Daladala yaua, yajeruhi 27

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
ABIRIA amekufa papo hapo na wengine 27 kujeruhiwa katika ajali jijini Dar es Salaam baada ya gari dogo kugongana na daladala katika makutano ya Barabara ya Mandela na Chang’ombe, Temeke.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 4.25 usiku na kuhusisha gari dogo lenye namba za usajili T361 AWC ambalo halijajulikana aina yake na daladala lenye namba T21 AZB Toyota Civilian.

Misime alisema gari hilo dogo ambalo lilikuwa likiendeshwa na dereva asiyefahamika, akitokea Tazara kwenda Kurasini huku daladala hilo likitokea Maduka Mawili kwenda Chang’ombe Polisi.

Alisema katika ajali hiyo, mwanamume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 aliyekuwa ni abiria katika daladala hilo, alifariki dunia papo hapo na abiria wengine 27 walijeruhiwa; wakiwemo 24 waliotibiwa hospitalini na kuruhusiwa huku watatu wakilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Aliwataja waliolazwa Muhimbili kwa matibabu zaidi ni Shukuru Seif (35), mkazi wa Temeke Mikoroshini, Shaban Kassim (36) wa Tandika na Max Cleofes (38).

Maiti amehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke.

Alisema madereva wote walikimbia baada ya ajali na polisi wanaendelea kuwatafuta huku magari hayo yakiwa katika Kituo cha Polisi Chang’ombe.
 
Toyota Civilian!!!!!!!????????????????????????
All in all bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe.
 
Kuna mkoa wa Temeke????

Nwy pole nyingi kwa majeruhi na RIP kwa aliyeondoshwa duniani!!!Hizi ajali sijui zitapungua lini!
 
Kuna mkoa wa Temeke????

Dar-es-Salaam imegawanywa katika mikoa ya Kipolisi, kwa hiyo, Temeke, Ilala, Kinondoni ni Mikoa (Kiutawala ndani ya Jeshi la polisi). Vilevile TANESCO nao wana-operate kwa hadhi ya mikoa kwa Temeke, Kinondoni, na Ilala. Hii ni maalumu tu kwa Dar-es-salaam kutokana na ukubwa na wingi wa watu.
 
Back
Top Bottom