Daktari wa rais Kikwete apanda cheo

Status
Not open for further replies.
Hongera sana Dr Janabi! Ni muhimu ukatuwekea bayana hali ya kiafya ya Kikwete


mi sidhan anastahili kuwa profesa...kama umekuwa dk wa raisi ukadiriki kudanganya watanzania zaidi ya million kadhaa afya ya raisi wao,,mpka yanamkuta tena anadondoka anashindwa\ kuweka wazi presidaa anaumwa nini jiulize udk ameshindwa kuwa mkweli tena kwa kukaa na press na kutudanganya anachojua..leo hii u PROF SI ATATUDANGANYA KUPITA KIASI...LOH USHAUPATA SINA BUDI KUKUPONGEZA ILA KWA HILI LA RAIS JIREKEBISHE KWANZA
 
muungwana ameshauriwa na 'dr" wake kuwa hewa ya pale jangwani ni chafu sana ndio maana anaanguka anguka akihutubia pale kwahiyo msijemkashangaa mkutano wake wa mwisho wa kampeni akahamia uwanja wa taifa!!

si arudi pale pale atumie mask....taifa mbali jamani wengine wa kibamba tutshindwa kumsikilzia
 
Kilaza huyu mbona JK anaanguka kila siku ina maana maradhi ya Jey keyi hayatibiki?? Asiondoke kwenda USA mpaka baada ya 31 oct
 
kikwete alimchagua kwa kuwa ni mtafiti katika maswala ya ukimwi..si wote mnajua JK ana umeme ana ameshabadilisha damu mara nyingi tu...
 
Congrats Prof... Umefanya kazi nzuri na nakuombea uendeleze focus kwenye research kila utakapopata nafasi... I pray that after this position you are having now, ufungue center nzuri sana ya kusaidia wagonjwa hapa Tz.. wahsauri university mje mfanye kazi hapa we need your skills mno na opportunity za research nadhani unajua zipo kaisi gani

You are a good teacher, humble

Hayo ya siasa naweka kando mkuu
 
Congrats Prof. Janabi,
You are doing a great job monitoring the defective and thinned jugular vein that takes blood to the head of our dear president. Had it not been you and your expertise surely we would be speaking in a different languages now.

I hope your further research will sufficiently help in ensuring that we have someone healthy upto 2015.


Sorry Caren, Does jugular vein takes blood to or from the head?
 
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425




PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Daktari wa Rais Kikwete awa Profesa

Daktari Mkuu Binafsi wa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Janabi amepandishwa daraja la usomi wa utibabu na kuwa Profesa wa Chuo cha Utibabu cha South Carolina (MUSC) kitengo cha magonjwa ya moyo nchini Marekani kuanzia Oktoba Mosi, mwaka huu, 2010.

Dk. Janabi (47) amekubali kupandishwa daraja hilo ambako atakuwa Profesa Mshiriki wa Tiba katika Idara ya Utibabu, Sehemu ya Tiba ya Moyo, kwenye chuo hicho kilichoko mjini Charlestown.

Hata hivyo, Dk. Janabi ambaye ni mmoja wa Watanzania wachache wenye sifa na ujuzi mkubwa zaidi katika udaktari, anaendelea kuwa Daktari Mkuu Binafsi wa Rais Kikwete.

MUSC ni chuo kikuu kikubwa zaidi na maarufu zaidi kuliko kingine chochote katika Jimbo la South Carolina na anakuwa Mtanzania wa kwanza kupata utambuzi na heshima ya namna hiyo kwenye chuo hicho ambacho amekuwa nao kikazi tangu mwaka 2003.

Dk. Janabi alipata Shahada ya Uzamivu (PhD) mwaka 2000 nchini Japan katika fani ya magonjwa ya moyo. Mbali ya kuwa Daktari Mkuu Binafsi wa Rais Kikwete, mtaalam huyo wa magonjwa ya moyo pia ni mtaalam bingwa wa masuala ya moyo kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Mkufunzi wa Heshima katika Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi cha Muhimbili (MUHAS).

Dk. Janabi pia ni Mwanasayansi Mwandamizi katika Utafiti wa Chanjo ya Ukimwi na Mkurugenzi Mwakilishi (Tanzania) wa Taasisi ya Kimataifa ya Madaktari wa Africa.

Amekuwa Daktari Mkuu Binafsi wa Rais Kikwete tokea 2006.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.


22 Oktoba, 2010



aA PIECE OF CRAP!OF ALL TIME HE HAD TO BE PROMOTED ON THIS MONTH OF ELECTION,,SO CCM THINK THIS WILL BOOST THEIR PRESIDENTIAL CAMPAIGN..ISNT THIS KURUGENZI YA MAWASILIANO SALVA RWEYEMAMU RELATED????I DOUBT IT..WHERE IS THE RECIPROCAL WA ALAFU UNAANGUKA OVYO..ALIKUWA WAPI KUTOA USHAURI??CORRESPONDENCE FROM USA???WELL...HELL...HAYO NI MAWAZO MGANDO SABABU HAKUNA ANYETAKA KUJUA KUWA UNA DAKTARI BINGWA??
 
a piece of crap!!of all time he had to be promoted at this month of the year...can anyone believe anything thats salva rweyemamu related????well....hell dont mean shit to me as long as kikwete keeps on collapsing...is this a campaign???
 
Hongera sana Prof, sasa kati ya wewe na Sheikh yahya nani anasikilizwa zaidi?nani anakubalika kwa presidaa, tusimlaumu prof kwa kugua kumbe yakha ndo top
 
Luluka
kulikoni ku-like post yangu leo? Hi kitu ya 2010 dah!

Ila naona sasa patient amepanda kutoka alipokuwa hadi kuwa Professor.

Ubishi unasaidia muda mwingine
 
Congrats Prof. Janabi,
You are doing a great job monitoring the defective and thinned jugular vein that takes blood to the head of our dear president. Had it not been you and your expertise surely we would be speaking in a different languages now.

I hope your further research will sufficiently help in ensuring that we have someone healthy upto 2015.

Aisee nimecheka hadi basi, jamani JF nimeamini inapunguza stress za maisha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom