DALADALA Miaka ya 80, Nauli ni USD 1 au TSH 5 (Gwala)

shillingi tano haikuwa inaitwa gwala bali ni dala ni ndio chanzo cha kuitwa magari hayo daladala
 
shillingi tano haikuwa inaitwa gwala bali ni dala ni ndio chanzo cha kuitwa magari hayo daladala
Enzi hizo, madaladala yalikuwa ni pick ups au canter inayobeba watu kinyume cha sheria na kuwapa kamisheni traffic, uda ilikuwa shilingi moja, mtoto thumni.... ukitaka chapchap unatoa dala.
 
Umenikumbusha mambo ya vilakshari hasa DAR (Vilianzia pugu to kkoo). Nakumbuka chache km love and peace, cassanova.
 
Ahsanteni sana vijana wa zamani coz mimi nilikuwa najiuliza kwanini haya mabasi yanaitwa daladala? Leo ndo nafahamu cnanzo chake ni nini
Lakini natamani hizi hoja angeziona Gavana wetu ingesaidia kujua mahali tulipo sasa kwani thamani ya shilingi yetu kwa sasa inahuzunisha
Nawasilisha
 
Enzi hizo, sikinde wakipiga shoo, unazuka na mabinti vigori wawili. mapulizo ya wakubwa tulikuwa hatuyajui jamani, ni enzi za starehe kweli kweli.

hahahahahaha umenichekesha kweli. Kumbe kuna mapulizo ya wakubwa.........................
Vijana wa zamani mna mambo nyie!!!!!!!!! Umenifanya nicheke asubuhi asubuhi
 
Tafadhari nitake radhi bwana, enzi hizo wanafunzi tunapanda daladala BUREEEEEE. Nitakukumbusha na mabasi ya Ikarusi (Kumbakumba)
Enzi gani hizo? nadhani hiyo picha ya basi uliloliweka ni kabla ya daladala ambapo usafiri dar ulikuwa ni wa UDA tu na nauli shilingi 1 mtu mzima na senti 50 watoto
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom