Daladala za Arusha zagoma

Chimemena

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
1,376
451
Jamani hapa Arusha leo daladala zote zmegoma ili kushinikiza madai ya madereva na wamiliki kwa selikal hususan traffic. Yaani ni karaha juu ya udhiha hakuna daldala since saa 11 alfajili.
 
Wakuu mlioko Arusha kuna mgomo wa magari ya abiria'hiece' kwa wale wa njia ya moshi arusha unaweza kujionea umati wa abiria kwenye vituo.
 
Mji wa Arusha lea ni balaa tupu, usafiri wa watu wa kawaida comon man hakuna. Watu wa daladala wamegoma hivyo kwenda kazini leo itakuwa shida. Madai yao nikwamba wananyanyaswa na trafiki polisi na kuonewa watu wao wanawekwa ndani bila sababu. Bila shaka imechangiwa na frustrations za maisha, kupanda ovyo kwa mafuta na gharama za maisha yote hiyo inachangia!!!!!! Ngoja tuone hadi mchana itakuwaje???????????
 
Daladala zote leo tangt alfajir zmegoma kufanya trip ili madai yao yaweze kusikilìzwa. Leo walalahoi ni full walking.
 
Wadau, huku barabarani naona mkusanyiko mkubwa wa watu na pikipiki za kutosha. Nilisikia kutakuwa na mgomo, je ndio huu? shida ni nini?
 
Haya! Jamani jamani! Kumekucha! Mlioko on line town! 2peni yanayoendelea. Ndiyo Tz ye2 hiyo.
 
Wadau, huku barabarani naona mkusanyiko mkubwa wa watu na pikipiki za kutosha. Nilisikia kutakuwa na mgomo, je ndio huu? shida ni nini?
Si umeona eeh?
Kwa ufupi hali ni mbaya sana barabarani.
Abiria wanapata shida isiyo kifani, maana ni route-march iliyoenda shule!
Sababu:
Madereva na makondakta wa vifodi wanalalamikia suala la wao kukamatwa kila wakati na kuswekwa ndani kwa makosa yasiyo na maelezo ya kuridhisha!
Mfano, dereva akishusha abiria mahali, anakamatwa na kupigwa faini au kutupwa selo, wakati barabara za Arusha nyingi hazina vituo official!

Kuna madereva wasiopungua 5 wapo Kisongo Gereza la mkoa, na hivyo madereva wote wameamua kuwa hawatatoa huduma ya usafiri hadi hao wenzao watakapoachiliwa huru bila masharti yoyote!
 
kwa kweli polisi wa barabarani Arusha huwa ni waonevu sana......sasa madhara yanaenda kwa wananchi.........watoto wa shule ndio wanaoteseka zaidi........
 
Nikiwa kwenye usafiri binafsi ASUBUHI YA leo, maeneo ya JR nimeshuhudia gari, COASTER ikipopolewa mawe na kuvunjwa vunjwa vioo, na kuna baadhi ya abiria wameumizwa kwa mawe, kisa amepakia abiria!

Kwa ufupi ni kwamba kila eneo la kituo kumewekwa MATEJA wanaohakiki utekelezaji wa azma yao, na vijana hao hawaelewi kitu, walishaajikatia tamaa ya maisha kiasi wanaona kuangusha tofali kwenye windscreen ni kazi ndogo!
 
Yani huku ni tabu tupu..coaster za moshi arusha hazitaki abira wa kushukia njiani hivyo leo ni kwa miguu tuu..
 
kwa kweli polisi wa barabarani Arusha huwa ni waonevu sana......sasa madhara yanaenda kwa wananchi.........watoto wa shule ndio wanaoteseka zaidi........
Hakika watoto wa wa shule za Saint Kayumba Kiswahili Medium wako kwenye wakati mgumu sana. Leo barabarani zinatamba gari za watu binafsi, gari za rangi ya Njano za shule za Watakatifu(St. PakaJimmy) na bodaboda!
 
Mji wa Arusha lea ni balaa tupu, usafiri wa watu wa kawaida comon man hakuna. Watu wa daladala wamegoma hivyo kwenda kazini leo itakuwa shida. Madai yao nikwamba wananyanyaswa na trafiki polisi na kuonewa watu wao wanawekwa ndani bila sababu. Bila shaka imechangiwa na frustrations za maisha, kupanda ovyo kwa mafuta na gharama za maisha yote hiyo inachangia!!!!!! Ngoja tuone hadi mchana itakuwaje???????????

Elezea vizuri basi, traffic police wanawanyanyasa kivipi? Je wanawekwa ndani bila makosa? Wakati mwingine tuwe na mawazo chanya, maana ajali zikizidi tena mtawalalamikia police!!!!
 
katika mji wa Arusha leo asubuhi watu wanaotumia daladala kama usafiri wa kuwapeleka ktk shughuli zao wamejikuta wakikumbana na adha ya kutokuwa na usafiri baada ya madereva hao kugoma kutoa huduma hio wakishinikiza wenzao waliokamatwa na polisi wa barabarani wawaachilie wenzao. Mji mzma wa Arusha raia wamebidi watumie boda boda na wale wasio na uwezo wa kumudu usafiri uwo wa bodaboda imewabidi watembee umbali mrefu kufika makazini na shuleni.
Nawasilisha
 
Ni poa tu nimepata kisingizio cha kufanya mazoezi leo asubuhi nahisi wakiendelea wiki hivi nitakua fiti mbaya...
 
Duuuh poleni sana wana arusha. wakigoma wanafunzi vyuoni eti CDM wanawachochea. Je, madaladala men wanachochewa na CDM pia? magamba tatueni matatizo sio kuendekeza politik za visingizio bana.
 
katika mji wa Arusha leo asubuhi watu wanaotumia daladala kama usafiri wa kuwapeleka ktk shughuli zao wamejikuta wakikumbana na adha ya kutokuwa na usafiri baada ya madereva hao kugoma kutoa huduma hio wakishinikiza wenzao waliokamatwa na polisi wa barabarani wawaachilie wenzao. Mji mzma wa Arusha raia wamebidi watumie boda boda na wale wasio na uwezo wa kumudu usafiri uwo wa bodaboda imewabidi watembee umbali mrefu kufika makazini na shuleni.
Nawasilisha

Niko maeneo ya Posta Meru,kuna fujo fujo,,,,wanafunzi wengi na watu wanapiga kelele sana!Naona km kutatokea fujo hapa le japo polisi wameishaanza kupita na washawasha zao.
 
Preta! Mambo vp? Hali ni tete sana hasa ktkt ya mji kwani mi mwenyewe nipo na usafiri wa binafsi ila hali ni mby kwn kuna jam ya kutisha kuanzia hapa stend ya mkoani,line police na huku Goliondoi road haki mi naona hiace ni muhimu kuwepogo sana na k2 kingine nimeona ni kwamba nimegundua ya kwamba wa2 wanakuwaga na magari sana yani kuna familia zingine zimeamua kila mtu atoke na gari. Mambo ni mazito.
 
Umeme shida,chakula ni haba,maji tabu,huduma za afya ovyo,usafiri kimeo,.....na hii ndio nchi yetu ya ahadi,..mmmmmh
 
Back
Top Bottom