Daladala yachomwa moto na dereva wa bodaboda Mbezi

Filipo

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
9,342
5,536
Daladala iliyokuwa imebeba abiria maeneo ya mbezi beach (makonde) imechomwa moto na madereva wa bodaboda baada ya kumgonga mwenzao na kufariki hapohapo wakati dereva alipokuwa anajaribu kukwepa gari iliyokuwa ina'overtake' lori na kuzidi upande wake hivyo kulazimika kuzidi upande wa kushoto na kuigonga pikipiki hiyo. Dereva wa daladala amelikimbia na kuliacha gari ndipo madereva wa bodaboda kuamua kuichoma moto kwa hasira.
Source: clouds fm breaking news
 
Watanzania tukubali tusikubali hatuna serikali,tumeachwa kama wakiwa tumalizane wenyewe ikibidi hata kwa kuuwana...hii ni hatari!!
 
Inasemekana polisi wamefika eneo la tukio. Wamejaribu kurudisha hali ya amani na sasa pako shwari ila gari inaendelea kuungua.
 
Aisee! Hawa jamaa wa TOYO & BODABODA ni soo,jana tu kuna mwizi aliiba toyo yani kilichompata bila shaka udongo ndiyo ina siri hiyo.
 
Madereva wa bodaboda wapo inferior sana na huwa wanahisi kudharauliwa na madereva wa magari. Ndio maana wakaghadhibika namna hiyo!
 
Hilo bifu hata huku kwetu ughaibuni lipo saana mpaka linatisha. wahusika wa usalama wasipoangalia!!!!!!!!!!! mimi sijui
 
Sasa tukienda kwa staili hiyo nadhani bodaboda karibu zote zingekwisha teketezwa kwa moto kwa sababu bodaboda hizi ndo zinaongoza kwa kuua na kuvunja watu miguu na mikono. Je sahihi kuwa pikipiki hizi zipigwe kiberiti na wananchi pindi ajali inapotokea?
 
Hii tabia ya magari kuchomwa na madereva wa 'boda boda' inaanza kuzoeleka njia hii ya Bagamoyo...few months back madereva wa boda boda walichoma Toyota LandCruiser Prado pale Tegeta Chanika kwa kumgonga dereva wa boda boda ikiwa makosa ni ya dereva wa boda boda mwenyewe!
 
Hii tabia ya magari kuchomwa na madereva wa 'boda boda' inaanza kuzoeleka njia hii ya Bagamoyo...few months back madereva wa boda boda walichoma Toyota LandCruiser Prado pale Tegeta Chanika kwa kumgonga dereva wa boda boda ikiwa makosa ni ya dereva wa boda boda mwenyewe!

Nchi yetu ni uwanja wa fisi....kutokana na kukosekana kwa wasimamizi wa sheria zetu ili kulinda mali na usalama/uhai wa Watanzania
 
nakumnbuka siku moja wanabodaboda walitaka kulichoma gari la jamaa yangu mmoja hivi kumbe jamaa walikuwa wamemfananisha tu jamaa alitoa silaha ndipo jamaa waliporudi nyuma na ndiyo manusura yake baada ya polisi nao kuingilia. hawa ndugu zetu ni hatari sana
 
Hao boba wangekomeshwa na wao jins life ilivyotight wanamchomea mtu gari yake?tena wawezakuta ndo hiyo ya ngama inamuwezeshea life sasa sjui akale wapi?
 
Back
Top Bottom