DAKTARI AOMBA RUSHWA LAKI NA NUSU, wanawake laivu...

angekuwa mkeo au dadako ndo amepata fistula ungeongea haya unayoongea? au labda wewe ulipokuwa unazaliwa, maza ako ndo angepata fistula, ndo ungeishi na kukua ukiwa unaijua fistula ilivyo, na maneno haya yasingethubutu kutoka mdomoni mwako. hujui ulitendalo. hata kama watakuwa walipokea kofia na vitenge, au hata kama wangefanya chochote kila, our women don't deserve this kabisa. they really do not have to be treated that way. by the way, kuwa ccm au cdm ni uamuzi tu wa mtu, na hatupo vitani hapa, sio kwamba ukiona mtu yuko ccm basi unaomba mabaya yamkute hata apate shida kama iyo ndo furaha yako,....sidhani kama siasa za chuki kama wewe zitasaidia. zaidi ya yote usikute huyo mama ni mwanachadema au cuf, na wala si mwanasisiemu. angekuwa ameshafaidika na ccm angekuwa na laki na nusu atoe ili mtoto wake apone na asipate fistula. ukifuatilia utakuta hajafanya chochote kusapoti ccm na pengine ni mpiganaji mmoja wapo huko uswahilini.

kanga na kofia alipokea vimeshachakaa unakataa nini, we msemaji wake?
 
kusema kwamba madoctor wanafanya hivyo kutokana na uzembe wa selikali, si sahihi. tunakubali kabisa kuwa huduma au vitendea kazi ni vichache sana, lakini mshahara wa doctors tz, ukilinganisha na mishahara ya watz wengine ni average tu. si mbaya si nzuri sana. wanatakiwa kuridhika nacho na napinga kwa nguvu zote kwamba wao tu ndo wapendelewe kuliko fani zingine, pamoja na kwamba mshahara wao hata hivyo ni mkubwa kuliko wa wengine.

RUSHWA NI TABIA YA MTU BINAFSI ILIYOKO MOYONI MWAKE, hata wakipewa milioni tano kwa mwezi, rushwa watakula tu, maadamu wana roho zao mbaya, vifo vya wangojwa vitatokea tu. hii issue ilitokea sio leo, ni mwaka mmoja ulishapita hata kabla hawajaanza hiyo migomo ya mgogoro na serikali. hivyo usiingize kabisa hi issue na matatizo haya ya juzi...

kwa wale walioishi muda kidogo, hakuna ambaye hajui kuwa, ukienda hospitali za serikali lazima utoe rushwa ndo utahudumiwa vizuri na manesi au doctor. UTU NI KITU CHA MUHIMU SANA, hata kama umegombana na mtu, usimalizie hasira zako kwa mwingine. kama wao wanaona hawalipwi vizuri, asingemsababishia yule mama matatizo ya maisha vile...na kumpotezea mtoto wake wakati yeye doctor watoto wake wanapumua na kufurahia home....imagine kama mamake doctor au dadake ndo angepata fistula kwa kukosa laki na nusu? hivi kuna asiyejua kuwa sector ya hospitali ndo yenye rushwa kuliko hata mahakamani na polisi?.....cha ajabu, watu wengine wanawatetea madoctor wa aina hii, wakirusha lawama kwa serikali na kuwasafisha madotor. subirini wake zenu na dada zetu wapate fistula, ndo mtajua kuwa hawa madoctor ni mahanithi au la. na ashukuru mungu huyo mwenye mme alikuwa mtu wa uswahilini, mtu mwingine unamfanyia mkewe hivyo, lazima akutoe roho...wasifikiri wao ndo wametushika sana sisi wananchi viganjani mwao kwasababu wanatuchoma sindani...

utu ni nini?, wewe acha kutupotosha, tatizo lako unaangalia jirani sana, katika issue ya mishahara unakosea unapoangalia btn walimu, manesi,madaktari na watumishi wa kawaida wa umma,..laiti kama mshahara wanaojigawia mashirika makubwa ya umma kama TRA,TANESCO,TANAPA, BOT, Na wizara zote ungezidiana kwa kiasi kidogo kidogo na madaktari hawangekuja kulalamika wala kufanya migomo, haiwezekani waziri anapewa mil. 10 afu mwalimu anapewa laki 3 na dk anapew lak 7 cjui 9...huo ni uhuni...system ipo corrupt sana..sasa wenye akili wanagoma wenye akili afu waoga wanaumia,
 
watakaosoma comments zetu ndio watakaojaji nani ana ufahamu na nani alikimbia umande shule.

Mkuu Ubungoubungo, nitakuwa mtu wa ajabu kusubiri comments za watu "wakitujaji"...sidhani kama natafuta umaarufu, au kuwa judged etc..afterall hatujuani...okay, let's say "watujaji" then what? a trophy for it??am not interested in that unless you are!!!!

1.Ninachokisema unapotumia lugha ya kejeli na matusi hata huo ufahamu wako ninakuwa na mashaka nao, kwani as a great thinker sidhani hata kama ukiguswa namna gani kihisia unapaswa kujibu namna hiyo kwa comments zako hapo juu mkuu.

2. Ukiachana na matusi,kejeli na dharau umeongelea mambo mengi mfano incident ya mtu kupasuliwa vichwa na miguu, nk...lakini ingekuwa vizuri kufahamu kosa lilikuwa ni la nani na lilitokea..Then kuna suala la uwajibishwaji(Je ni sheria haikufuatwa?)..sasa kama watu waliwajibishwa kutokana na makosa yale ,mbona unarudiaha hilo suala kwa madaktari tena wakati uchunguzi ulifanyika kabla?!!!)

Kuna mengi umeongea katika comments zako ambayo si ya kweli mkuu wangu, and above all taking out of anger, so ninaposema kutokuwa na ufahamu, namaanisha ufahamu wa jambo KWA USAHIHI kabla ya ku-post, and not any other meaning you might interpret!
 
kuna kipindi cha wanawake laivu niliona siku moja, kuna ushuhuda wa mama mmoja alihojiwa hadi kiria akatoa mchozi.....kwa wale walioona na kusikia watakumbuka hili, ndo nilijiuliza hawa madoctor mbona hawana huruma?...mama mjamzito hadi alifikia kupata fistula, hadi leo hii, kwasababu ya laki moja na nusu. maelezo yalikuwa hivi....

1. MAMA alikuwa mjamzito, akaenda muhimbili, alipofika doctor akampima akasema kuwa asubiri kidogo mtoto ashuke.

2. mama alipoona mtoto ameshuka akamwita doctor na nesi, lakini walipokuja uchungu ukawa umepungua, si unajua uchungu huwa unakuja na kuondoka wakati mwingine.

3. ikafika kipindi doctor akamwambia mama aende nyumbani tu kwasababu uchungu wake hata zaa leo, au labda alete laki moja na nusu ili amzalishe...that means kulikuwa na possibility kuzalishwa laini si kwa mkono mtupu, laki na nusu.

4. mama alikuwa hana pesa hiyo, laki na nusu, ikabidi aondoke tu aende home. alipofika kwenye daladala, uchungu ukamkamata tena, akajifungua mle kwenye daladala..sijui yalikuwa magari ya mbagala siju wapi..nimesahau.

5. maisha yakaendelea, lakini kuanzia siku hiyo, wakilala tu bila kujijua mama alikuwa anastukia godoro limelowa. akikaa akisimama anakuta kiti kimelowa mkojo...mwanzo alikuwa hajui, alipoenda hospitali akakutwa amepata fistula, tena si ya kibofu cha mkojo tu, ni kwamba hadi ya rectum...utumbo mpana umechanika pamoja na kibofu hivyo kinnyesi pia kinatokea kwenye vvagina pamoja na mkojo mfululizo.

6. sijui ni kwasababu gani, yule mtoto alikaa miezi kadhaa akafariki, labda kutokana na kukosa huduma nzuri siku ile anajifungua mabarabarani mbele za watu na kwenye daladala. akawa amepoteza mtoto aliye mzaa kwa shida ya kukosa laki na nusu, na laki na nusu ikawa imemsababisia apate fistula ya haja kubwa na kibofu. hadi leo hii bado anaumwa fistula, na mtoto alishakufa.

7. hii ndo hali halisi, laivu bila chenga ya wanawake wetu wanapoenda huko hospitali.

8. kiria alienda hadi kwa doctor kumhoji, doctor alimwambia kuwa amemsahau yule mama hamkumbuki, mama kang'ang'ania kuwa "doctor umenisahau wakati uliniomba laki na nusu na kunirudisha home kwasababu sikuwa nayo?...wanabishana, doctor amemruka na akasema kama alikosea pengine ilikuwa kwasababu ya uchovu au ni makosa ambayo mwanadamu yeyote anaweza kuyafanya bila kukusudia ila hakumwomba laki na nusu.

9. nesi anaulizwa anasema, yap, alitakiwa ajitahidi, mkono mtupu haulambwi au la angeenda hospitali za kulipia huko, hakuna vya bure siku hizi, mbona mkienda hospitali za binafsi mnatoa hela nyingi hata iyo laki na nusu ndogo? nesi alifunguka ajabu hadi nilijiuliza alikuwa haoni kamera?

WHAT DO YOU THINK ABOUT THIS, na hawa ndo watu wanaoogoma na kutelekeza watu wafe, kumbe rushwa wanapokea sana na madawa yetu wanaiba sana...think about it, angekuwa ndo mke wako ingekuwaje? ungejisikiaje? utu wa mwanamke uko wapi hapa, hivi hata kama jamani wamekasirishwa ndo wafanye hivi kwa wamama wajawazito ambao wako nusu kuishi nusu kifi? kwani hata madoctor hawakuzaliwa na mwanamke? hawa jamaa ..duh...

fulani , alishatoa kibari kwamba LIWALO NA LIWE. liwalo- KUPOKEA RUSHWA NA KUACHA WATU WAFE , na liwe-watu kufa na kutoa rushwa. wataalamu wa afya wanatii agizo la waziri mkuu.
 
fulani , alishatoa kibari kwamba LIWALO NA LIWE. liwalo- KUPOKEA RUSHWA NA KUACHA WATU WAFE , na liwe-watu kufa na kutoa rushwa. wataalamu wa afya wanatii agizo la waziri mkuu.
yap, watatii agizo unalolishabikia hata kwa dada zako na ndugu zako. jiandae kunukishwa mkojo masaa 24 ya watu wako wa karibu. ndo utajua nini nilikuwa naongea hapa. yaani hata tuongee hadi kesho, there is no justification kwamba kwasababu serikali imeshindwa kutoa vifaa na mishahara mizuri kwa madaktari basi wao wanalipiza hasira zao kwa wananchi ambao hata hawajui ugomvi wa madoctor na serikali ukoje, hata huo mshahara anaopata doctor kwa mwezi wao wanaweza kukaa zaidi ya miezi sita hawajapata iyo hela. mwogopeni hata MUNGU TU, roho ya mtu ni muhimu kuliko pesa na hayo marupurupu. bora mfanya jambo litakaloiumiza serikali lakini si jambo litakalowaumiza raia wema wasio hata na hatia, hata iyo kauli ya liwalo na liwe hawakuongea wao. nashindwa kuelewa, watu wanaoshabikia hiki kitu ni wa chama gai...hicho chama mtu wa akili yako atakachokuwa anatoka, kinaaibishwa sana kuwa na mtu kama wewe unayefikiri unakipigania kumbe unachafua jila lake. kukiwa na maslahi ya raia wa tz tuweke vyama pembeni tukemee maovu.
 
madokta wa tanzania hasa muhimbili wanataka wakianza kazi tu wame matajiri kupitia kwa wagonjwa masikini. sasa fikiria wewe dokta uko kwenye gari yako umewasha kiyoyozi . harafu yule mama mwenye fistula yupo kituo cha daladala anasuburi daladala aende hospital kwa tatizo ulilomsababishia
 
yap, watatii agizo unalolishabikia hata kwa dada zako na ndugu zako. jiandae kunukishwa mkojo masaa 24 ya watu wako wa karibu. ndo utajua nini nilikuwa naongea hapa. yaani hata tuongee hadi kesho, there is no justification kwamba kwasababu serikali imeshindwa kutoa vifaa na mishahara mizuri kwa madaktari basi wao wanalipiza hasira zao kwa wananchi ambao hata hawajui ugomvi wa madoctor na serikali ukoje, hata huo mshahara anaopata doctor kwa mwezi wao wanaweza kukaa zaidi ya miezi sita hawajapata iyo hela. mwogopeni hata MUNGU TU, roho ya mtu ni muhimu kuliko pesa na hayo marupurupu. bora mfanya jambo litakaloiumiza serikali lakini si jambo litakalowaumiza raia wema wasio hata na hatia, hata iyo kauli ya liwalo na liwe hawakuongea wao. nashindwa kuelewa, watu wanaoshabikia hiki kitu ni wa chama gai...hicho chama mtu wa akili yako atakachokuwa anatoka, kinaaibishwa sana kuwa na mtu kama wewe unayefikiri unakipigania kumbe unachafua jila lake. kukiwa na maslahi ya raia wa tz tuweke vyama pembeni tukemee maovu.

UHAI- ni KITU CHA MSINGI kabisa. Usichanganye UHAI NA SIASA kwani havichanganyiki. fulani kiongozi mashuhuri alitakiwa KUACHA KUTUMIA SIASA ili kukomesha watu fulani. napenda sana uhai LAKINI sipendi CHAMA FULANI kama navyo penda uhai.
 
UHAI- ni KITU CHA MSINGI kabisa. Usichanganye UHAI NA SIASA kwani havichanganyiki. fulani kiongozi mashuhuri alitakiwa KUACHA KUTUMIA SIASA ili kukomesha watu fulani. napenda sana uhai LAKINI sipendi CHAMA FULANI kama navyo penda uhai.
kama wewe ulishawahi kufuga kuku..unajua kuku akiwa anaumwa mdondo? au akiwa anaharisha?...akili zake zinakuwa fupi kwelikweli. nachelea kukulinganisha wewe akili yako bora hata na ya kuku mgonjwa...umeongea nini sasa? kutopenda kwako ccm ndo justification ya kutoa roho za watu?...mwogopeni hata aliyewapa iyo kazi, asijekuichukua awape watu watakaowahudumia wananchi mkabaki walevi ombaomba vilabuni huko kama mlivyozoea kuiba madawa yetu kupeleka pharmacy na kunywa mipombe ovyo hadi mnapoteza fahamu kuamka mnakuta wenzenu wamewavua nguo za ndani na kuwaogesha uharo wa kilevi....mnawashukuru bila kujua kuwa mmeshapoteza ring....ndo maana madoctor wote walevi, tatizo lenu ndo hilo. hata ulimboka alitegewa mtego wake kwenye kilevi, kule bar, usiku ndo akanaswa, kwasababu akili zenu zimejaa ulevi na si utu.
 
Kinachosikitisha zaidi ni kuona kuna watanzania ambao hawana aibu kutetea unyama hadharani kabisa. Dhambi kama hizi kuzitetea ni kosa kubwa zaidi kuliko dhambi yenyewe...
 
KIUKWELI WHO na mashirika mengine ya afya yamesisitiza kua mimba sio ugonjwa na kusema akina mama wote wajifungue bure. Lakini ukiangalia kwa undani bado sera hiyo ngumu kutekelezwa katika nchi za africa. Hii nikutokana na uhaba wa vifaa na uhaba wa human resource kwa maternal health.
Mleta mada tuna shukuru kwa kutukumbusha wananchi kudai haki zetu za msingi. Japo ninashaka kuwa uchunguzi uliofanya haukuwa wa kina. Haikuelezwa kua laki na nusu iliombwa kwa nini. Navyo fahamu itakua kwa ajili ya kujifungua kwa njia ya upasuaji. Sasa sijui kama gharama ya kujifungua kwa upasuaji inafikia kiasi hicho.
Chamsingi hawa wahuskika wachukuliwe hatua...kama mama anachosema ni cha kweli.
Pole mama,usihofu utapata matibabu na kupona fistula.AMANI IWE NAWE
 
Kwa majibu anayotoa Ubungoubungo na wasi wasi sana na ufikiri wake, amepanic na anatoa matusi, jamani tusije kuwa tunasumbuana na form six leaver wa Perfect Vision ambaye anafungua Jf baada ya kuchezea Magame, hivi mods kwa nini msiweke kakipengere ka kuwajudge wanaojiunga Jf?..
 
Well kila mtu ataongea lake na kila mtu ana tabia yake.inawezekana hata wewe hupo ulipo unaomva rushwa.sisemi dr mwenzangu hakukosea kama mama kapata fistula that means kulikuwa na some signs of prolonged labour of which the doctor should have taken action but dont judge kwamba wote siye ni wala rushwa.
 
jambo ambalo mleta mada helewi ni kuwa hospital nyingi hakuna vifaa na dawa husika so inabid wajigarmie na ukipga mhesabu kama ni upasuaji si chini ya laki na kama kawaida yetu ccm imetudanganya huduma ni bure. mkiambiwa mkanunue vifaa mtasema ni rushwa..nch ya ks..ge hii.
 
jambo ambalo mleta mada helewi ni kuwa hospital nyingi hakuna vifaa na dawa husika so inabid wajigarmie na ukipga mhesabu kama ni upasuaji si chini ya laki na kama kawaida yetu ccm imetudanganya huduma ni bure. mkiambiwa mkanunue vifaa mtasema ni rushwa..nch ya ks..ge hii.

Kwa majibu anayotoa Ubungoubungo na wasi wasi sana na ufikiri wake, amepanic na anatoa matusi, jamani tusije kuwa tunasumbuana na form six leaver wa Perfect Vision ambaye anafungua Jf baada ya kuchezea Magame, hivi mods kwa nini msiweke kakipengere ka kuwajudge wanaojiunga Jf?..
form six leaver? kuna kitu gani cha kutoelewa hapa? ni kwamba rushwa iliombwa sio kwamba afanyiwe operation, ni rushwa yaani. hakuna asiyejua kuwa kuna subsidies kwenye hospitali wamama wajawazito wanahudumiwa bure, hata ukienda hizo za mission wanapata hiyo subsidy. kama labda ulikuwa hujaelewa ni kwamba iliombwa rushwa ya kawaida kabisa na wakati wa kipindi kiria alimfuata doctor na nesi akawahoji na doctor hakuongea chochote kuwa ilitakiwa amfanyie operation. kwa kifupi yule mama hakuhitaji uppasuaji ndo maana alijifungua hata kwenye daladala, ilikuwa ni roho mbaya tu ya doctor pale unapoombwa rushwa ukikataliwa unaamua kukomoa.sasa hayo mengine sijui yanaingiaje hapa.
 
jambo ambalo mleta mada helewi ni kuwa hospital nyingi hakuna vifaa na dawa husika so inabid wajigarmie na ukipga mhesabu kama ni upasuaji si chini ya laki na kama kawaida yetu ccm imetudanganya huduma ni bure. mkiambiwa mkanunue vifaa mtasema ni rushwa..nch ya ks..ge hii.
kwa mama mjamzito hakuna vifaa gani? laki na nusu ingenunua mipira na nyembe? ndo kisingizio chenu kumbe mnachukua rushwa kwa wagonjwa, mtu anaumwa halafu bado unao ujasiri wa kumkamua....mbona wamama wote wakienda hospitali kujifungua huwa wanaenda na ivyo vifaa, si mnawambia kabisa wakija clinic, na wanakuja wamejiandaa vifaa vyote wanavyo....ya nini sasa muwaombe rushwa? mabwabwa nyie.
 
Huyu daktari aliyefanya hicho kitendo alikosea sana, thats obvious na sitamtetea just because am also a doctor.
Lakini jamani, frustrations ni nyingi sana mahospitalini kwetu....... akili inachoka sana, mtu unawaza mambo mengi, na ukute nyumbani hali ya kipesa ni ngumu, una overload ya wagonjwa, kodi ya nyumba unadaiwa,unawaza kutoka hapo uende hospitali ya wahindi kpiga part time though akili imechoka na unataka sana kupumzika........ Mimi huwa nasali kila siku Mungu aniongoze sana nisitolee frustrations zangu kwa wagonjwa because i know ni vibaya sana......
Narudia, siungi mkono alichokifanya daktari mwenzangu, pole sana mama aliefanyiwa kitendo hiki
 
Mswahili anapoapa usimuamini kwa hiyo hata huyo dokta kiapo chake cha hypcratic hakina maana kabisa na kama nguo ya kuvaa kwani unaweza kuivua wakatai wowote ule na ndiyo maana tunasikia baadhi ya madaktari siku hizi kubaka wagonjwa.
 
Back
Top Bottom