Vin Diesel
JF-Expert Member
- Mar 1, 2011
- 9,088
- 6,368
Kwenye usafiri raia hawana ustaarabu kabisa.
Gari yenyewe ni bugati au vitz,star let!?
Safi uporoto, nipo tu ila kwa tahadhari coz sipendi kueleweka tofauti na ninavyomaanisha.aine mambo umeadimika siku hizi.
Mi sipendi daladala za muhimbili watu tunagombania mlangoni wengine wanapitisha vikapu madirishani ukiingia ndani siti zote zina vikapu inabidi usimame pamoja na kuchafuliwa nguo/viatu mlangoni.
<br />hi bro let me try to drill ur words..! sio vizuri mwana kumwambia mwenzio hayo uliyo mwambia nadhani hata wewe unaona kua hauko sawa au ni viipi mkubwa..!
Jamani bado tu unayo moyoni ? pole haikuwa dhamira yangu kukukwaza, naomba tuwe marafiki wa keyboard.Safi uporoto, nipo tu ila kwa tahadhari coz sipendi kueleweka tofauti na ninavyomaanisha.Kwa ujumla siku hizi hakuna cha mwenge, mbagala au mbezi, kugombea daladala ni kila kona ya Dar, utakuta wengine wanapita hata kwa dereva!!! na wakati mwingine utakuta abiria wenyewe ni wachache sana ila ni mazoea tu
wana jf last week nilikuwa natoka job na kusimama na sista du mmoja pale posta kituoni tukisubiri gari ya mbezi ya kimara, ilipokuja watu waligombea kinoma mie mwenyewe ilibidi nikae pembeni ili kunusuru afya, usalama na ustaarabu wangu. Lakini kutahamaki nilimuona yule sister du amepata siti tena ya dirishani, duh niliishiwa nguvu na kushangaa kuona aliwezaje kuingia pale mlangoni angali alionekana very soft and civilized. Ilibidi tu nitembee hadi akiba ili nizunguke na bus. Toka siku hiyo niko radhi hata nikope lakini nihakikishe anytime my car is working. Kweli ukitaka uone usumbufu wa daladala dar subiri siku uharibikiwe na gari.

masista duu wa mbagala kiboko, wanavaa mapensi ndan kwa shughuli ya kupitia dirishani.ni zaidi ya maninja