Daktari Uingereza amfokea Cameron kwa kukiuka utaratibu Hosiptalini..

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,513
11,276
Daktari bila kujali nani yuko mbele yake ameamua kusisitiza juu ya kufuata Utaratibu waliojiwekea Hospitalini kwao..
David Cameron kwa kutambua kuwa walikosea, mara moja wakaomba radhi na kuheshimu alichosema Daktari..
Inavutia pale siasa zinapowekwa kando na taaluma ikaheshimiwa..
Labda viongozi na wataalamu wetu watajifunza kitu hapa...

Kwamba haijalishi wewe ni nani, ni lazima uheshimu taratibu na taaluma za wengine......
Na kwamba haijalishi mtu ni nani ni lazima umsisitize kufuata utaratibu kwa mujibu wa taaluma yako, usiruhusu Taaluma yako kupuuzwa na wanasiasa....

Last edited by a moderator:
Hii si heshima kwa kiongozi mkuu wa nchi. Huku ni kukosa adabu kwa huyu Dakitari. Kuna mazingira ya kuweza kufikisha ujumbe na siyo kuropoka kama alivyofanya huyu dakitari. Kumbuka mamlaka aliyonayo kiongozi mkuu wa nchi ndiyo yanayobeba uhalisia na ustawi wa jamii husika, na ndiyo maana ikitokea kafanya vizuri haohao (mmoja wapo ni huyo Dakitari) wanamsifia na akikosea wanamuadhibu kwa kura. Nadhani huyo dakitari ataja kiona cha moto (kimya kimya).
 
Kila mtu aheshimu sehemu za kazi za wenzake, sio basi wewe umekuwa mkuu wa nchi kila sehemu unaingia bila ya kufuata utaratibu. BIG UP DR
 
Nimeipenda hii,safi sana na ndiyo maana wenzetu wameendelea.Hakuna kuchekeanachekeana,ni kuwajibika tu!
 
Hii si heshima kwa kiongozi mkuu wa nchi. Huku ni kukosa adabu kwa huyu Dakitari. Kuna mazingira ya kuweza kufikisha ujumbe na siyo kuropoka kama alivyofanya huyu dakitari. Kumbuka mamlaka aliyonayo kiongozi mkuu wa nchi ndiyo yanayobeba uhalisia na ustawi wa jamii husika, na ndiyo maana ikitokea kafanya vizuri haohao (mmoja wapo ni huyo Dakitari) wanamsifia na akikosea wanamuadhibu kwa kura. Nadhani huyo dakitari ataja kiona cha moto (kimya kimya).

siyo bongo hapo mazee,manake bongo ukiwa mwenyekiti wa mtaa tu,basi ushakuwa kamungu mtu fulani hivi,mpaka nzi utataka wakuheshimu.Utakuja kushangaa huyo daktari anapandishwa cheo hapo hospitalini!
 
fikra za kibongo ambako rais anasadikiwa km mungu. wenzenu proffesionals wanaheshimika saaana. na mara zote wanasiasa ndo waharibifu wa taratibu zetu.
 
Japokuwa ni demokrasia lakini dokta kajishushia heshima angeongea nao vizuri tuu.
 
Dah! Watu tunapenda news za kudhalilisha viongozi..
(hata kama they deserve it but saa ingine ni vizuri kupembua…)
The news is so exaggerated… nashukuru the clip ilikuwepo for when
I read I thought as in kweli kafokewa… Hey guys you call that kufokewa???
And wala sio kwamba the doctor was directly addressing Cameron,
there were a lot of other people there and as much as the doctor alimaka…
hakufoka… Hizi news hizi.. makes us not to trust them sources anymo'
 
Hii si heshima kwa kiongozi mkuu wa nchi. Huku ni kukosa adabu kwa huyu Dakitari. Kuna mazingira ya kuweza kufikisha ujumbe na siyo kuropoka kama alivyofanya huyu dakitari. Kumbuka mamlaka aliyonayo kiongozi mkuu wa nchi ndiyo yanayobeba uhalisia na ustawi wa jamii husika, na ndiyo maana ikitokea kafanya vizuri haohao (mmoja wapo ni huyo Dakitari) wanamsifia na akikosea wanamuadhibu kwa kura. Nadhani huyo dakitari ataja kiona cha moto (kimya kimya).

mawazo ya magamba hayo

kiongozi gani wa nchi anaongoza bila kujua utaratibu wa hata idara ndogo tu?? sasa akienda nyuklia department si anaweza kuanza kuharibu kila kitu

heshima za kipumbavu kama hizi zinaboa sana

a hospital is a divine place especially if we appreciate that souls are rescued there............ pooofffffff
 
siyo bongo hapo mazee,manake bongo ukiwa mwenyekiti wa mtaa tu,basi ushakuwa kamungu mtu fulani hivi,mpaka nzi utataka wakuheshimu.Utakuja kushangaa huyo daktari anapandishwa cheo hapo hospitalini!
Wewe ndugu yangu hufahamu, unajua wazungu hawapo kama unavyoweza kuzani. Suala la kuheshimiana lipo na sivyo kama unavyofikiria eti jamaa kapata ujiko, hapana, nao wanavisasi kama kawaida ila sema tu wenzetu bifu zao huwa ni bifu kweli wala si za kuuma na kupuliza.
 
eti sifahamu..sifahamu wazungu au?usinitishe wewe,mwenyewe nimetembea na dunia naijua vilevile na hao wazungu wako unaowaabudu.Wenzetu wanaheshimiana katika kazi zao,hakuna dharau hata kama unapiga deki ofisini,bosi na wafanyakazi wenzako watakuheshimu vizuri tu,tofauti na bongo mtu akiwa na kicheo mbuzi,basi ni dharau tu na kujiona kama mungu flani hivi.Ndiyo mana utakuta kiwanja bosi tajiri ana ukwasi wa kufa mtu,lakini yuko simple sana na anajichanganya na wafanyakazi wake mpaka huwezi kujua kama yeye ndiye bosi.Na akikosea akaingia anga zako,unampa ukweli na most of the time ata appreciate na kukuona kweli unawajibika na unaijua na kuipenda kazi yako.
Point hapa ni kwamba Cameron ameelewa kuwa amekosea na Dr kampa kubwa bila kumuangalia usoni.Kusema kwamba Cameron atamuadhibu huyo Dr ni fikra na hisia tu za kibongobongo!
 
Back
Top Bottom