Daktari anapomtibu mgonjwa anaesumbuliwa'kuchekacheka'

Faith

Member
Jul 9, 2008
52
11
Daktari asakwa kwa kumbaka mgonjwa

2008-08-12 11:13:27
Na Lulu George, PST Tanga


Daktari wa zahanati ya Manundu iliyoko katika Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka mgonjwa wake.

Daktari huyo aliyetambulika kwa jina moja la Mkenga, anadaiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 19 ambaye alikwenda katika zahanati hiyo kwa matibabu.

Akitoa taarifa hiyo ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Bw. Nyakoro Sirro alisema tukio hilo lilitokea Agosti 9, mwaka huu saa 6:00 mchana.

Kamanda Sirro alisema inadaiwa kuwa, siku ya tukio, msichana huyo ambaye ni mfanyakazi wa ndani, alifikishwa katika zahanati hiyo na mwajiri wake kutokana na kusumbuliwa na tatizo la kuchekacheka ovyo.

Hata hivyo, alisema baada ya mgonjwa huyo kupokelewa katika zahanati hiyo, daktari alimtaka mwajiri huyo aondoke na amwache mgonjwa kwa madai kuwa, tatizo lililokuwa likimsumbua ni dogo tu ambalo angeweza kulipatia tiba ya haraka.
Kwa mujibu wa Kamanda Sirro, mwajiri wake aliondoka na kurejea baada ya saa nne na kumkuta binti huyo akiwa ameacha kucheka cheka na hivyo waliondoka na kurudi nyumbani.

Hata hivyo, alisema binti huyo alianza kulalamikia kupata maumivu makali sehemu zake za siri akidai amebakwa na daktari wa zahanati alikopelekwa kwa tiba.

``Baada ya kufika nyumbani, inaonekana binti huyo alianza kulia maumivu makali na baada ya kuhojiwa na mwajiri wake ndipo alipoeleza kitendo alichofanyiwa hospitalini,`` alisema.

Alisema walienda polisi na daktari alipofuatwa kazini kwake, hakupatikana na inavyoelekea alitoroka.

Wakati huo huo, Khalfani Ali, mkazi wa kijiji cha Kiruku, Wilaya ya Tanga, anashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 anayesoma darasa la saba katika Shule ya Msingi Kiruku.

Kamanda Sirro alisema tukio hilo lilitokea Julai 30, mwaka huu saa 6:01 mchana katika kijiji cha Kiruku ambapo mtuhumiwa alimvizia njiani binti huyo wakati akitokea shuleni.

Alisema mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya polisi kukamilisha upelelezi.

SOURCE: Nipashe

http://ippmedia.com/ipp/nipashe/2008/08/12/120412.html

hii ni hatari kwa kweli au ndo alikua anamtibia?
 
Lakini si mgonjwa amepona..au? LOL


Mwanzo nilidhani hivyo pia.
Kwa kumchapa viboko angenyamaza pia. Hii haimaanishi amepona!


Huyu doctor inaonekana atatumia tranquilizer gun kwa mgonjwa anayekataa kuchomwa sindano.



.
 
Inachekesha sana . Jamaa huyu alimtamani kabla ya kumbaka nadhani aliunderestmate tatizo . Akipatikana ni adhabu kali hii inasikitisha ni lazima tukubali kwa ulimwengu wa sasa hivi hakuna wa kumwamini.
 
Kwa matibabu sampuli hii inabidi mabinti zetu tusiwaache peke yao na madaktari,huyu daktari anyongwe akipatikana,dunia imeharibika kama hata daktari haaminiki,its very sad
 
Aisee siku hizi madaktari wanatisha. Kuna dk mmoja wa Muhimbili alimbaka mgonjwa wa kike. Huyo dada alipelekwa na mumewe kusafishwa baada ya misacarriage, wenyewe wanaitwa DNC. Alimpa dawa ya usingizi ndipo akammega. Msichana alipotoka usingizini akaona shahawa kwenye K*** ndipo zilipopimwa zikaonekana ni za Dk. Kesi sijaifuatilia kujua imefika wapi lakini dk. bado yupo MMC anaendelea na kazi.

Kuna Dk mwingine bingwa wa matatizo ya akina mama na ana hospitali yake kule Mbezi Beach ana katabia ka kuwasugua kisimi wanawake wakati anawaexamine. sijui anataka kuwa-arouse ili awananihii!!!!???

Kuna Dk. mwingine Gyane wa hospitali moja Mikocheni anatabia ya kutongoza wagonjwa hata kama wana mimba ya miezi 6 na kuendelea

Jamani hawa madakatari sijui wana pepo la ngono?

Mimi mke wangu simpeleki kwa dk wa kiume kamwe!!!!!
 
Hata mi niliskia kuhusu huyo doctor wa muhimbili,pia miaka ya nyuma hapo hapo muhimbili doctor mmoja alimbaka mama alie pooza miguu kesi ilifika mahakamani na kwisha kienyeji
 
Mchola, ni kweli hili tatizo lipo. Mara ya kwanza nilisikia likiripotiwa sana nchini Marekani miaka kadhaa iliyopita. Matukio haya hapa kwetu hayakuwa yanaripotiwa. Mahakama inaweza kuamuru muathirika kulipwa mamilioni.


Cheki kwenye google.



.
 
HEBU TUENDELEE KUSHAURIANA. Ninaishi jirani na sekondari moja ya wasichana pekee, miaka kadhaa ya umri wangu wa sekondari( Im now aproaching 40) ugonjwa huu wa kucheka cheka ulikuwa ukiwapata wasichana hao wanafunzi na tiba iliokuwa ikitumika sana ni kuwaruhusu kutoka nje ya shule (Town live) kama kwenda shopping,nk na wakirudi shuleni ugonjwa huu ulikuwa ukipotea kabisa zaidi nadhani hii Mode ungeipeleka JF Doctor's
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom