daktari aliyeshiriki mgomo aelezea yaliomkuta kutoka vyombo vya usalama mkoani dodoma......so sad!

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
wakuu je ni kweli Tanzania tumefikia mahala hapa?kuwatisha na kuwadhalilisha wataalamu wetu?hebu sikia kisa cha madaktari walioshiriki mgomo katika ule mji unaotambulika kuwa ni makao makuu ya ccm na serikali na pia ni mji ambao mara kwa mara hupokea wawakilishi wa wananchi kutoka Tanzania nzima.nini maoni yetu juu ya hili???
Serikali ifahamu kuwa kutumia mabavu na nguvu kubwa kupita kiasi si njia ya kufikia suluhu,naomba madaktari popote tulipo tukemee kitendo kilichofanyika Dodoma na mimi kama muathirika,tulikamatwa kwa nguvu bila hata kupewa nafasi ya kuwaaga wenzetu,tumehojiwa kwa masaa tisa huku tukiwa tumefungiwa na maafisa upelelezi,tumepekuliwa majumbani tunakoishi na baadhi kuzuiliwa vitu vyao vikiwemo laptop,moderm,frash,tumechukuliwa finger prints na picha,na kupewa ratiba ya kureport ofisini kwao 4hrly na baadae kutapper down follow up kwa simu 4hrly na kuchukua taarifa zetu utafikiri wezi huu ni udhalilishaji wa taaluma yetu...
 
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kijiji cha Nyakaduha Wilaya ya Geita mkoani Mwanza, Aaron Yegela, ametiwa mbaroni kwa tuhuma za wizi wa dawa za binadamu zenye thamani ya Shilingi milioni mbili.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa na kuhojiwa kwa saa kadhaa na Jeshi la Polisi na baadaye kuachiwa kwa dhamana.
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuiba dawa zilizopelekwa kituoni kwake kutoka Hospitali ya Wilaya ya Geita kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa.
Kwa mujibu wa Polisi wilayani Geita, mtuhumiwa huyo amefunguliwa jalada la uchunguzi namba GE/223/RB/12 na baada ya kukamilika atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka.
Imedaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alifikishwa polisi na Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Omary Dihenga kufuatia ukaguzi uliofanywa na Mfamasia wa Wilaya, Ramadhan Msuya kwa kushirikiana na Katibu wa Afya wa Hospitali ya Wilaya ya Geita.
Uchunguzi huo uligundua upotevu wa dawa mbalimbali zikiwemo Quenine, Amoxilin, Aspirin, Panadol na chupa za maji (drips) ambazo katika uchunguzi huo, iligundulika orodha ya mgao wa dawa zilizokutwa kwenye Zahanati ya Nyakaduha zilikuwa tofauti katika uwiano wake, hivyo kulazimika kufanyika ukaguzi wa kushtukiza Desemba 21, mwaka jana.
 
kumbe siku hizi kudai haki yako kama mtaalamu ni sawa na kuwa mwizi wa dawa!!
 
Natarajia wakirudi kazini kukutwa na mikasa ya wizi wa dawa mfululizo maana wengi wamemisi hizzi dawa kwa muda
 
mafisadi wanaombwa kurudisha fedha lakini madaktari mweh ni vitisho,ubabe na dhihaka.
 
Itahitaji mtu akajilipue pale magogoni labda ndio hao watawala watakapoamka kwenye hilo lundo la usingizi walilonalo! Mpe pole daktari kwa huo unyanyasaji.
 
Natarajia wakirudi kazini kukutwa na mikasa ya wizi wa dawa mfululizo maana wengi wamemisi hizzi dawa kwa muda
tujiulize kwa nini waibe dawa je ni tabia au hali ngumu mifukoni mwao?
 
Maafisa usalama wote Tanzania hakuna mwenye shule wala akili.
wanahangaika na madaktari ila sijui walikuwa wapi Nchi ikihujumiwa kupitia iptl, Richmond, Epa etc.
walikuwa wapi Sokoine, Nyerere, Kolimba wakiuawa maybe wao ndio waliowaua.
Usalama wa taifa gani? hivi kati yao woote hakuna hata mwenye chembe ya uzalendo. tunajua akili hawana lakini uzalendo je?
 
hivi unategemea daktari huyu ataendelea kutekeleza majukumu yake kama kawaida?je hawa wanausalama walipata maelekezo kutoka kwa mizengo pinda au walijiamulia wenyewe?hili halikubaliki na lazima mtu awajibishwe.
 
kama waziri mkuu alituaminisha kuna wanajeshi wa kutosha kuziba pengo la madaktari waliogoma iweje sasa anawashurutisha madaktari kufanya kazi?akubali alipotoka katika kushughulikia mgomo wa madaktari.
 
ni matumaini yangu kuwa kamati iliyopewa jukumu kubwa la kushughulikia suala hili litawahoji madaktari waliofikwa na matatizo ya namna hii na pia kutoa tamko kali dhidi ya unyanyasaji huu.naamini kamati inapitapita humu jf ni wajibu wake kuangalia mambo yote yaliyotokea wakati wa sakata hili.
 
Mambo haya huwaga nayaona kwenye serikali za kidikteta duniani. With regard to my point our government is a dictatorship type. Hakuna demokrasia ya kweli Tz. CHADEMA chukueni nchii 2015.
 
Back
Top Bottom