga udhalimu uliokuwa unafanyika Vietnam. Ile vita ilipokwisha tulikuwa na furaha kubwa.Nakumbuka Ndugu Kawawa aliitisha mkutano wa hadhara Jengo la Umoja wa Vijana wa CCM[TANU],kuwaeleza vijana kwamba,''Vietnam,vita imekwisha jana."'
Kwa hiyo itakuwa vizuri kama Rais Kikwete atamuagiza Waziri Membe amualike Dalai Lama na hawa watu wengine watukufu waje hapa Dar es Salaa wafanye huo mkutano,wasitafute refund ya ticket zao,badala yake waje Dar es Salaam. Labda pia tunahitaji kumwomba Balozi wa China ili tuweze kumualika Dalai Lama. Kuna mambo mengi sana kuhusu China ambayo hatuyafahamu.Tunaambiwa kwamba watu 35 milioni wamekihama Chama cha Kikomunisti. Watu wana manung'uniko mengi sana kule China.
Halafu mafundisho ya Dalai Lama yanaweza kuisaidia Afrika. Kwa sababu yule Guru Padmasambava,aliyeipeleka dini ya Budha Tibet,alipofika kule alikuwa na kazi kubwa ya kuzikabili imani za kishirikina. Kulikuwa na matatizo makubwa ya ushirikina,na Padmasambava aliitwa aende kule. Alikuwa anaishi India au Burma. Ninaposema ushirikina nina maana ushirikina. Huyu Padmasambava alikuwa ni mtu ambaye makazi yake ni makaburini. Akichoka kuishi katika makaburi sehemu fulani,anaenda kuishi katika makaburi sehemu nyingine. Kwa hiyo watu wa Tibet walipokuwa na matatizo na uchawi,wakamwita,kuona kama anaweza kuwasaidia. Dini yao ya Tibet,ambayo inaitwa ''Lamaism'',sasa hivi ni mchanganyiko wa dini ya Budha na dini ya asili. Halafu pia inafaa kueleza Dalai Lama ni mtu gani. Dalai Lama ni kiongozi wa Tibet ambaye habadiliki. Hakuna kura za kumchagua Dalai Lama. Hakuna Palace Coups. Dalai Lama peke yake ndiye anayeiongoza Tibet. Hiyo ndiyo Katiba yao. Dalai Lama anaongoza mpaka siku ya kufa kwake. Akifa mwili wake unahifadhiwa. Halafu imani yao ni kwamba roho yake inaingia katika mwili wa mtoto mdogo. Kwa hiyo wale Lama,ambao ndio mapadre wa Tibet,wanazunguka nchi nzima kutafuta Dalai Lama ametua wapi. Wakimpata huyo mtoto,ndie wanampeleka Potala,ambayo ndiyo Ikulu yao,kuwa Dalai Lama. Huyu ni mtoto bado,inabidi aende shule,halafu baadaye anakuwa Dalai Lama. Ndiyo maana huyu Dalai Lama wa sasa,anaitwa Dalai Lama wa 14,ina maana mabadiliko ya uongozi yamefanyika mara 14. Hata hivyo,inaaminiwa na Watibeti wengi kwamba Dalai huyu siyo reincarnation ya Dalai Lama wa 13. Hata yeye mwenyewe amesema hivyo,kwamba siyo reincarnation wa ''Chenrezi'',ambalo ndilo jina la Dali Lama wa 13. Huyu Dalai Lama alichaguliwa bila kujali usahihi wa chaguo. Alichaguliwa kuwafurahisha Wachina. Ina maana huyu Dalai Lama wanayempinga Wachina,alichaguliwa kuwafurahisha wao.
Kwa hiyo nadhani huu mkutano ni bora uletwe hapa Kempiski,wale Waskandinavia,waambiwe waulete huu mkutano hapa. They should be given alternative venues,if they should choose so. Huu ni mkutano wa amani. Wars cost money. Na hawa Wachina tumewaona jana wanaomboleza kifo cha mmoja wao aliyeuawa kikatili na majambazi. Hayo ndioy maadili tunayozungumzia.. Wars cost money,na sasa hivi kuna Financial Crsis Duniani. Pia siyo rahisi kuziuza kwa wananchi vita ya nchi moja ya Afrika kupigana na nchi nyingine ya Afrika.Nilikuwa nasoma jana katika gazeti moja la Marekani,kwamba kesi za litigation Marekani siku hizi zimekwenda out of fashion kwa ajili ya hii Financial Crisis,na walikuwa wanauliza lawyers wale wanaozitegema hizi kesi watafanya nini. Kwa hiyo inashangaza kuona Bw. Reginald Mengi na waandishi wa habari wanadaiana hela,wakati huu wa Financial crisis.
 
sababu zilizo wafanya sa kumnyima visa dalai lama ni hizo hizo ambazo zinaifanya jamhuri hii isimwalike huyo muumini (dalai lama). hapa kwetu juzi tu tulikuwa na ugeni kutoka china (sikumbuki alikuwa waziri mkuu au rais kwani sikufuatilia); sa hakwenda, na wameona ni umuhimu wa uhusiano wao na china kuliko wa tibet!

macinkus
 
Back
Top Bottom