Daktari na mwalimu nani zaidi?

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
Mara kadhaa tumeshuhudia makundi mbalimbali ya watumishi wa umma yakiingia mgogoro ma Serkali kubwa likiwa ni maslahi.
Nitumie nafasi hii kuongelea MADAKTARI na WALIMU. migoggo ya makundi haya mawili dhidi ya Serikali mara kadhaa imekuwa na sura tofauti husani hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na makundi haya. Nina miaka mingi sana sijashuhudia Walimu wakifikia hatua ya kugoma toauti ya Madaktari ambao mara kadhaa wameamini kuwa migomo ndiyo suluhisho la madai yao. Hii tafsiri yake ni nini? Je Madaktari ni muhimu zaidi ya walimu?. Inawezekana ni kweli kwa vile pamoja na kwamba wamefundishwa na walimu bado Mwalimu hurudi kwa Daktari huyo huyo ili kulinda afya yake. Je ulinzi wa uhai wa watu ni kigezo tosha cha Daktari kuwa nguvu zaidi ya mtumishi mwingine wa umma? Mbona inaonekana kama ilikuwa ni lazima Daktari azaliwe, ila asiye Daktari alizaliwa kwa makosa? Madaktari mkae chini na Serikali mpate suluhisho badala ya kutumia ubabe kwa vile mnajua mmebeba uhai wa watu. Hizo talanta kawapa Mungu. Muwe kama walimu, mtambue kuwa ninyi ni watoa huduma mliotumwa na mwenyezi Mungu kufanya kazi hiyo kwa alijua watakuwepo watu wana matatizo na suluhisho ni ninyi.
 
Hakuna zaidi Kwani wote ni muhimu...unazalishwa Na dokta then unafundishwa na mwalimu kuwa dokta nk
 
Kugoma c lazima uingie barabarani.....if u wanna know whether teachers wapo kwnye mgomo or what angalia perfomance ya wanafunzi ie std 7, form 4 and 6.
 
wote mhim,u, sema daktari kwa uchache wao na wengi kuwa more intellectual, na sifa ya kuuzika kila mahali, wakiamua kitu wanaweza, kwani wakitimuliwa, kesho utasikia yuko sehemu nyingine anapata zaidi ya huku alikofukuzwa. Walimu wengi hawauziki, akitimuliwa ualimu anaona ndo mwisho wa kila kitu. Hali hii imepelekea kuwa na mgogoro miongoni mwao, ambapo walimu wasiouzika huamua kurudi shuleni kuambulia hiyo 200,000/= kwa mwezi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom